Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Darasa analopewa hapo na Ukraine linamtosha - amejua kwamba alikuwa hajui.
Mtu mzima hukubali jambo kwa ishara ukimbana.

Putin anashindwa kusema tu lakini matendo yake kwa Siku za hivi karibuni ni kwamba anakiri alikosea kutoa amri ya kuivamia Ukraine.

Kilichobaki ni kule kujitutumua kuwa ana uwezo wa kuikoromea U.S na NATO lakini kashajua kina ni kirefu hawezi kuogelea.
 
Putin hatothubutu tena kuvamiavamia majirani hovyo
Sasa hivi hata vi nchi vidogo kama Estonia au Latvia hawezi kuvamia au kuvikoromea.

Ataendelea tu na nchi ambazo ni makoloni yake kama Belarus, Armenia na vile vi nchi sita (6) vinavyoishia na "...stan" au "...jan"
 
Naomba sifa ya ATACMS
MGM-140 Army Tactical Missile System (ATACMS) is a surface-to-surface missile. Makombora ya Masafa mrefu. Yakifika, Urusi wataanza kuondoka wenyewe. Makombora haya yapiga shabaha kwa usahihi umbali wa km 300. Pia inaweza kutumika kwenye M270 Multiple Launch Rocket System (MLRS) na HIMARS. Lina uzito wa kg 1,670.
 
Duh! Zaidi ya Uzito wa metric Tani moja na nusu, likianguka mahali tu kishindo chake si ni balaa aisee. Ole ni kwa Mrussi ambaye ndio mlengwa.
Asante kwa ufafanuzi.
 
Ndo utakuwa mwisho wa hii Vita.
Amina kaka. Lau ikitokea hivyo tutamshukuru sana Mungu kwani hakuna vita nzuri hata siku moja;
Japo sina undugu na Ukraine, lakini najua thamani ya binadamu na huko wapo binadamu wenzangu kama mm. Haipendezi wakateseka kutokana na uamuzi wa mtu mmoja kuanzisha vita - kitu ambacho kingeliweza kuepukika. Inasikitisha na kuhuzunisha sana kunapokuwepo kwa vita isiyo na sababu za kimsingi. Eti sitaki jirani yangu awe rafiki na fulani. Ndicho anachadai Putin.
 
Uonevu tu. Hata Marekani wanapakana, mbona hamletei kibesi? Ukraine ina ardhi yenye rutuba, anaitamani sana. Kilimo kinakubali.. Ndo maana ni nchi ndogo ila inalisha Dunia kuanzia mafuta ya alizeti, ngano nadi viazi vya chips. Ina chuma pia tena cha pua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…