Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Kama atafanikiwa kurudisha maeneo mengi yaliyokwishatekwa huenda akawa na 'upper hand' ila kwa Sasa bado mapema.
Ni muda mwafaka kwani mwelekeo wa game linavyoendelea hiyo miji mitatu Svatove, Kreminna na Bakhmut ni uhakika itakombolewa sio muda mrefu.
Halafu umewasikia Mamluki (Wagner)wanavyolilalamikia jeshi la Urussi. Hiyo ni ishara ya kuwa huko ndani Hali sio shwari hadi Urussi wanahamisha ndege-vita ili zisisambaratishwe kwa kipigo kutoka frontline ya Ukraine
 
Kwenye mazungumzo,Ukraine atakuwa kwenye position nzuri zaidi kuliko kama mazungumzo yangefanyika kipindi kile majeshi ya Urusi yapo ktk viunga vya Kiev.
Kwa sasa Ukraine hana sababu ya negotiations. Formula aliyopewa Russia ziko very clear. Mbili kati yake nimezipenda sana.

1. Ondoka kwenye territories za Ukraine including Crimea.

2. Kubali kulipa gharama za uharibifu wa miundombinu na hasara zingine.

Hizi Russia akizitekeleza Ukraine inakuwa haina sababu ya kukataa mazungumzo.

Ukraine atakuwa very strong kwenye Negotiations kama atamfurusha Russia kwenye ardhi yake kwanza.
 
Hii video imenipa raha. Maana yake HIMARS kapata long range missile.

Rostov ni mbali kutoka frontline ya Ukraine kwenye kila direction.
Yan we acha tu. Hawa wazee wa HIMARS wanajua vizuri mno jinsi ya kumshikisha adabu Mrussi anayejifanya eti supa pawa. Naona safari hii wamebisha hodi huko iliko base yao mbali ili kumpa Mrussi "advertise" iko siku wazee watatua Kremlin na viunga vyake.
 
Russia kashawashiwa full light mara tatu (3) sasa. Shambulio la Drones kwenye air base zake two times na hilo la Rostov. HIMARS na M270 ni machine hatari sana. Zikitua sehemu lazima kishindo kisikike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…