Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
Mpigie Chura Kiziwi atakupa mkeka full
Sina huo mkeka Dogo ,,alafu ni asili Tu Ulimwengu kuficha au kupoteza viumbe vyake tangu na tangu,,Kwani Wewe hujawai kupoteza/kuficha vyako kwa ajili ya maslahi na mustakabali wa Maisha yako ya sasa,,,yajayo na ya baadaye?
 
Mdogo wangu kwa Jina anaitwa msabaha Iddy, alipotea yangu mwezi wa 12,mwaka 2021 huko katavi alikokuwa a kufanya shughuli zake.

Tulipofuatilia tulipigiwa sim ya vitisho kwa private number ukiambiwa tusijisumbue kutafuta sababu hatutomuona tena😭
 
Mdogo wangu kwa Jina anaitwa msabaha Iddy, alipotea yangu mwezi wa 12,mwaka 2021 huko katavi alikokuwa a kufanya shughuli zake.

Tulipofuatilia tulipigiwa sim ya vitisho kwa private number ukiambiwa tusijisumbue kutafuta sababu hatutomuona tena[emoji24]
Duuh[emoji24][emoji24] poleni saana mkuu,ilikuaje? Jazia nyama kidogo tupate mwanga
 
SIKU 280 TANGU APOTEE ADINANI HUSSEIN MBEZI MIKONONI MWA POLISI

Maarufu kama (ADAM),umri wa miaka 32,mkazi wa Kinyerezi,mtaa wa Faru,Jimbo la Segerea,Baba wa watoto wanne.

1.Adinan Hussein Mbezi alipotea tarehe 12 September 2023 alipokuwa safarini Mwanza

2.Adinani Hussein Mbezi alizaliwa mwaka 1992 ni mfanyabiashara anaye miliki vituo 11 vya kuoshea magari Dar es saalam vya "ONE TOUCH"
Pia ni mwanasiasa
ambaye alishawahi kuwa CCM baadae akagombea udiwani kupitia ACT WAZALENDO uchaguzi wa 2020 kata ya Yombo Vituka.

3.Tarehe 12 September 2013 ADINANI alipiga simu kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE kumtaarifu kuwa amekamatwa na Polisi,kwamba wapo njiani kurudi Dar es saalam atamjulisha kituo watakacho mpeleka baada ya kufika Dar es saalam.

4.Tarehe 19 September 2023 ADINANI alipiga simu kwa Mama yake mlezi anayeishi maeneo ya ZOO,Chanika,Dar es saalam kwa kupitia namba ya simu 0659167082

Akimueleza Mama yake kuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Tazara,akaomba Mama yake amsaidie kumpatia namba ya Kaka yake aitwaye SAMIR HUSSEIN MBEZI

Pia aliomba Mama yake ampe taarifa rafiki yake aitwaye AMIR KHALID NASIBU (SAM) mwenye namba za simu 0711959432
ambaye amekuwa akishirikiana na familia katika kumfuatilia ADINANI kwa kila hatua.

5.ADINANI alijitahidi sana kufanya mawasiliano na ndugu zake kila kituo alichokuwa anapelekwa Jijini Dar es saalam tangu akamatwe Mwanza.

Alipiga simu akiwa Central Police Station,alipiga simu akiwa Kituo cha polisi Stakishari na simu ya mwisho alipiga kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE akiwa Tazara kupitia simu ya Polisi nambari 0659167082

Sasa akimtaarifu mke wake kuwa amepigwa sana,anahali mbaya ambayo mke wake aligundua hali ya mme wake kuwa yupo katika mateso

ADINANI aliomba mke wake atume kiasi cha Shillingi laki 5 katika namba 0659167082 ambayo alisema namba ya simu ya Polisi aliyekuwa naye wakati huo,kwa ahadi ya kiasi hicho kingesaidia asiendelee kuteswa zaidi.

