Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Huyo mwanasiasa ni muflisi kisiasa. Anakumbuka shuka wakati kumekucha. Urussi ndo imeshalegezwa na kilichobaki sasa ni kupigwa kama ngoma.
1. Yule muuaji (Wagner) mwenyewe amekiri kwamba hii ngoma ni nzito - Mrussi itamchukua muda zaidi miaka 2 kufikia lengo lake.
2. Ukraine kila uchao anazidi kupata support ya kimataifa dunia nzima
3. Kipigo anachopata Mrussi kwa sasa si cha kawaida e.g. Brigade 155 Guards Naval infantry... yote Imeteketezwa
4. Zipo ishara za wazi e.g. wanasiasa kuchoshwa na vita kitu ambacho kitaua kabisa morale wa askari na mbaya zaidi morali kwa Raia wa Urussi.
Katika hali kama hiyo ni rahisi kuanzisha kundi la vuguvugu kuiondoa Serikali iliyopo madarakani(Mapinduzi).
****5. Zipo tetesi katika baadhi ya mitandao kwamba Putin aliyeko madarakani kwa sasa sio Putin Original. Huyu wamemwita Putin Double.
Tafadhali, mwenye abc za hii kitu atufumbue macho na kututanabahisha hii kitu inamaanisha nini.(Wameweka hata picha zao Original Putin na Putin Double ) e.g. Hiyo picha hapo juu ni Putin Double sio Putin Original.


Original Putin (left) and Putin’s Double (right)?
 
Wangemteka kabisa,waombe dau ili wamkabidhi kwa zele mchezo uishe.
 
Kupitia nyuso za mashujaa hawa unaweza kupata picha halisi ya mapigano,
Haiwezekani vikosi vyenu viwe vinateketezwa,alafu wengine wawe na furaha namna hii.
Naomba ujumbe huu uwafikie pro-russia.
Mungu ibarike Ukraine.
 
Kwa mujibu wa taarifa hii una maana;

1. Zaidi ya wanajeshi 3,000 wameuawa direction ya Vuhledar peke yake?

2. Full Brigade ina zaidi ya askari 3,000, kama Brigade hiyo imefutwa yote maana yake direction ya Vuhledar hakuna resistance tena?

3. Kama maelezo ya kifungu (2) ni sahihi, majeshi ya Ukraine yamekomboa miji ipi direction ya Vuhledar.?

4. Kama hakuna miji ambayo Ukraine imeikomboa direction ya Vuhledar, majeshi yetu hawahitaji tena kukomboa maeneo hayo na kwamba wamewasubiri wengine waje ndo waendeleze mapigano.?

Naomba kueleweshwa tu maana taarifa hii imenistua kidogo. Nikipata source nitafurahi sana.
 
Vuhledar ipo mikononi mwa Ukraine, Warusi walikuwa wanajaribu kupiga operesheni kule kuitwaa. Wakakutana na resistance kali, Askari na vifaa vyao vizito vya kijeshi vikaangamizwa. Kwa hiyo Vuhledar sasa pako shwari

Na Kule Bakhmut , Intensity ya mashambulizi ya Warusi imepungua sana. Ukraine imepeleka re-inforcements za kutosha na Zelensky amesema wazi kuwa Ukraine haitoiachia Bakhmut!
 
Naona kama hujaelewa hoja yangu, huenda ulisoma kwa haraka haraka. Naomba urudie kunisoma tena ndo ujibu hoja. Ikikupendeza ujibu kwa mtiririko wa maswali yangu.
 
Naona kama hujaelewa hoja yangu, huenda ulisoma kwa haraka haraka. Naomba urudie kunisoma tena ndo ujibu hoja. Ikikupendeza ujibu kwa mtiririko wa maswali yangu.
Mkuu Sehemu ikiwa Vitani, hauwezi sema mumeikomboa kama hawajasurrender au kuretreat. Hata kama Brigade nzima wamekufa. Ipo hivi, Frontline akifa mtu analetwa mtu.

Pia mjini Ukraine haitumii silaha nzito kama ifanyavyo Urusi, sababu kuna wananchi na tunaogopa kuua watu wetu hivyo mjini mtu unaingia kwa taratibu kama unaua mbu alietua kwenye korodani sababu ukitumia nguvu unaua waukraine ukizingatia Urusi wanajificha kwenye makazi ya watu.

Hivyo hadi msafishe kabisa ndo mrangaze kukpmboa. Huwezi sema mumekomboa wakati bado kuna sehemu kuna adui. Sehemu kuwa chini ya jeshi maana yake mumekamata anga, ardhi na maji kiasi kwamba nzi hakatizi. Vuhledar bado kuna mapambano japo ipo chini ya Ukraine. Nashindwa nikufafanulieje. Wewe una nyumba yako upo ndani mwizi yupo nje anataka kuingia. Huwezi sema una amani hadi pale mwizi atakapoondoka. Lazima ufunge milango vizuri. Kuna sehemu mwizi yupo ndani wewe nje unapigana kumtoa nje uingie. Vuhledar Mrusi yupo nje anapambana kuingia. Hajakata tamaa, Wananchi bado wanajificha kwenye mahanadaki.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…