Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Na sasa ndio wametisha zaidi, wameenda kujificha kwenye mitambo ya nuclear.
Ila mimi siwalaumu hawa warusi sababu wanadai tarehe 24 February walipoivamia Ukraine hawakuwa wakijuwa kama wanafanya uvamizi.

wanadai walipokuwa wakisikia mizinga walikuwa wanasonga mbele wakijua kwamba wanakabiliana na majeshi ya NATO, baada ya kufika UKRAINE hasa ndo wakakuta hakuna NATO wala sisimizi bali raia wasio na hatia wa Ukraine.

Yaani kwa sasa, wote watatu, Raia wa Ukraine, Wanajeshi wa Ukraine na Wanajeshi wa Urusi wote ni wahanga wa Ukichaa wa Putin.

wote wanaviziana kuuana, sababu hawaaminiani.
 
Hawawezi kuaminiana kwa sababu Warusi wametumwa/wamekuja Ukraine kwa Agizo la Putin(Hawajaitwa na Ukraine), raia wa Ukraine baadhi yao wamenaswa ktk mapigano na ili wasiuawe kikatili na majeshi ya Urusi, inabidi wawe watiifu kwa lazima na hivyo kwa shuruti wanakubali majumba yao yatumike kama maficho kwa wanajeshi ya Warusi. Wanajeshi wa Ukraine wapo kutimiza kiapo cha Kuilinda nchi yao dhidi ya Maadui wa nje na ndani dhidi ya Taifa lao(Wanatimiza wajibu wao) na wanatii agizo la Rais wao Zelensky.
Kwa mantiki hiyo wote watatu, kama ulivyosema, utakuta wanawatumikia mabwana watatu: 1. Wale wanaomtii Putin 2. Wale walionaswa ktk Mapigano wanapokea Amri ya Wanajeshi wa Urussi, 3. Wanajeshi wa Ukraine wanaotii Amri ya Rais wao Zelensky.
Katika Hali kama hiyo, ni kweli utakuta wote ni Wahanga kutokana na Ukichaa wa Putin.
 
Naongezea tu:
Tano, Wewe una furahia huyo Mrusi anapokuwa na kuonesha KIBURI kwa kukataa kuacha vita au Uvamizi kwa nchi nyingine hususan JIRANI yake.
Sita, Wewe unafurahia majibu yake ya Kejeli, Ufedhuli, Vitisho na Dharau anapokemea na Kuagiza Mataifa mengine (hata UN) eti wasimsaidie na wajiepushe na tena wamwache aendelee na uonevu wake dhidi ya Ukraine; vinginevyo na wao watajumlishwa hapo.
Huoni kama anakufuru?
 
😂😂😂 wametisha sana hadi wanaenda kuingia uvunguni wa vitanda vya raia kukimbia Drones na risasi za wanajeshi wa ukraine.
 
😂😂😂 wametisha sana hadi wanaenda kuingia uvunguni wa vitanda vya raia kukimbia Drones na risasi za wanajeshi wa ukraine.
Hahahahaaa. Kama ninawaona vile. Sasa ni nini kilichowaleta Ukraine?😛
 
Baada ya kuwateka Warusi, jamaa ikabidi atest Tactical vest wenyewe wanaziita "SARMAT-M" za Urusi. Zinasaidia mwanajeshi akishambuliwa risasi isimfikie. Inakinga kifua na mgongo. Sasa angalia risasi zinavyopenya kirahisi
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…