Mke wake ROSEMERRY MASSAWE alitekeleza ombi la mume wake kwa kutuma laki tano.

6.Ndugu wa ADINANI walifika kituo cha Polisi Tazara,ambapo afande Kaduma mwenye namba 0757078736 alikana kumshikilia ADINANI kituo cha Tazara

Mwisho walienda Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo walielekezwa waende Kituo cha polisi kati ofisi ya ZCO kandaa maalum DSM,kumuuliza Afande Mafwele kuhusu ndugu yao kushikiliwa na Polisi

ZCO Mafwele alikana kumshikilia ADINANI,aliwatolea orodha ya mahabusu wanaoshikiliwa kituoni pale, Jina la ndugu yao halikuwemo katika orodha ya mahabusu.

Pia aliwataarifu kuwa na wao Kanda maalum ya Dar es saalam wanamtafuta ADINANI kama mtuhumiwa,wakimpata wataitaarifu familia yake.

7.Ndugu wa ADINANI katika kumtafuta ndugu yao walifanikiwa kuonana na Kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi,ambaye aliwathibitishia kuwa ndugu yao yupo Kituo cha Polisi Tazara,aliomba kiasi cha shillingi million 10 ilikuwasaidia kumaliza sakata la ndugu yao,

Ndugu walitoa kiasi cha shillingi million 10 kupitia dereva wake,lakini baada ya kutoa kiasi hicho,Kigogo huyo aligeuka kuwapa jibu kumbe ni majina tu ndiyo yanafanana,lakini ndugu yenu hayupo kituo cha polisi Tazara

8.Baada ya siku kadhaa kupita ndugu wa ADINANI walipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari wa Kituo cha polisi Mburahati kupitia namba ya simu 0713440820

Askari huyo aliwaeleza Kuwa ADINANI yupo Kituo cha Polisi Mburahati na hali yake ni mbaya sana.
Askari huyo aliomba watumiwe kiasi cha Millioni 2 na laki 5 ili wasiendelee kumuadhibu na kumpa mateso ndugu yao.

Ndugu walipotuma shillingi million mbili na laki tano simu hiyo haikuwahi kupatikana tena.

9.ADINANI alikuwa na mpenzi wake mwingine Dodoma,ADINANI alimpigia mpenzi wake huyo kumjulisha kuwa amekamatwa na Polisi na kumtaarifu kuwa kama anamtafuta amtafute kupitia rafiki yake mwenye namba 0742866092

Alipompigia mtu huyo alikata simu ya kawaida akapiga video call na kuwataarifu ADINANI hayupo tena Duniani

10.Gari ya ADINANI yenye usajili T146 DPY imeonekana kituo cha Polisi Selander bridge.

Chanzo: Meya wa Zanani Jacob Boniface
20240711_184151.jpg
20240711_184159.jpg
 
Zikiwa zimepita siku 29 tangu kada wa Chadema, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) adaiwe kupotea, hatimaye leo Julai 14, 2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zacharia Bernard amesema wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Julai 14, 2024 Kaimu kamanda Benard amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.
IMG_20240714_155817_476.jpg
 
View attachment 3035589
Kada maarufu wa Chadema mkoani Tanga, Kombo Mbwana maarufu kama "Mzalendo" anadaiwa kutekwa Tarehe 16/06/2024 majira ya saa 2 mbili 2 asubuhi, akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Kwamatuku Wilaya Ya Handeni.Mke wa Kombo anasema siku ya tukio, walipata mgeni aliyejitambulisha kuwa ni "mtu wa serikali" akamtaka Kombo waongee, akieleza kwamba kuna eneo alinunua karibu na alipojenga Kombo. Baada ya kutoka Kombo hakurudi na hakupatikana tena kwenye simu hadi leo. Na huo ndio ulikua mwisho wa Kombo kuonekana hadharani.Hadi leo hajulikani alipo. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chadema mkoa wa Tanga, ndugu Michael Haule inaeleza kuwa wamemtafuta Kombo katika vituo vya Polisi na hospitalini lakini hawajamuona. Wametoa taarifa polisi lakini Kamanda wa Polisi amesema nao pia wanamtafuta. #JusticeForKombo #BringBackKombo
View attachment 3042824
Polisi - Tanga, wakati tunalalamika kwamba Kombo Mbwana Twaha ametekwa na watu wasiojulikana Handeni, Polisi walitoa RB Na. HAN/CID/23/2024 kwamba wamefungua jalada la uchunguzi kutekwa na kupotea kwa KOMBO. Kumbe wanachunguza kutekwa na kupotea mtu ambaye wao wanamshikilia.
GSeF-2kWUAACw7D.jpg
 
