Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Operesheni iliyofanikiwa ya Ukraine kukabiliana na Urusi, wataalam wa Vita wanataka katika masomo ya kimataifa kuhusu mbinu na mikakati ya kijeshi Ijumuishwe. Ukraine wameweza kukomboa Km 6000 za mraba kwa siku chache. Wamefanyaje? Wanataka ifundishwe kwenye shule za jeshi. United24media wameweka video fupi jinsi ilivyofanywa.
 
NLAW Training. Ninachofurahia ni kwamba, hakuna sehemu ndani ya Ukraine ambapo Urusi wamekaa kwa amani, wanashindwa kwenye mahandaki. Na hakuna Mkoa hata mja Urusi wanashikilia kwa 100%. Vijana wetu wanazidi kuhitimu mafunzo ya kijeshi ya kutumia vifaa vya kisasa.
 
Operesheni iliyofanikiwa ya Ukraine kukabiliana na Urusi, wataalam wa Vita wanataka katika masomo ya kimataifa kuhusu mbinu na mikakati ya kijeshi Ijuishwe. Ukraine wameweza kukomboa Km 6000 za mraba kwa siku chache. Wamefanyaje? Wanataka ifundishwe kwenye shule za jeshi. United24media wameweka video fupi jinsi ilivyofanywa. Nayo imehifadiwa
View attachment 2379350
Hakika ni kielelezo kizuri sana kwa vizazi vijavyo, ni funzo tosha kwa wanaodhani kwa kutumia ubabe unaweza kujitwalia maeneo ya nchi nyingine kimasihara. Imenikumbusha ile Operation ya dk.90 iliyofanywa na makomandoo wa Israel huko uwanja wa ndege Entebe Uganda (OP. Thunderbolt) na kufanikiwa kuokoa maisha ya abiria na pia kufanikisha kuondoka nao huku wakiwaacha majeshi ya Iddi Amini baadhi yao mizoga na wengine majeruhi. Imenikumbusha jinsi Tz ilivyomfurumusha nduli Iddi Amin hadi kupelekea kuanguka kwa utawala wake.
Hongera sana makamanda na wapiganaji wa Ukraine, Hongera Taifa la Ukraine.
 
Mkuu, hili swali lako zuri sana. Nilikujibu kwa ufupi tu. Sasa nina muda ngoja twende deep kidogo. Ukiacha Silaha, Mwanajeshi anatakiwa awe na vifaa vya Msaada wa Kwanza vya kumsaidia au kusaidia mwenzake[military first aid kit]
View attachment 2378849
Vipo vitu vingi vinatakiwa lakini kuna vitu vya Muhimu unatakiwa uwe navyo.
View attachment 2378854
Sterile gauze bandage:
Hii Bandeji ina matumizi mengi: Kuzuia jeraha la mtu aliyeungua, kuzuia damu kuvuja. kurekebisha mfupa ulioteguka.
View attachment 2378864
Bandeji ya Dharura:
Bandeji ya dharura pia inaitwa "bandeji ya Israeli" imeundwa mahsusi kusaidia wapiganaji kwa kujitegemea kutumia hata kwa mkono mmoja.
View attachment 2378865
Plasta ya Kufungia jelaha
View attachment 2378867
hemostatic Bandage
Hii ni bandeji fulani imekaa kama zig zag, yenyewe sio ya kuzungusha, kwani mtu anaweza pata jelaha sehemu ambapo ili ya kuzunguka haiwezi faa mfano Kifuani. So inatumika hii
View attachment 2378871
Gloves. hivi mtu anavaa anapotoa hutumia ili kuzuia maambukizi na uchafu kuingia kwenye kidonda au kwa mtoa huduma.
View attachment 2378875
Thermal blanket:
Hii kazi yake ni kutunza joto kukiwa na baridi, hii moto haupenyi hivyo unaweza jikinga na moto au jua kali, hii unaweza kingia maji kwenye mto au Maji ya mvua kama huna sehemu ya kubebea nk. Hii ipo kama ganda la ndani la pakti ya sigara ila yenyewe imara zaidi.
View attachment 2378876
View attachment 2378886
Tourniquet au CAT tourniquet: Hii unaifunga ili kuzuia damu kuvuja sana. Inazuia damu kupotea. Ipo kama ile ya kupimia presha hospitali ambayo wanafunga kwenye mkono.
View attachment 2378888
Emergency Shears
Huu ni Mkasi wa kukatia nguo, Mkanda au kiatu ili kurahisisha utoaji huduma ya kwanza. Umetengenezwa kiasi kwamba kichwa hakiwezi jeruhi mwili unapokuwa unakata, kishikio ni Plastiki.
View attachment 2378897

View attachment 2378955View attachment 2378965
View attachment 2378957
View attachment 2378959
Marker Pen: Hizi ni kalamu imara za kuwekea alama kwenye tourniquet. Pia zinasaidia kuweka alama sehemu. Mfano kwenye mti au ubao kutoa ishara kwa wenzako wajue mumepita wapi. Pia unaweza kuandika kwenye nguo ya mtu alopoteza maisha muda na sehemu ili kuweka kumbukumbu sawa. Hii inahimili hali zote za hewa. Haifutiki kwa urahisi
View attachment 2378904
Nasopharyngeal Airway: Hii inasaidia kupitisha hewa.
View attachment 2378911View attachment 2378925
Hivi ni baadhi ya vitu unavyoviona kwenye hilo begi la kifuani ambalo pia halipitishi risasi. hivyo ni kinga
Asante kwa maelezo ya kina Mkuu,kuwa na jeshi la kisasa ni gharama sana,hapo tunazungumzia first aid kit ya mwanajeshi mmoja tu,bila silaha na mambo mengine,sijui Africa tunamudu hii?
 
Asante kwa maelezo ya kina Mkuu,kuwa na jeshi la kisasa ni gharama sana,hapo tunazungumzia first aid kit ya mwanajeshi mmoja tu,bila silaha na mambo mengine,sijui Africa tunamudu hii?
Hapo ni kwa Uchache. Pia anatakiwa awe na military canteen kiasi kwamba akifika sehemu anapika anakula.
p-29756-otg2370lg_french_canteen_set_vietnam_indochina_issue.jpg
canteen kit.png
images (1).jpg
1665137097957.png
 
Back
Top Bottom