Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
Tarehe 13/10/2024 saa 19:30 jioni kiongozi mwingine wa CHADEMA jimbo la Vwawa Hussein Mwashambwa ametekwa nyara na watu waliojitambulisha ni askari polisi Ruanda Mbozi. Ndugu wamemtafuta vituo vyote vya polisi hayupo. Mnatulazimisha tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe?
20241016_131125.jpg
 
Tarehe 13/10/2024 saa 19:30 jioni kiongozi mwingine wa CHADEMA jimbo la Vwawa Hussein Mwashambwa ametekwa nyara na watu waliojitambulisha ni askari polisi Ruanda Mbozi. Ndugu wamemtafuta vituo vyote vya polisi hayupo. Mnatulazimisha tuingie kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe?
View attachment 3126519
Taarifa za namna hii za Watu kutekwa na kisha kupotezwa huwa zinanikera Sana kuzisikia. Zinakera hasa.
 
Mdogo wangu kwa Jina anaitwa msabaha Iddy, alipotea yangu mwezi wa 12,mwaka 2021 huko katavi alikokuwa a kufanya shughuli zake.

Tulipofuatilia tulipigiwa sim ya vitisho kwa private number ukiambiwa tusijisumbue kutafuta sababu hatutomuona tena😭
Na mlipotezea? situation kama hiyo ilitokea kwa jirani yangu, ila jamaa yao alipatikana katupwa msituni, wafugaji walimuokota, inaonekana wale jamaa baada ya kuona msako umepamba moto (walitangaza kwenye radio za mkoa)wakaamua kumtelekeza tu
 
Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka Wimbish la utekaji unaofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wa vyombo vya ulinzi na usalama.alianza setiva akapatikana bahati nzuri makosa waliyofanya vyombo vya ulinzi na usalama hayatajirudia tena.sasa hv ukitekwa tu jua ndio bai bai mama jeni hutoonekana tena.maana ukiknekana tu utatoa siri zao ambazo wahusuka washa kataa kuhusika nazo tokea mwanzo mwa huu utekaji.mwenyezi mungu mnusuru Nondo kwenye mikono ya wadharimu
 
Kwa hiyo unataka nkituambiqje kuhusu Nondo?
 
View attachment 3035578
Kwa jina anaitwa Samuel John Mwita
Anafanyakazi Baobab secondary school. umri wake ni miaka 51 amepotea tangu jumatano tarehe 3/7/2024 Alfajiri.
Amepotea katika mazingira yasiyoeleweka RB number MPG/RB/980/2024. Ripoti ipo kituo Cha polisi Mapinga . Mwenye taarifa za kupatikana kwake atupigie kwa namba 0743812622 au 0712217762 au kituo Cha polisi kilicho karibu.

Sambaza kwa magroup mengi kwa ajili ya maombi na upatikanaji wa Mr. Samuel John Mwita.
 
View attachment 3035589
Kada maarufu wa Chadema mkoani Tanga, Kombo Mbwana maarufu kama "Mzalendo" anadaiwa kutekwa Tarehe 16/06/2024 majira ya saa 2 mbili 2 asubuhi, akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Kwamatuku Wilaya Ya Handeni.Mke wa Kombo anasema siku ya tukio, walipata mgeni aliyejitambulisha kuwa ni "mtu wa serikali" akamtaka Kombo waongee, akieleza kwamba kuna eneo alinunua karibu na alipojenga Kombo. Baada ya kutoka Kombo hakurudi na hakupatikana tena kwenye simu hadi leo. Na huo ndio ulikua mwisho wa Kombo kuonekana hadharani.Hadi leo hajulikani alipo. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chadema mkoa wa Tanga, ndugu Michael Haule inaeleza kuwa wamemtafuta Kombo katika vituo vya Polisi na hospitalini lakini hawajamuona. Wametoa taarifa polisi lakini Kamanda wa Polisi amesema nao pia wanamtafuta. #JusticeForKombo #BringBackKombo
View attachment 3042824
Kwa mzigo ulivyoplaniwa haikuwa siku yake huyu jamaa alikuwa anaenda. Tungeishia kulalamika na kumpost tu
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili wakiume na wakike nyumbani kwa mganga wa kienyeji anayefahamima kwa jina la Abdulikarim mkazi wa Kimara Baruti
IMG_20250115_145612_419.jpg
 
Back
Top Bottom