Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
#HABARI: Mwili wa mtu mmoja wa jinsia ya kike ambaye jina lake halijafahamika, umekutwa ukielea na kuopolewa ukiwa umeharibika, katika bwawa la Mbimba linalotumika kwa shughuli za umwagiliaji, lililopo kandokando ya barabara kuu ya Tanzania Zambia wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Chanzo: ITV
 
09 Agosti, 2024

TAARIFA KWA UMMA

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UTEKAJI NA UPOTEAJI WA WATU NCHINI

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinasikitishwa na kinalaani vitendo vya kukamatwa, kutekwa na kuteswa kiholela kwa wananchi kunakoendelea nchini bila ya vyombo husika vya dola kuwajibika ipasavyo.

Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za watu kupotea katika mazingira tatanishi, kutekwa na kuteswa na baadae kuonekana huku baadhi yao wakiwa wamefariki na wengine wakiwa na majeraha makubwa katika miili yao. Tunasikitishwa pia na namna ambavyo vyombo vyetu vya dola hususani Jeshi la Polisi limekuwa likifanyia kazi taarifa hizo. Mara kwa mara Jeshi la Polisi limekuwa likikanusha kutokea kwa matukio hayo lakini baadae inakuja kubainika kwamba matukio hayo ni ya kweli. Mara nyingine Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata raia wema wanaotoa taarifa hizo kwa kile kinachosemekana kusambaza taarifa za uongo badala ya kufanyia kazi taarifa hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinazowapasa kufanya wajibu wao wa kulinda watu na mali zao.

TLS, kwa mamlaka iliyopewa kupitia kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002), inapenda kuvikumbusha vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi juu ya majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria ya kulinda watu na mali zao. Matukio haya ya utekaji ni kinyume na Ibara ya 13 (6) (e) na 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; pamoja na Mikataba ya Kimataifa inayozungumzia Haki za Binadamu na inayozuia uteswaji wa watu kama vile Mkataba dhidi ya Mateso na Unyanyasaji au Adhabu Nyingine za Kikatili au Udhalilishaji (Convention against Torture and Other Cruel, Inhuman or Degrading Treatment or Punishment), Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (The International Covenant on Civil and Political Rights).

TLS inatambua na kuheshimu taarifa za Jeshi la Polisi zinatolewa zikitaarifu umma kwamba matukio hayo yamekuwa yanafanyiwa uchunguzi lakini tunasikitika kwamba hakuna taarifa kamili ya uchunguzi wa tukio hata moja ambayo imewahi kutolewa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi juu ya watuhumiwa wa matukio hayo. Hali hii inaendelea kutia hofu kwa wananachi juu ya usalama wao na mashaka juu ya uwezo wa Jeshi la Polisi kuchunguza na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wa matukio hayo.

Kupitia tamko hili, tunaambatanisha orodha ya baadhi ya watu ambao wananchi au/na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimewahi kutoa taarifa za kupotea au kutekwa kwao ambapo baadhi yao walipatikana na baadhi yao wakiwa na majeraha huku kukiwa na wengine ambao waliopotea katika mazingira tatanishi na hawajapatikana mpaka leo. Tunaamini kwamba Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vitafanyia kazi na kuhakikisha watu hao wamepatikana na wahusika wote wa matukio haya wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo husika vya haki ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Wito wetu;

Tunamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume maalumu ya kuchunguza matukio yote ya kupotea kwa watu, kutekwa na kuteswa;

Tunamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume Maalum ya kuchunguza ushiriki wa Jeshi la Polisi kwenye masuala ya Utekaji kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likituhumiwa kushiriki katika vitendo hivyo;

Tunapendekeza kuundwa kwa chombo maalumu cha kudumu cha kuangalia utendaji wa vyombo vya dola (oversight body) ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa mujibu wa

Katiba na Sheria; na

Tunalitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi yake kwa weledi kwa mujibu wa Katiba na Sheria ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi na mali zao unaimarika

TLS inaendelea kufuatilia matukio haya kwa ukaribu na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika kuhakikisha wahusika wote wa matukio haya wanafikishwa katika vyombo mahususi vya haki ili haki ionekane inatendeka. Hata hivyo, tunatoa rai kwa watanzania wote kuwa makini wakati wote na kutokubali kuitwa au kukutana na watu wasiowajua au kwenda mahali wasipopajua na ikibidi sana wawasiliane na wakili yeyote kabla ya kukutana au kwenda mahali wasipopajua.

