Mkuu, usijifunge akili. Tumia hii Vita kujifunza na kujua jinsi Silaha zinafanya kazi. Achana na ubishi wa kijinga. Hii thread tunaelimishana si kubishana. Tafuta thread za Vita ya Ukraine za kubishana.
Wiki ya Kwanza ya Vita Mrusi alifika KM 10 kutoka Mji Mkuu wa Ukraine Kyiv. Ila sasa hivi karudishwa nyuma Km 595.
Ndani ya Siku 20 za Kwanza Urusi walifika ndani ya Mikoa 13 lakini sasa hivi wapo ndani ya Mikoa Minne kama sio Mitatu.
Urusi kapoteza Vifaa, Mifumo na Wanajeshi wengi. Inakadiliwa Wajeshi zaidi ya 35 elfu wa Urusi wamefia Ukraine. Hapa hatujahesabu wasiojulikana walipo. Hii ni idadi ya maiti zilizoonekana
Wakati Ukriane imepoteza Major Generals 2, Urusi imepoteza Majors Generals 12. Ngoja nikuache uendelee kusikia unachotaka kusikia.