Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Angalia HIMARS ilivyoharibu magari ya Ugavi ya Urusi aina ya KamAZ-6350. Hapa ni Nova Kakhovka, Mkoani Kherson
View attachment 2340515
Kazi iendelee. Kuna jamaa kule "tuitani" jana eti kaweka kauzi kwamba 90% ya wanajeshi wa Ukraine waliokwenda kwenye Counter Offencive Operation Kherson ni RIP. Hii itawadhihirishia hata na wasomaji wengine kwamba ile Taarifa ilikuwa ni Chai ya rangi.
 
Dalili ya mvua ni mawingu. Kama Kirill (deputy) mtawala aliyesimikwa Kherson kashakimbia na kurudi moscow, maana yake kaona maji ya shingo, Kherson tena siyo territory yake. Moto uliopelekwa jana siyo wa kitoto.
Yap. Kirill(Deputy) amewaonesha wenzake (Warusi-wavamizi walioko Kherson) kwa vitendo halisi ni nini cha kufanya Chap /Fasta. Wasisubiri damu itoke masikioni. Hapa sio pa kukaa tena. Kimbiaaaa, Ondokaaa; Funga rambo chapa mwendoooo. i.e. mwenye macho haambiwi tazama.
 
HIMARS kumi na moja ni mzigo wa maana. Putin aliingia choo cha kike. Hakujua kuwa wanaume wanamsubiria uani atoke na taulo wampe za uso.
Hahahaaa. Nimeangalia ramani ya Urusi nikajiuliza: Hivi ikitokea Mrusi (Putin)akaamua kukimbia katika hali iliyopo hana pa kukimbilia zaidi ya baharini?
 
Inasemekana huko Kherson mambo si mepesi kwa pande zote,...
Unafuu kwa Ukraine ni kuwa Urusi haiku mine Kherson hivyo inawasaidia sana Ukraine kusonga mbele
Tunawaombea; Mungu awajalie wepesi wapambanaji wa Ukraine wayafikie malengo waliyo jiwekea kwa mafanikio makubwa.
 
PRAGUE -- The European Union's top diplomat, Josep Borrell, says the bloc's 27 members have agreed to suspend an agreement with Russia, which had made it easier for Russians to obtain tourist visas, as a sanction for Moscow's unprovoked invasion of Ukraine.
 
Waukraine wako smart

Wamechagua kuanza na Kherson kwa sababu wakifanikiwa kuitwaa,Warusi watapoteza Morali sana hata ya kushikilia au kupigania mikoa ya mashariki.

Kwa sasa hatupati sana taarifa za Kherson kwa sababu jeshi la Ukraine limeomba watu wapige kimya kuhusu hii offensive, kwa sababu picha na video zinaweza kuwapa clue maadui kujua zilipo positions za vikosi vya Ukraine na hivyo kuleta madhara
 
Hapa ni Mji wa Belgorod huko Urusi. Wanaonia joto la jiwe. Hawa walikuwa wanaishambulia Ukraine kutokea Urusi, Kombora likatua hatua chache tu na kuua Warusi. Matarajio ilikuwa litue Kherkiv
 
Back
Top Bottom