Kwa kujibu wa ukurasa rasmi wa X (zamani Twitter) wa Maria Sarungi Tsehai, idadi ya raia wanaopotea ama kutekwa inazidi kuongezeka siku hadi siku kiasi cha kuzua taharuki miongoni kwa Watanzania. Taarifa za ndugu wa wanaopotea huwa zinatolewa vituo mbalimbali vya polisi, na kuna wakati juhudi za kuwapata wanaopotea zinagonga mwamba kabisa. Hapa chini ni baadhi ya majina ya waliopotea na/au kupatikana, kwa mujibu wa ukursa huo wa Maria Sarungi, kadri alivyokusanya kutoka vyanzo mbalimbali, kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka huu 2024.

WALIOTEKWA 2021 - 2024
(ISIPOKUWA 1. & 2. )

Hii orodha inajumuisha waliotekwa na waliopatikana na pia ambao hawajapatikana.
Kama kuna mtu una taarifa yake kutekwa 2021 - 2024 na humwoni katika orodha wasiliana nasi DM:

  1. Mr Thomas Mungo Ihuya- Alikuwa anafanya kazi mahakama kuu Mwanza alipotea tangu March 2018 mpaka leo hajapatikana
  2. Dennis Kantanga- Alitekwa sasa ni zaidi ya miaka 4 hajawahi kupatikana wala kusikika. Alikuwa akiitwa Dennis Kantanga alikuwa mkazi wa shinyanga mjini na alikuwa akifanya shughuli za tehama kwa maana ya kutengeneza na kuuza computers, desktop pamoja na laptops na vifaa vingine vya technolojia ikiwepo cctv's. Siku anachukuliwa alifatwa dukani kwake na watu wawili au zaidi lakini waliofika dukani walikuwa wawili na kujitambulisha askari waliondoka kwa gari yake mwenyewe(Dennis) na ikawa mwisho wa kusikikika kwake. Katika utaratibu wa kureport polisi na kutrack simu ilionekana simu yake iliwashwa Musoma na baada ya hapo haikupatikana tena. Gari yake ilikuja kupatikana maeneo ya nzega ikiwa imeegeshwa katikati ya mji baada ya wiki moja or so.
  3. Abdallah Salumu Msangi - Alipotea Iringa mwishoni mwa mwezi july 2021 na hajapatikana mpaka leo. Kazi yake alikuwa lecturer chuo cha Mkwawa tawi la UDSM.
  4. Joseph Mnyonga - Alitekwa july 2021 nyumbani kwake Mwanza na watu waliojitambulisha kuwa ni askari polisi kutoka mkoa wa Mwanza mpaka sasa hajapatikana.
  5. Mzee Haji Soft - Alikuja kuchukuliwa kibarazani kwake alipokuwa amekaa, ilikuja gari ikisema kuwa wao ni mapolisi, toka hapo hakuonekana tena mpaka leo, tumetafta sanaa...ikiwemo polisi, mortuary mpaka kwa waganga
  6. James Sije - Alitekwa na askari polisi anayeitwa sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi nyakato 17 Aug.2021 mpaka sasa hajapatikana.
  7. Tawfiq Mohamed - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
  8. Self Swala - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
  9. Edwin Kunambi - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
  10. Hemed Abass - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake watano. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
  11. Rajabu Mdoe - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake watano. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
  12. Alphone Bilasenge - Alitoweka ghafla. Simu yake mara ya mwisho ilizimiwa kibeta Bukoba mjini (Kagera)