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Boniface A.K Mwabukusi

Rais

KIAMBATISHO:

ORODHA YA WATU WALIOTEKWA/KUPOTEA 2016-2024.

S/N
JINA
MAELEZO MAFUPI
MAKAZI
1.​
KOMBO MBWANA TWAHA​
Alitekwa nyumbani kwake Handeni Tanga na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 15 Juni 2024, baadaye polisi walikanusha kuhusika na kufungua jalada la uchunguzi. Siku 29 baadaye polisi walikiri kuhusika na kumshikilia kwa hizo siku zote.
Handeni - Tanga​
2​
KENNEDY MWAMLIMA​
Alitekwa Mbeya na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 11 Aprili 2024. Alipatikana Igunga Tabora Tarehe 16 Aprili 2024 akiwa ametapakaa majeraha. Kwa maelezo yake alikuwa akiteswa katika vituo vya polisi na alikuwa akiulizwa nani anamtuma kukosoa serikali katika mtandao wa TikTok.
Mbeya Jiji -Mbeya​
3​
EDGER MWAKALEBELA​
Alitekwa tarehe 23 Juni 2024 Ubungo Dar es Salaam.
Akapelekwa kituo cha polisi
OysterBay na baadaye​
Arusha kabla ya kupatikana tarehe 27 Juni 2024 mkoani Katavi porini akiwa ametapakaa majeraha.
Dar es Salaam.​
4​
JAMES SIJE​
Alitekwa na askari polisi anayeitwa Sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi Nyakato tarehe 17 Agosti 2021 mpaka sasa hajapatikana.
Nyakato –Mwanza​
5​
JOSEPH MNYONGA​
Alitekwa Julai 2021 nyumbani kwake Mwanza na watu waliojitambulisha kuwa
Mwanza.​

ni askari polisi kutoka mkoa wa Mwanza mpaka sasa hajapatikana.
6​
DOTTO KABWA​
Alitekwa tarehe 4 Julai 2022 na askari polisi anayejulikana kwa jina la Wambura Mwita kutoka kituo cha polisi Ifunda Iringa na hajapatikana mpaka leo.
Ifunga-Iringa​
7​
YAHYA ALLY​
Alitekwa tarehe 6Septemba 2022 Mbagala Kizuiani na askari polisi wakiongozwa na OC-CID Abdalah Suleiman.
Mpaka sasa hajapatikana.
Mbagala – Dar es Salaam.​
8​
CHANDE KIZEGA​
Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 18 Agosti 2022 akiwa dukani kwake Machinga Complex. Mpaka sasa hajapatikana.
Dar es Salaam​
9​
Mzee SAMUEL MKONGO​
MATIKOAlitekwa mkoani Geita tarehe 27 Januari 2023 na askari polisi Sgt. Hamis mwenye namba 0789938835 na kupelekwa kituo cha Muriaza –Butiama mkoani Mara. Ndugu walifika hapo na wakamuona akiwa ametapakaa majeraha, lakini waliporudi kumletea chakula hawakumkuta tena kituoni hapo na hajaonekana mpaka leo.
Geita mjini.​
10​
CHARLES
MWAMPYATE​
ADEN​
Alitoweka tangu tarehe 7 Decemba 2023 akiwa Dar es Salaam na hajapatikana mpaka leo.
Dar es Salaam.​
11​
WILLIAM HERMAN​
Alitekwa Mwanza tarehe 1 Januari 2024 na askari polisi anayefahamika kwa jina la Sgt. Mageni Musobi A.K.A
Kangaye-Mwanza​

Majani wa kituo cha polisi Nyakato.
12​
DAVID GASPER LEMA​
Alipotea akiwa njiani kutoka
Mwanza kwenda Dar es​
Salaam tangu tarehe 6 Aprili 2024 na mpaka sasa hajapatikana.
Mwanza​
13​
JEROME KISOKA a.k.a MAPII​
Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 14 Novemba 2023 eneo la Njoro, Moshi mkoani Kilimanjaro na hajapatikana mpaka leo.
Moshi-Kilimanjaro​
14​
RIDHIWANI HEMED MSANGI
(PIA AMEKUWA​
AKIJULIKANA KWA JINA LA
ABDALLAH SALUM MSANGI)​
Alipotea mkaoni Iringa mwishoni mwa mwezi Julai 2021 na hajapatikana mpaka leo. Kazi yake alikuwa mhadhiri (Lecturer) Chuo Kikuu cha Mkwawa ambalo ni tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Iringa​
15​
BENSON E.A. ISHUNGISA​
Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 26 Novemba 2023 akiwa nje ya Hospital ya Makangarawe Yombo mkoani Dar es Salaam. Benson alikuwa akimsubiri abiria nje ya Hospital hiyo na hata bodaboda wenzake walipoulizwa kituo cha polisi anachopelekwa hawakujibiwa. Mpaka leo hajapatikana.
Dar es Salaam​
16​
HAMZA SAID​
Katibu wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Geita. Alitekwa tarehe 17 Decemba 2023 nyumbani kwake mtaa wa Mwatulole mkoani Geita na watu waliojitambulisha ni askari polisi. Mpaka leo Katibu huyo hajapatikana
Mwatulole-Geita​

