Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Operesheni iliyofanikiwa ya Ukraine kukabiliana na Urusi, wataalam wa Vita wanataka katika masomo ya kimataifa kuhusu mbinu na mikakati ya kijeshi Ijumuishwe. Ukraine wameweza kukomboa Km 6000 za mraba kwa siku chache. Wamefanyaje? Wanataka ifundishwe kwenye shule za jeshi. United24media wameweka video fupi jinsi ilivyofanywa.
Your browser is not able to display this video.
 
NLAW Training. Ninachofurahia ni kwamba, hakuna sehemu ndani ya Ukraine ambapo Urusi wamekaa kwa amani, wanashindwa kwenye mahandaki. Na hakuna Mkoa hata mja Urusi wanashikilia kwa 100%. Vijana wetu wanazidi kuhitimu mafunzo ya kijeshi ya kutumia vifaa vya kisasa.
Your browser is not able to display this video.
 
Hakika ni kielelezo kizuri sana kwa vizazi vijavyo, ni funzo tosha kwa wanaodhani kwa kutumia ubabe unaweza kujitwalia maeneo ya nchi nyingine kimasihara. Imenikumbusha ile Operation ya dk.90 iliyofanywa na makomandoo wa Israel huko uwanja wa ndege Entebe Uganda (OP. Thunderbolt) na kufanikiwa kuokoa maisha ya abiria na pia kufanikisha kuondoka nao huku wakiwaacha majeshi ya Iddi Amini baadhi yao mizoga na wengine majeruhi. Imenikumbusha jinsi Tz ilivyomfurumusha nduli Iddi Amin hadi kupelekea kuanguka kwa utawala wake.
Hongera sana makamanda na wapiganaji wa Ukraine, Hongera Taifa la Ukraine.
 
Asante kwa maelezo ya kina Mkuu,kuwa na jeshi la kisasa ni gharama sana,hapo tunazungumzia first aid kit ya mwanajeshi mmoja tu,bila silaha na mambo mengine,sijui Africa tunamudu hii?
 
Asante kwa maelezo ya kina Mkuu,kuwa na jeshi la kisasa ni gharama sana,hapo tunazungumzia first aid kit ya mwanajeshi mmoja tu,bila silaha na mambo mengine,sijui Africa tunamudu hii?
Hapo ni kwa Uchache. Pia anatakiwa awe na military canteen kiasi kwamba akifika sehemu anapika anakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…