  13. Albert Kiseya Selembo - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  14. Moloimeti Yohana Saing'eu- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  15. Ndirango Senge Laizer- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  16. Joel Clemes Lessonu - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  17. Simoni Nairiam Orosikiria - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  18. Damiani Rago Laiza - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  19. Mathew Eliakimu Siloma - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  20. Lukas Kursas Njausi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  21. Taleng'o Twambei Leshoko - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  22. Kijoolu Kakey Olojiloji - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  23. Shengena Joseph Killel- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  24. Maseke Mwita Maseke - Aliondoka nyumbani TARIME - Nkerege mwaka 2022 kwenda Geita akawa anakaa Geita kimakazi kujishughulisha na kazi ndogo ndgo kwa zaidi ya miezi 6 na aliweza kuwa anarudi hata nyumbani Tarime kusalimia baada hapo simu yake haikuwahi kupatikana ,jitihada za kumtafuta kwenye vituo vya police& hospital vimegonga mwamba maana hazijazaa matunda.
  25. Molongo Daniel Paschal - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  26. Simeli Parmwati Karongoi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  27. Lekayoko Parmwati Sirkoti- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  28. Sapati Parmwati Sirkoti - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Alituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi..
  29. Ingoi Olkedenyi Kanjwel - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  30. Sangau Morongeti Ngiminisi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  31. Morijoi Ngoisa Parmati- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  32. Morongeti Meeki Masako - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  33. Kambatai Lulu- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  34. Orias Oleng'iyo- Ni mzee wa makamo sana. Aliumizwa wakati vikosi vya usalama vilitumia risasi dhidi ya wakazi wa Loliondo. Alichukuliwa na watu wanaoaminiwa kuwa sehemu ya vikosi vya usalama na hajaonekana tena.
  35. Wilson Kolong- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  36. James Taki- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  37. Joseph Jartan - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi.
  38. Kelvin Shaso Nairoti - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  39. Lekerenga Koyee Orodo - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  40. Fred Victor Ledidi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  41. Simon Morintant - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
  42. Dotto Kabwa - Alitekwa 4th july 2022 na askari polisi anayejulikana kwa jina la Wambura Mwita kutoka kituo cha polisi Ifunda Iringa na hajapatikana mpaka leo.
  43. Chande Kizega- Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 18th Aug.2022 akiwa dukani kwake Machinga Complex. Mpaka sasa hajapatikana.
  44. Yahya Ally - Alitekwa 6th Sept.2022 Mbagala Kizuiani na askari polisi wakiongozwa na OCCID Abdalah Suleiman. Mpaka sasa hajapatikana.
  45. Mzee Samwel Matiko Mkongo - Alitekwa Geita 27th Jan.2023 na askari polisi sgt. Hamis mwenye namba 0789938835 na kupelekwa kituo cha Muriaza –Butiama – Mara. Ndugu walifika hapo na wakamuona akiwa ametapakaa majeraha, lakini waliporudi kumletea chakula hawakumkuta tena kituoni hapo na hajaonekana mpaka leo. Tarehe 23 Machi 2023 tulitaarifiwa kuwa DCI alifika Mkoani Geita kushughulikia jambo hilo. Tarehe 24 Machi 2023 tukataarifiwa kuwa DCI ameunda timu na ilihoji ndugu wa Samwel.Kuna taarifa askari waliomteka Mzee Samweli Matiko Mkongo wamekamatwa akiwemo Sgt. Hamisi. Sgt. Hamisi analalamika kuwekwa lock up wachache wakati kwenye jambo hilo wako wengi. Anadai kuwa taskforce ya kuteka watu wasumbufu katika mikoa ya Geita na Mara iliundwa na wakubwa. Analalamika kwa nini wakubwa wanahojiwa wakiwa nje? Anajiuliza ni kwa nini Tume ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) imewang'ang'ania wao tu.
