Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili wakiume na wakike nyumbani kwa mganga wa kienyeji anayefahamima kwa jina la Abdulikarim mkazi wa Kimara baruti.

“January 12,2025 tulipata taarifa za kuibwa watoto wawili wadogo mmoja wa kike mwingine wakiume, mmoja Miaka mitano mwingine minne, dada wa kazi kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji Kimara walishirikiana kufanya kitendo cha kihalifu kuiba watoto”, SACP Jumanne Muliro, Kamanda Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam.

Aidha Watoto wote wamefanyiwa vipimo Afya zao ni njema na wamekabidhiwa kwa wazazi wao wakati shauri la watuhumiwa likisubiriwa kukamilika ili kufikishwa ✅
 
Awali isimbaa taarifa hii;

Asalam alykum warahmatullah wabarakatuh

Kwa majina naitwa Mohammad Kassim Naomba msaada wenu ndugu zangu kushare habari hii ya kuibiwa kwa watoto wawili Jana jioni tar 11/1/2025 majira ya saa 12

Aliowachukua watoto ni dada wa kazi aliekaa nao siku 3 tu (nadhani aliijia Hilo)

Tunaomba mtusaidie kushare kwenye groups na mitandao ya kijamii kadri muwezavyo dunia imekua mbaya sana hatujui watoto wana hali gani


hivyo msaada mkubwa tunahitaji No juhudi zenu kuendelea kusambaza habari hizi na kwa yoyote atakae sikia hizi habari au kuwaona watoto hao tunaomba


UWASILIANE:

+255 744 555 574

Au kutoa taarifa kituo cha police chochote kilicho karibu na wewe

👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻

 
Wapendwa Katika Bwana. Mungu ni Mwema kila wakati.

Naomba msaada wenu.
IMG-20250116-WA0032.jpg

Familia ya Alphonce Mutasingwa wa Bugene inawatangazia kupotelewa na Mtoto wao Danieli Edwini Mutasingwa. Aliondoka nyumba asubuhi ya tarehe 13/01/2025 na mpaka sasa hajarudi nyumbani.

Sura yake ni kama inavyoonekana katika picha hapo juu. Ana umri wa miaka 13 na yuko darasa la Saba. Tunaomba atakayemuona atoe taarifa kwenye kituo cha Police au kwa Simu namba 0755005692/0680491286/ 0789617281. Tunaomba pia mtusaidie kusambaza taarifa hii kwenye makundi mengine ya Whatsapp. Tunatanguliza Shukurani na Mungu awabariki sana.
 
Anaitwa Furaha Augostino Lukosi ni mkazi wa Kinyerezi Kifuru,Dar es saalam.

Alipotea usiku wa tarehe 27 April 2024 kuamkia 28 April 2024 alfajiri saa kumi.

Alipakia abiria kijiweni kwake Kifuru toka hiyo siku hajaonekena tena.

Umri wake ni miaka 23, familia yake imezunguka vituo vyote vya polisi na hospital bila mafanikio.

Mtu yoyote akimuona au akipata taarifa apige simu namba 0718024723,+255 653 319 772,ni Dada yake..."
View attachment 3035601
Dah inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom