Warusi baada ya kuona wanazidiwa, wameamua kukimbilia Mashariki na Kusini mwa Ukraine. Napo tutawafurumisha warudi kwao. Kasikazini mpakani na Belarus kupo salama, hamna fyokofyoko ya Urusi. Wameufyata mkoa.
Ungeandika majeshi ya PUTIN ingekuwa sahihi zaidi. Sawa na majeshi ya Nduli Idd Amin kuyaita majeshi ya Uganda. Warusi hawaungi mkono uvamizi na ubeberu huo ni vile wako chini ya dikteta hawana uhuru wa kupinga.
Drone ya Ukraine ikionesha Vifaru vya Urusi maeneo ya Rubizhne Mkoani Luhansk baadhi ya Magari yalikuwa yamebeba Nitric acid, ambayo ni hatari kwa binadamu