  46. Aziz Kinyonga - Alipotea mwaka jana mwez wa pili, hadi anapotea alikuwa akiishi chamaz dar es salaam na mkewe n watoto wawili, Gar yake ilikutwa imetelekezwa maporini Mtwara, siku anapotea usiku mkewe alimpigia simu ilipokelewa ila alikuwa anasikia mabishano na mumewe na mwanamke simu ilivyokatwa hadi leo hajapatikana zaid ya mwaka, kwa mujibu wa mkewe walikuja askar kukagua nyumba hawakupata walichotaka waliulizia kama ana miliki silaha anapohifadh, walikuta laki 2 askar wakapita nayo wakasepa, ikaja tena Noah tinted ikashusha kioo mkono ukapoint nyumba hakumfahamu km ni mumewe au nan maana kilishushwa nusu, baada ya hapo wamehangaika mochwar zote hadi vituo vya polis hawajampata, gar walimwambia apeleke laki 5 ili wampatie mkewe kule kituoni, familia imekata tamaa hadi leo.
  47. Mohamed Mayengo Kalebela - Walikatwa jumla watu 6 wa maeneo ya katoro mwaka 2023 mwezi wa 4 tarehe 5 na tukatafuta vituo vyote vya mkoa wa geita na mwanza bila mafanikio hadi Leo hawajulikani kama wapo au wamekufa na hakuna ilyerudi kwake.
  48. DEUSDEDITH SOKA - Alitekwa maeneo ya Kinondoni Studio Asubuhi saa 7:00 Asubuhi na kupelekwa garage ya Ostarbay Polisi, baada ya muda mchache kelele zikawa nyingi ndipo wakampeleka kituoni japo hawakumsajili hadi ilipofika jioni.
  49. Amon Mrimi Magige - walikuja na defender mbili wakamchukua nyakato Mwanza, tangu mwezi wa kumi mwaka Jana mpaka sasa haijulikani alipo imeshakuwa historia.
  50. Jerome Kisoka a.k.a Mapii - Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 14th Nov.2023 Njoro-Moshi na hajapatikana mpaka leo.
  51. Benson E.A. Ishungisa - Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 26th Novemba 2023 akiwa nje ya Hospital ya Makangarawe Yombo . Benson alikuwa akimsubiria abiria nje ya hospital hiyo na hata bodaboda wenzake walipoulizwa kituo cha polisi anachopelekwa hawakujibiwa. Mpaka leo hajapatikana.
  52. Charles Aden Mwampyate - Alitoweka tangu 7th Dec.2023 akiwa Dar es Salaam na hajapatikana mpaka le0.
  53. Mussa Venerable Mziba - Alitekwa Disemba 7 2023 alipokuwa ofisni kwake, walikuja watu waliojitambulisha kama polisi na kumwita nje ya uzio wa geti na kuondoka naye. Musa ni mfanyabiashara wa madini na alikuwa amekwisharipoti polisi kesi ya kusumbuliwa na mshindani wake wa kibiashara na polisi wengine. Hadi sasa simu yake imezimwa na familia haina taarifa zake.
  54. Hamza Said - Katibu wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Geita. Alitekwa 17th Dec.2023 nyumbani kwake mtaa wa Mwatulole – Geita na watu waliojitambulisha ni askari polisi. Mpaka leo katibu huyo hajapatikana.
  55. William Herman - Alitekwa Mwanza 1st Jan.2024 na askari polisi anayefahamika kwa jina la sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi Nyakato.
  56. Yonzo Shimbi Dutu- Alitekwa 2 Machi 2024 na askari polisi wa kituo cha polisi Kwimba Mwanza akiwa na wenzake maeneo ya Bushini-Kishapu Shinyanga. Wenzake waliachiwa ila yeye hajapatikana na hayupo vituo vyote vya polisi.
