Mkuu; Labda nikuulize hivi: Nani aliwawezesha au ni Nani alikuwa nyuma ya hayo matokeo? Hapakuwepo na shinikizo?
Je, hiyo kura ilikuwa kura Huru? Suala la Ethnicity ni hoja ya kizamani sana iliyopitwa na wakati. Watu wako huru kuishi popote alimradi tu wafuate Taratibu za nchi husika. Yaani tukishabikia ukabila... daah! e.g. Mmasai wa Kenya aseme ni Mtanzania kwa sababu Wamasai wapo Tanzania?. Kuongea Ki-Russia au kuwa na mila na desturi za Ki-russia haihalalishi au hakumfanyi mtu awe Mrusi. Hivo ni vitu mtu aweza kujifunza. Lakini Sheria inabainisha mipaka, wapi ni mwanzo wa Nchi na mwisho n.k. na inatambulika kiMataifa.
Unyonge na kunyanyaswa kunategemea mental perception ya Mtu. Wapo watu wanapenda upendeleo wa hapa na pale. Asipopata anadai kunyanyaswa. e.g. Mtu huna vigezo say kitaaluma lakini unataka uajiriwe kama Mtaalam. Ukikataliwa unazua hoja ya upendeleo na kunyanyaswa.