17​
YONZO SHIMBI DUTU​
Alikamatwa tarehe 2 Machi 2024 na askari polisi wa kituo cha polisi Kwimba Mwanza akiwa na wenzake maeneo ya Bushini-Kishapu mkoani
Shinyanga. Wenzake waliachiwa ila yeye hajapatikana na hayupo vituo vyote vya polisi.
Kishapu-Shinyanga​
18​
LILENGA ISAYA LILENGA​
Alitekwa tarehe 11 Mei 2024 maeneo ya Kibirizi mkoani Kigoma na watu wanaodaiwa ni polisi kisha kutokomea naye kusikojulikana. Mpaka sasa hajapatikana.
Mwandiga-Kigoma​
19​
TAWAFIQ MOHAMED​
Alitekwa tarehe 26 Decemba
2021 eneo la Kamata,​
Kariakoo mkoani Dar es Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana.
Dar es Salaam​
20​
SELF SWALA​
Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es
Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana.
Dar es Salaam​
21​
EDWIN KUNAMBI​
Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es
Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana.
Dar es Salaam​
22​
HEMED ABASS​
Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es
Dar es Salaam​

Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana.
23​
RAJABU MDOE​
Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es
Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana.
Dar es Salaam​
24​
MZEE HAJI SOFT​
Alichukuliwa nyumbani kwake Temeke na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 13 Julai 2021 na mpaka sasa hajapatikana.
Temeke – Dar es
Salaam​
25​
ALPHONCE BILASENGE​
Alitoweka ghafla. Simu yake mara ya mwisho ilizimwa eneo la Kibeta, wilaya ya Bukoba mjini mkoani Kagera tarehe 6 Januari 2022.
Kagera​
26​
ALBERT KISEYA SELEMBO​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi akiwa na kesi ya Mauwaji.
Loliondo - Arusha​
27​
MOLOIMETI YOHANA
SAING’EU​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha Polisi akiwa na kesi ya Mauwaji.
Loliondo - Arusha​
28​
NDIRANGO SENGE LAIZER​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022
Loliondo - Arusha​

wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
29​
JOEL CREMES LESSONU​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
30​
SIMONI NAIRIAM
OROSIKIRIA​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
31​
DAMIAN LAGO LAIZER​

32​
MATHEW ELIAKIMU SILOMAAlitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​

33​
LUKAS K. NJAUSI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
34​
TALENG’O TWAMBEI
LESHOKO​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
35​
KIJOOLU KAKEI OLOJILOJI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo – Arusha​
36​
SHENGENA JOSEPH KILLEL​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo Arusha​
37​
MASEKE MWITA MASEKE​
Alitoweka tangu tarehe 10 Juni 2022 mpaka sasa hajapatikana.
Nkerege -Tarime- Mara​
38​
MALONGO DANIEL PASCHALAlitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya
Loliondo - arusha​

serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
39​
SIMELI PARMWATI
KARONGOI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
40​
INGOI OLKEDENYI KANJWEI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
41​
SANGAU MORONGETI
NGIMINIS​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
42​
MARIJOI NGOISA PARMATI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​

43​
MORONGETI MASAKO​
MSEEKIAlitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
44​
KAMBATAI LULU​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
45​
ORIAS OLENG’IYO​

Loliondo -Arusha​
46​
WILSON KOLONG​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 12 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
47​
JAMES TAKI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 13 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye
Loliondo - Arusha​

aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
48​
JOSEPH JARTAN​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 13 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
49​
KELVIN SHASO NAIROTI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
Loliondo - Arusha​
50​
LEKERENGA KOYEE ORODO​