  57. Abdulrazak Mohamedi- Alikamatwa na Polisi huko Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru tangu tarehe 07 March 2024 kwa tuhuma za ugaidi.Cha ajabu Ndugu walipoenda kituo cha polisi cha Tunduru mjini kwa OCD kuulizia ndugu hawakumkuta na polisi wanasema hawajamkamata wao. Ndugu wakasema “kama hamjamkamata basi tufungue shauri la ndugu yetu kupotea” polisi wakakataa wakatufukuza na kuwaambia wakamtafute ndugu yao kwingine. Baadae ndugu wamefuatilia hadi kwa RPC wa Ruvuma ndo wakafungua kesi ya kupotea. LAKINI Alikamatwa na polisi maeneo ya Cross road Tunduru mjini mchana kweupe, watu kibao walishuhudia tukio hilo. Hadi hajapatikana
  58. 58DEUSDEDITH SOKA - Alitekwa 12 March 2024 nyumbani saa kumi usiku na badae kupelekwa kwenye Godown na kupigwa na kuumizwa sehemu ya jicho, na mgongoni. Aliachiwa baadaye.
  59. David Gaspar Lema - Alitekwa 6 Aprili 2024 Baada ya kelele nyingi kwenye mtandao aliachiwa.
  60. Yusuph Dudu - Alitekwa tarehe 9 April mwaka 2024 mpaka sasa hajulikani alipo. Siku ya tukio wanaume wawili walikwenda nyumbani kwake wakiwa na silaha mida ya saa moja usiku wakagonga mlango akafungua mtoto wake wa kiume mwenye miaka 8 wakamwambia amwite baba yake. Yusuph alivyofika mlangoni wakamwambia awafate nje wana mazungumzo nae. Baada ya Yusuph kutoka nje kuwafata hatua kadhaa kutoka kwenye nyumba yake walitokea watu wengine wanane wakiwa na silaha. Walitembea mpaka yalipokuwa magari yao wakamchukua Yusuph na kuondoka nae na tangu siku hiyo mpaka leo hajarudi nyumbani na hajulikani alipo. Taarifa ya kutekwa kwa Yusuph imeripotiwa katika kituo cha Polisi Mbagala maturubai kupewa RB yenye namba MBL/RB/2891/2024. Yusuph alikuwa anafanya kazi katika bank ya Habib iliyopo stesheni dar. Yoyote atakae pata taarifa zake atoe taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu nae au awasiliane na namba 0676125590 au 0717699898.
  61. Kennedy Mwamlima- Alitekwa Mbeya na watu waliojitambulisha ni askari polisi 11 April 2024. Alipatikana Igunga Tabora 16th April 2024 akiwa ametapakaa majeraha. Kwa maelezo yake alikuwa akiteswa katika vituo vya polisi na alikuwa akiulizwa nani anamtuma kukosoa serikali katika mtandao wa TikTok.
  62. Kastory Kapinga - mwanafunzi wa Saint Augustine University of Tanzania . Arusha Centre mwaka wa tatu Alitekwa Mbinga, Ruvuma Ghafla alitoweka na chuo hakuonekana geto lake lilikuwa limefungwa. Takribani miezi miwili sasa. Alikuwa anapenda kutumia mtandao wa kijamii wa facebook, Baada ya hapo hajaonekana tena. Tumekuja kushtukia tarehe 25 ya mwezi wa nne baada ya kutoonekana chuo. Taarifa kituo cha polisi zilifika.
  63. Lilenga Isaya Lilenga - Alitekwa 11th May 2024 maeneo ya Kibirizi-Kigoma na watu wanaodaiwa ni polisi kisha kutokomea naye kusikojulikana. Mpaka sasa hajapatikana.
  64. Daniel Elias Sayi - Alichukuliwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake tarehe 13 May 2024. Waliondoka naye kwa gari na hadi sasa hajaonekana wala kupatikana katika vituo vya polisi.
  65. Kombo Mbwana Twaha- Alitekwa nyumbani kwake Handeni Tanga na watu waliojitambulisha ni askari polisi 15th June 2024. Baada ya kupotea kwa siku 29, jeshi la polisi mkoani Tanga limekiri kumshikilia, kwa tuhuma za makosa ya kimtandao.
  66. Edgar Mwakalebela (alias Sativa )- Alitekwa 23 june 2024 Ubungo Dar es Salaam. Alipatikana 27 june 2024 huko Katavi porini akiwa ametapakaa majeraha.
  67. Mjukuu wa Mustafa Songambele - Mfanyabiashara wa Kariakoo alitoweka baada ya kufunga duka lake jioni na hadi leo hajapatikana wala hakuna taarifa zake

