Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Mkuu, Ngoja wapelekwe huko halafu vijana wa Ukraine wawatolee usongo.
 
Supa-pawa hawezi kufikia hali hii
OOhooO!!? Toka huko porini we nanihii; huyo Supa poa unayemwita "supa-pawa" Ndo keshafikia hapo unaambiwa sasa. Usupapawa mbona alishautema kitambo siku nyingi.? Sikuizi huyo kwisha habari yake, anajua tu kutimua vumbi(mbio). Vijana wa Ukraine weshamtoa upepo.
 
Kama hali iliyopo ni tete kihivyo basi Mrussi akili zake zitakuwa zipo kule kwenye lile tundu la kutolea taka mwili. Hao wafungwa wa kike watakuwa weaker than wale waliokusanywa kutoka mitaani(Mobilised) ukizingatia jinsia yao na huko jela wanakotokea (afya zao zitakuwa duni) na bado hawana mafunzo ya kijeshi au ya Unesi. Huko ni kuwatoa kafara kwa kweli.
 
2. Silaha za Ukraine ni precision, yaani zikitumwa zipige sehemu zinapigw palepale, tofauti na mrusi ambaye makombora yake uoiacha yale machache ambayo ni guided , hana efficiency ya kutosha kwenye kupiga target.
Hii nimeipenda. Mrussi hutupa makombora yake kwa mtindo wa kusia(Broadcast)i.e anabahatisha-bahatisha tu. Hutupa makombora mengi kwenye eneo kwa wakati mmoja ili walau kombora mojawapo libahatike kupiga target. Matokeo yake ni matumizi mabovu ya makombora jambo ambalo sasa limemsababishia kuishiwa silaha yeye na mamluki (Wagner) wake.
 
Tusubiri huenda mwakani tukashuhudia mazungumzo ya kutafuta suluhu.
 
Kwenye mazungumzo,Ukraine atakuwa kwenye position nzuri zaidi kuliko kama mazungumzo yangefanyika kipindi kile majeshi ya Urusi yapo ktk viunga vya Kiev.
Kama atafanikiwa kurudisha maeneo mengi yaliyokwishatekwa huenda akawa na 'upper hand' ila kwa Sasa bado mapema.
 
Tusubiri huenda mwakani tukashuhudia mazungumzo ya kutafuta suluhu.
Naam; kama ikitokea hivo, basi Ukraine atakwenda kwenye meza ya mazungumzo akiwa kifua mbele kwani Mrussi hatoweza au hatathubutu kumnyanyapaa au Kumwona ni duni na Mrussi ataongea kwa heshima na adabu mbele ya Ukraine kwani sasa Mrussi anajua kitakachompata zaidi endapo ataonesha ujeuri wowote ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…