51​
FRED VICTOR LEDIDI​

52​
SIMON MORINTANTI​
Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa
Loliondo - Arusha​

nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi.
53​
MOHAMED KAYEGO KALEBEAlikamatwa na watu wengine sita (6) na maafisa waliojitambulisha kuwa ni askari polisi tarehe 5 Apriil 2023 huko Katoro mkoani Geita. Ndugu walifika vituo vyote vya polisi hawakumkuta na hajapatikana mpaka leo yeye na hao wenzake ambao majina hayajatambulika mpaka sasa.
Katoro - Geita​
54​
AMON MRIGI MAGIGE​
Alikamatwa na askari wa jeshi la Polisi wakiwa na gari za Polisi Land Cruiser Pick Up mbili hapo tarehe 1 Octoba
2023. Mpaka sasa hajapatikana na hayupo kituo chochote cha polisi wala gerezani.
Mwanza​
55​
AZIZ KINYONGA​
Alipotea siku kadhaa, kwa maelezo ya mke wake anasema baada ya mume wake kupotea siku kadhaa baadaye ilifika gari aina ya Toyota Noah na ndani ya ile gari alionekana mtu akinyosha kidole kuonyesha nyumba yao. Mke anasema hakujua ni mume wake. Anadai walishuka watu waliojitambulisha ni askari walikagua nyumba wakakuta kuna laki mbili wakachukua na kuondoka. Baadaye gari ya mume wake Aziz lilikutwa limetelekezwa mkoani Mtwara. Hajapatikana tangu tarehe 1 Februari 2023.
Chamazi – Dar es Salaam.​

56​
YUSUPH DUDU​
Alitekwa nyumbani kwake na watu wenye silaha waliojitambulisha ni polisi.
Watu hao walipofika nyumbani kwa Yusuph walimkuta mtoto wake mwenye miaka 8 wakamwambie kamwite baba yako na kisha Yusuph alivyofika walijitambulisha ni askari polisi na kuondoka naye tangu tarehe 9 Aprili
2024 mpaka sasa hajapatikana. Jarada la uchunguzi la kupotea kwake limefunguliwa kituo cha polisi Mbagala Maturubai MBL/RB/2891/2024.
Mbagala – Dar es Salaam​
57​
KASTORY KAPINGA​
Mwanafunzi wa chuo cha SAUT, kituo cha Arusha mwaka wa tatu alipotea akiwa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili 2024. Hajapatikana mpaka sasa.
Ruvuma - Mbinga​
58​
DIONIZ KIPANYA​
Alitoweka tangu tarehe 27 Julai 2024 huko Sumbawanga mkoani.
Hajapatikana mpaka leo.
Sumbawanga- Rukwa​
59​
SHADRACK CHAULA​
Alitekwa tarehe 2 Agosti 2024 kijijini kwao Ntokela, wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Siku 20 kabla ya kutekwa Shadraka Chaula alitolewa jela kwa michango ya watanzania walioamua kumlipia faini baada ya kufungwa jela au kulipa faini kwa kosa la kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Ntokela – Rungwe – Mbeya​

60​
PROSIPER THEONAS MNJARIAlitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa Polisi na walikuwa wameongozana na watumishi wa TANESCO. Watekaji wao walisema nyumba yao ina deni kubwa sana la umeme yeye akajibu kuwa ni mpangaji tu awaunganishe na mwenye nyumba lakini walikataa na kuondoka naye mpaka sasa hajapatikana.
Chamazi – Dar es Salaam​
61​
THOMAS MUNGO IHUYA​
Alikuwa anafanya kazi Mahakama kuu Mwanza alipotea tangu March 2018 mpaka leo hajapatikana.
Mwanza​
62​
DENNIS KANTANGA​
Alikuwa mkazi wa mkoa wa Shinyanga Mjini na alikuwa akifanya shughuli za TEHAMAkwa maana ya kutengeneza na kuuza computers, desktop pamoja na laptops na vifaa vingine vya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo CCTV. Siku anachukuliwa alifuatwa dukani kwake na watu wawili au zaidi lakini waliofika dukani walikuwa wawili na kujitambulisha kuwa ni askari. Waliondoka kwa gari yake mwenyewe(Dennis) na ikawa mwisho wa kusikikika kwake. Katika utaratibu wa kuripoti polisi na kutrack simu ilionekana simu yake iliwashwa wilayani Musoma mkoani Mara na baada ya hapo haikupatikana tena. Gari yake ilikuja kupatikana maeneo ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa imeegeshwa katikati ya mji
Shinyanga​