JESHI LA POLISI LINASEMAJE KUHUSU MATUKIO HAYO YA UPOTEVU WA RAIA?
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi Nchini halihusiki na vitendo vya utekaji huku akisema ni kweli matukio ya utekaji na Watu kujiteka yapo lakini Polisi wanapambana kuwakamata Wahalifu na kuwaokoa wanaotekwa.

Akiongea Mkoani Simiyu jana, Julai 15, 2024, IGP Wambura amesema “Hatuhusiki na utekaji Watu, sisi ni Jeshi ambalo linalinda usalama wa Watu na mali zao, wanaoleta tuhuma za namna hiyo ni vitendo vya kutuvunjia adabu, matukio ya utekaji yaliyofanyika Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa na kuwakamata Wahalifu na kuwaokoa wale waliotekwa”

“Kwa mfano alitekwa Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi na kuuawa wale ni Jeshi la Polisi?, Jeshi la Polisi limewakamata wale, kuna Mtoto mwingine ametekwa Geita na Watekaji wakadai milioni 5 kwa Wazazi wake, Jeshi la Polisi limewakamata na kuokoa Mtoto, wale Watekaji ni Jeshi la Polisi?”

“Kuna Mtoto ametekwa Mbeya na Wazazi kudaiwa watoe milioni 20 lakini Mtoto huyo aliuzwa na Mama yake kwa huyo aliyejifanya Mtekaji ili wapate pesa kwa Baba wa Mtoto, hao ni Jeshi la Polisi?, kuna Watu wanajipoteza na kudai wametekwa, tumeshuhudia juzi Mwanza Mtoto wa miaka 12 amejiteka na Mdogo wake na kudai pesa kutoka kwa Mzazi wake”

“Cha msingi Jamii yetu ibadilike, Jamii yetu iache taarifa za uongo tuzingatie maadili, kuteka Watu, kujiteka na kutoa taarifa za uongo, nyie Waandishi mnapopewa taarifa hizi muwe mnacheki na Vyombo vyenye Mamlaka ya kuchunguza, tusichukue tu maneno ya Mtu mmoja anasema nimetekwa, ametekwa, amepotea, tayari mnakwenda kutoa taaarifa”
#MillardAyoUPDATES
 
People said Magufuli should die to end these….
Magufuli is no longer…….! Where this coming from? Unknow people wasn’t Magufuli business? We hated him for no resons?
JPM Alichukiwa bure tu. Utekaji serious ulianza enzi za JK, kumbuka Dr. Ulimboka wa Muhimbili, mhariri Absalom Kibanda nk.
 
Screenshot_20240719_102357_Chrome.jpg

Matukio ya watu kutoweka katika mazingira yenye kutatanisha huku askari polisi wakihusishwa kuwashikilia yanaendelea kushika kasi nchini.

