Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
1. Katekwa na Polisi ili kuwatisha waropokaji. Polisi wamepelekwa mahakamani. Wamekana na kushinda kesi. Wako huru. Hawajamteka.
2. Katekwa na Chadema ili kuwasingizia polisi. Siku zimekuwa nyingi; polisi hawaogopi kusingiziwa. Umma unaamini ni polisi. Chadema wakimpoteza Soka moja kwa moja, itakula kwa polisi. Polisi wakishindwa kumwokoa Soka toka mikononi mwa Chadema, itakula kwao. Mpira uko eneo la goli la Polisi.
3. Ametekwa na wajanja wanaotumia jina la Polisi (Rogues). Kutokamatwa kwao ni hatari kwa kila mtu na kila taasisi. Wakiishazoea watateka viongozi wetu na kusababisha hali ya hatari. Watekaji wasiokamatika ni sawa na silaha moja kupotea kutoka ghala la silaha. Polisi wako lawamani katika nadharia hii.
4. Soka na wenzake wamejiteka ili polisi na chama cha watani wa jadi walaumiwe. Kazi mojawapo ya polisi ni kufichua waliojiteka. Kwa kujiteka ukafanikiwa kutokamatwa, wanaolaumiwa ni polisi. Sifa moja ya Polisi na serikali ni kuwa na MKONO MREFU. Nani kaukata ukawa mfupi usimkamate Soka aliyejiteka?
5. Soka ametekwa na chama cha watani wa jadi wa Chadema kwa sababu Soka ni Chadema. Kwa kuwa kuna mzimu “unawaroposha” wanachama wa chama hicho kukiri utekaji; Polisi wana ushahidi wa mazingira kuwatumia watopokaji kuisaidia polisi. Asipopatikana si kosa la chama kilichoteka. Ni kosa la taasisi inayojihusisha na kuzuia utekaji. Bado Polisi hawajachomoka. Niwasaidieje?
Mpaka hapa, naweza kusema, aliyemteka Soka na wenzake, ameiteka polisi maana nadharia 4 kati ya 5 zinagota kwa polisi. Nani aikomboe polisi kutoka mikono ya watekaji?
Tumewahi kuuona mkono mrefu wa Polisi ukiwa kazini. Majuzi tu, ndani ya masaa 24, waliomuua Binti Asiimwe mwenye ualbino walikamatwa.
Tumesikia habari za mganga wa kienyeji aliyezika watu. Tunaogopa tusijeambiwa akina Soka wako humo. Kwamba walienda kupiga ramli chonganishi