baada ya wiki moja. Ni miaka 4 sasa imepita toka kutoweka kwake.
63​
Damas Vedastus Bulimbe​
Alipotea tarehe 15 Novemba 2023 huko Geita.
Hajapatikana mpaka leo.
Geita​
64​
Lucas Magambo Bulimbe​
Alipotea tarehe 15 Novemba 2023 huko Geita.
Hajapatikana mpaka leo.
Geita​
65​
Matuki Makuru​
Alitoweka tarehe 15 Februari 2024 wilayani Serengeti mkoani mara. Hajapatikana mpaka leo.
Serengeti, Mara​
66​
Dastan Gervas Nestory​
Alitoweka tarehe 9 Julai 2024 huko Mkoani Geita.
Hajapatikana hadi sasa.
Geita​
67​
Adinan Hussein Mbezi​
Alitoweka tarehe 16 Septemba 2023 huko mkoani Geita. Hajapatikana hadi leo.
Geita​
68​
Lengaripo Lebahati Lukumay​
Alitoweka tarehe 7 Mei 2021 huko mkoani Mwanza.
Hajapatikana hadi sasa.
Mwanza​
69​
Akidu Twaha Salim​
Alitoweka tarehe 6 Oktoba 2023 mkoani Dar es Salaam.
Hajapatikana hadi sasa.
Dar es Salaam​
70​
Enock John Chambala​
Alitoweka tarehe 6 Julai 2024 huko mkoani Tanga.
Hajapatikana hadi sasa.
Tanga​
71​
Dioniz Kipanya​
Alitoweka tarehe 26 Julai 2024 huko mkoani Katavi.
Hajapatikana hadi sasa.
Katavi​
72​
Nusra Omari​
Alitoweka tarehe 7 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam.
Alipatikana akiwa amefariki.
Dar es Salaam​
73​
Theresphora Mwakalinga​
Alitoweka tarehe 17 Julai 2024 huko mkoani Dodoma.
Alipatikana akiwa amefariki.
Dodoma​
74​
Donald Kalist Mboya​
Alitoweka tarehe 29 Juni 2024 huko mkoani Kagera.
Hajapatikana hadi leo.
Kagera​
75​
Ilham Makoye​
Alitoweka tarehe 2 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam.
Alipatikana baadae.
Dar es Salaam​
76​
Barack Majigeh​
Alitoweka tarehe 5 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam.
Hajapatikana hadi leo.
Dar es Salaam​
77​
Joshua​
Alitoweka tarehe 5 Julai 2024 huko mkoani Iringa.
Hajapatikana hadi leo.
Iringa​
78​
Yusra Musa​
Alitoweka tarehe 9 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam.
Alipatikana akiwa amefariki.
Dar es Salaam​
79​
Angel Albert Kamugisha​
Alitoweka tarehe 15 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam na baadae kupatikana.
Dar es Salaam​
80​
Brighton Amos Emmanuel​
Alitoweka tarehe 16 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam na kuja kupatikana baadae.
Dar es Salaam​

81​
Azory Gwanda​
Alitoweka tarehe 17​
Novemba 2017 Kibiti mkoani Pwani na hajapatikana hadi leo
Pwani​

82​
Ben Saanane​
Alitoweka tarehe 15 Novemba 2016 Dar es
Salaam na hajapatikana hadi leo​
Dar es Salaam​

83​
Simon Kanguye​
Alitoweka tarehe 20 Julai 2017 Kigoma na hajapatikana mpaka leo.
Kigoma​
 
Salaam Wakuu,

Nimeanzisha uzi huu ili tushikamane kama Watanzania kutafuta au kutoa taarifa ya watu waliopote. Kumeibuka wimbi la Watu wa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Rais ndo Mwenyekiti wa kwanza wa usalama, kupitia thread hii ataweza kujua ni kiasi gani watu wanapotea bila hatua zozote kuchukuliwa.

Pili nashauri Polisi kama kuna mtu wamemkamata, watoe taarifa mapema kwa ndugu na jamii ili wajue yupo Mikono salama. Hapa chini naweka baadhi ya watu ambao wamepotea, post zao au Malalamiko ya ndugu zao.

Hivyo usikalie kimya hili tatizo la watu kupotea. Tujulishane ili Mamlaka zione tatizo lilivyo kubwa.

Karibuni.