Taarifa mpya zinadai kuwa vijana wanne wilayani Temeke, Dar es Salaam na mkazi mmoja mkoani Geita wametoweka na jitihada za kuwatafuta hazijazaa matunda kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Taarifa zinasema vijana Ramadhan Sultan(20), Charles Kelvin (18), Abdulrazack Salim(18), na mwenzao ambaye taarifa zake hazikupatikana, wametoweka tangu Juni 20, 2024.
 
Umetoa uzi wenye jumbe tuchukue tahadhari usikubali kuongea na mtu usiyemjua siku hizi au unayemjua katika mazingira tata
 
Task_71c5c5bb39dcfc24.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya akiwa na mtoto Laitenes Taifa (3) aliyedaiwa kupotea tangu Julai 13, 2024 baada ya kutelekezwa katika basi la Kampuni ya AM linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Dodoma. Mtoto huyo ni mkazi wa Kijiji cha Ushokora wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora. Picha na Sharon Sauwa

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Muleba.png

Askari Polisi wanne akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Kata ya Goziba, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, John Mweji na mgambo watatu wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumuua Baraka Lucas.

Mwili wa Lucas (20) aliyekuwa mbeba dagaa wabichi Mwalo wa Kisiwa cha Goziba, ulipatikana ukielea Ziwa Victoria Juni 12, 2024 ikiwa ni siku nne kupita tangu adaiwe kukamatwa na polisi wa kituo hicho Juni 9, mwaka huu.

Ndugu zake baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa ndugu yao na askari wa doria usiku wa manane, walikwenda kituoni bila kufanikiwa kumuona na baadaye Juni 12, 2024 ndipo mwili wake ulionekana kando ya Ziwa Victoria ukielea.

Hii ni kesi ya pili kuhusisha maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya ile ya inayoendelea Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, ikiwahusisha maofisa saba walioshitakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis.

Washtakiwa hao saba ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC-CID) wa Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Gilbert Kalanje na aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi (OCS) cha Mtwara Charles Onyango aliyekuwa Mrakibu Msaidizi (ASP).

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Intelijensia, Nicholaus Kisinza, mkaguzi msaidizi wa Polisi Yesse Msuya, aliyekuwa mganga mkuu zahanati ya polisi akiwa na cheo cha mkaguzi msaidizi, Shirazi Mkupa na mshitakiwa Koplo Salum Juma Mbalu.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa Hamis katika kituo cha Polisi Mitengo wilaya ya Mtwara Januari 5, 2022 na kutupa mwili wake Majengo kata ya Hiari.

Madai ya mauaji Muleba

Katika kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili OCS, John Mweji, washitakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Jumanne Julai 23, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Masesa, huku polisi wakijaribu kuifanya kesi kuwa siri.

Hali hiyo ndiyo iliwapa wakati mgumu wanahabari kuweza kufahamu nani ni mgambo nani askari wa Jeshi la Polisi zaidi ya kuambiwa kuwa katika washitakiwa hao saba, Askari Polisi ni wanne na askari wa Jeshi la Akiba (mgambo) ni watatu.

Washtakiwa wengine mbali na OCS wametajwa kuwa ni Ahmad Rashid, Fransis Hayshi, Ally Jumanne, Emmanuel Massatu, Evodius Makaka na Athumani Malindo na watatu ni Polisi na watatu ni mgambo.

Akisoma shitaka hilo katika kesi hiyo ya mauaji (PI) namba 18914 ya mwaka 2024, Wakili wa Serikali, Agness Owino alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 9, 2024 na hawakutakiwa kujibu lolote na kupelekwa mahabusu gerezani.

Hii ni kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kusikiliza kesi za mauaji huku upande wa mashitaka ukiieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, 2024 itakapotajwa tena.

Chanzo: Mwananchi
 
(Warumi 12:19)

"Kisasi ni juu yangu, Mimi nitalipa, asema BWANA!!"

HAKIKA Mungu atawalipia kisasi hao ndugu wa waliouwawa bila hatia Wala kufuata Sheria.
 
Back
Top Bottom