Pia soma ===>>> Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

=====

BAADHI YA MICHANGO YENYE TAARIFA ZA KINA KUHUSU ORODHA YA WATU WALIOPOTEA
Hali ni mbaya sana, hali Kama hii ilikuwepo nchini Zaire (Congo DRC) enzi za Utawala wa Dikteta Mobutu Seseseko. Watu wengi waliokuwa wanakosoa Utawala wake walitekwa, kuuawa au kupotezwa kabisa na hawajawahi kupatikana hadi leo. Baadhi ya Watu wakosoaji waliobahatika Mapema kupewa taarifa za kutekwa kwao waliitoroka nchi hiyo ili kunusuru uhai wao.
Kumkosoa Rais Mobutu Seseseko ilikuwa ni kujikatia tiketi ya kifo. Naona hali kama hiyo Sasa ipo nchini Tanzania.
 
Rais ingilia kati hili kuna mtandao wa hujuma kwako. Polisi ifumuliwe yote kuanzia Waziri. Hii hatari kwa usalama wa Raia!
 
Rais ingilia kati hili kuna mtandao wa hujuma kwako. Polisi ifumuliwe yote kuanzia Waziri. Hii hatari kwa usalama wa Raia!
Hana huo muda unaweza Kuta na yeye amebariki haya Kwan umeona lini ametoa tamko kulaani?
 
AMEPOTEA AMEPOTEA AMEPOTEA

Anaitwa GIDEON MLOKOZI MASHANKARA ana umri wa miaka 30,mkazi wa Tabata Segerea,

Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.

Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la Polisi siku ya Ijumaa ya tarehe 02 August 2024 majira ya Saa 2 :00 usiku.

Akiwa katika ofisi ya magari ya rafiki yake inayojulikana kama RAPHAEL STAR iliyopo maeneo ya Segerea Stand.

Watu hao waliojitambulisha kama askari wa Jeshi la polisi walikuwa watano,walivamia ofisi hiyo wakiwa wamevalia kiraia na kumuweka Chini ya ulinzi.

Ndipo alipowahoji waoneshe vitambulisho lakini wakakaidi na kudai wanampeleka kituo cha polisi Tabata,atajua huko huko.

Walitumia nguvu na kumfunga pingu kisha wakamuingiza kwenye gari walilokuja nalo aina ya Landcruiser hardtop, ikiwa haina namba

Lakini mashuhuda waliokuwa nje ya ofisi wanasema,gari hilo halikuwa na namba kwa nyuma ila kwa mbele liliandikwa "STL" tu.

Gari hilo halikuelekea Kituo cha polisi Tabata kama walivosema bali lilielekea njia ya kwenda kinyerezi.

Familia ilianza juhudi za kumtafuta vituo vyote vya Polisi Jijini Dar es saalam bila mafanikio

Tulianza kituo cha polisi Tabata, tukaambiwa hayupo na hawana taarifa zake,Tukaenda kituo cha polisi cha Staki Shari,Kinyerezi na Buguruni pia hawakuwa na taarifa zake

Kesho yake asubuhi tuliendelea na vituo vingine tulianzia Central, Oysterbay na vituo vyote bila Mafanikio

Tumezunguka Hospitali zote jijini Dar es saalam na vyumba vya kuhifadhia maiti "Mortuary" bila Mafanikio.

Tulifungua taarifa kituo cha Polisi cha Staki Shari na kupewa RB namba STK/RB/6642/024

Baada ya siku ya tano bila Mafanikio tumeenda Central polisi kufungua jalada la Uchunguz,tumeambiwa upelelezi unaendelea.

Kwa niaba ya Familia tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa kuhusu ndugu yetu awasiliane na Baba yake GIDEON kwa namba 0786878133 au kwa namba ya rafiki yake ambayo ni 0624497811

Asante sana.
IMG-20240829-WA0034.jpg
 
View attachment 3082373
Tuache masihara, kwa kweli hali siyo shwari hata kidogo.
Hali ni mbaya sana.
 
Nina amini kwa dhati ya moyo hatuna mada maalum na jumuishi ya hii taharuki kubwa iliyoikumba Tanganyika ya watu kupotea ama kwa viashiria vya kutekwa ama kupoteana katika mazingira tatanishi
Kwa mwaka jana na mwaka huu inasemekana kwa majibu wa X mayor Jackob aka Boni Hai kuna Watanganyika si chini ya 100 ambao

Ama walitekwa ama walipotea katika mazingira tatanishi kati yao hao Wote ni wachache mno wamepatikana wakiwa hai na salama. Wamepatikana wakiwa hoi na majeruhi wamepatikana milili yao wakiwa marehemu ama mabaki ya miili yao!

Mada hii maalum inaangazia waliotekwa ama kupotea kwa sababu za kisiasa wakiwa ni wahanga wa ukosoaji wa utawala uliopo madarakani. Ni vema na ni jukumu letu JF kama sehemu ya jamii ya Tanganyika kuonesha mshikamano kwa kuwa na mada kama hii.

Kuna simulizi za wahanga waliosalimika katika mazingira ya kudra za Mwenyezi Mungu kuna simulizi za ndugu na jamaa walioshuhudia ndugu na jamaa zao wakitekwa na kuchukuliwa kusikojulikana Kuna simulizi za wahanga kabla ya kutekwa na kupotezwa.

Zote zinatisha, kuogofya na kutia simanzi mno! Mojawapo ya simulizi ni ile mhanga mmojawapo aliyekaa na kitambaa usoni 24/7 kwa miezi mitatu mfufulizo alivyoshuhudia vijana wengine wengi wakiwa katka hali hiyo kwenye gereza la siri lisilojulikana liko wapi.

Simulizi nyingine ni ya yule aliyesalimika risasi ya kisogo katikati ya pori lenye wanyana wakali Mpaka sasa haijulikani ni Watanganyika wangapi walitekwa na wanashikiliwa kwa siri maeneo gani, na nani na kwa ufadhili wa nani.

Mpaka sasa haijulikani kwa hakika Ni wangapi wako hai bado bila mateso Ni wangapi wako hai lakini wakiwa kwenye mateso makali. Ni wangapi wako hai lakini ni majeruhi wa majeraha makubwa ni wangapi wako hai lakini wameshapata ulemavu wa maisha.

Ni wangapi ni wafu lakini makaburi yao yapo ama miili yao bado ipo kwenye mochwari za hospitali mbalimbali
Ni wangapi ni wafu na miili yao haitakaa ionekane ama kupatikana milele kwa kifupi hali ni tete, inatisha, inaumiza na taharuki ni kubwa sana na hofu pia imetamalaki.

Mtandao wa X usiku wa jana wali host kipindi maalum kilichokuwa kinayajadili haya yote na the way forward..! Kipindi kimeisha saa saba usiku leo hii. Kwa yaliyokuwa yanazungumzwa hali ni ngumu na inatisha sana

Kuna swali muhimu sana la kujiuliza! Je watasalimika wangapi? Mamlaka zetu kupitia watendaji wake ni watu wa imani mbalimbali. Ni washika dini, ni wazazi, ni ndugu, ni jamaa. Wana nafasi kubwa kukomesha huu utekaji na upoteaji wa watu wa Tanganyika.

Wana nafasi kubwa kuwaachilia mateka wote wana nafasi kubwa kuwawajibisha wote wsliohusika na uovu wowote uliotokana na kuteka kutesa na kuua, wana nafasi kubwa ya kuondoa, hofu na taharuki iliyotamalaki Tanganyika na kuwahakikishia watanganyika usalama wao.

Soma Pia: Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”

Ni ngumu sana kuwalinda mateka.. Mateka si mahsbusu ama mfungwa wanaowekwa sehemu zinazojulikana na wote. Mateka hufichwa na kulindwa kwa mitutu 24/7

Je tuna jela za siri nje ya mfumo Tanganyika? Je tuna vyumba vya siri Tanganyika visivyo rasmi? Je tuna watesaji na wauaji wenye mafunzo rasmi lakini nje ya mfumo? Je ni Watanganyika?
NAOGOPA SANA..!
 
#TANZANIA: MAHAKAMA YAFUNGA DHAMANA YA KOMBO, AENDELEA KUSOTA RUMANDE TANGA
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz) mkoani #Tanga, Kombo Mbwana, aendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Wilaya ya Tanga kuhitimisha kwa kufunga dhamana yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 05, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Tanga, Moses Maroa kutokana na maombi ya jeshi la Polisi.

Kombo Mbwana ambaye ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (@bavichatanga) wilaya ya Handeni Vijijini, anakabiliwa na kesi ya jinai, akidaiwa kutumia kadi ya simu ya mkononi isiyosajiliwa bila kutoa taarifa, licha ya mashtaka yanayomkabili kuwa na dhamana, Mahakama leo imefunga dhamana hiyo baada ya jeshi la Polisi kupitia Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa (RCO) wa Tanga kuwasilisha pingamizi la dhamana kwa hoja ambazo Mahakama imekubaliana n
20240906_023133.jpg
azo.
 
ya kwamba serikali inateka watu!
wengine hupitia humohumo kwenye upepo mtu anakisasi anapita nawewe!.
wengine wanachomoka kwenda kutafuta maisha nchi jirani bila hata kutoa taarifa kwa ndugu!.

watu wanaotekwa kwa nguvu lazima lipo jambo,hamkusikia wale watu waliofia kwa waganga na wakahifadhiwa!.
siitetei serikali najua inatakiwa ije na majibu lkn kuna kiongozi alishawahi kusema zakuambiwa changanya na zako!.

kindly for the other issues it's too secret to be open,yes they do coz sometimes it's for the country!!.
 
hatari sana
 
#TANZANIA: MAHAKAMA YAFUNGA DHAMANA YA KOMBO, AENDELEA KUSOTA RUMANDE TANGA
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz) mkoani #Tanga, Kombo Mbwana, aendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Wilaya ya Tanga kuhitimisha kwa kufunga dhamana yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 05, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Tanga, Moses Maroa kutokana na maombi ya jeshi la Polisi.

Kombo Mbwana ambaye ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (@bavichatanga) wilaya ya Handeni Vijijini, anakabiliwa na kesi ya jinai, akidaiwa kutumia kadi ya simu ya mkononi isiyosajiliwa bila kutoa taarifa, licha ya mashtaka yanayomkabili kuwa na dhamana, Mahakama leo imefunga dhamana hiyo baada ya jeshi la Polisi kupitia Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa (RCO) wa Tanga kuwasilisha pingamizi la dhamana kwa hoja ambazo Mahakama imekubaliana nazo.

wengine wanachomoka kwenda kutafuta maisha nchi jirani bila hata kutoa taarifa kwa ndugu🥺!.
 
Zingatia

Mada hii maalum inaangazia waliotekwa ama kupotea kwa sababu za kisiasa wakiwa ni wahanga wa ukosoaji wa utawala uliopo madarakani. Ni vema na ni jukumu letu JF kama sehemu ya jamii ya Tanganyika kuonesha mshikamano kwa kuwa na mada kama hii.
 
#TANZANIA: MAHAKAMA YAFUNGA DHAMANA YA KOMBO, AENDELEA KUSOTA RUMANDE TANGA
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz) mkoani #Tanga, Kombo Mbwana, aendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Wilaya ya Tanga kuhitimisha kwa kufunga dhamana yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 05, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Tanga, Moses Maroa kutokana na maombi ya jeshi la Polisi.

Kombo Mbwana ambaye ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (@bavichatanga) wilaya ya Handeni Vijijini, anakabiliwa na kesi ya jinai, akidaiwa kutumia kadi ya simu ya mkononi isiyosajiliwa bila kutoa taarifa, licha ya mashtaka yanayomkabili kuwa na dhamana, Mahakama leo imefunga dhamana hiyo baada ya jeshi la Polisi kupitia Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa (RCO) wa Tanga kuwasilisha pingamizi la dhamana kwa hoja ambazo Mahakama imekubaliana nazo.
ya kwamba serikali inateka watu!
wengine hupitia humohumo kwenye upepo mtu anakisasi anapita nawewe!.
wengine wanachomoka kwenda kutafuta maisha nchi jirani bila hata kutoa taarifa kwa ndugu!.

watu wanaotekwa kwa nguvu lazima lipo jambo,hamkusikia wale watu waliofia kwa waganga na wakahifadhiwa!.
siitetei serikali najua inatakiwa ije na majibu lkn kuna kiongozi alishawahi kusema zakuambiwa changanya na zako!.

kindly for the other issues it's too secret to be open,yes they do coz sometimes it's for the country!!.
ya kwamba serikali inateka watu!
wengine hupitia humohumo kwenye upepo mtu anakisasi anapita nawewe!.
wengine wanac
hatari sana
Ni fedha nyingi sana zinatumika kuendesha huu mradi wa utekaji na upoteaji wa watu Kila siku mfano Kwa kijana @Sativa255 ambapo mama anasema alitoa M 35 unadhani kwa hao ambao wako mafichon zinatumika sh ngapi na hizi zote ni Kodi zetu na pia ni watu wetu"

ASKOFU
MZEE WA MP
20240906_025800.jpg
AKO
 
Back
Top Bottom