Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Vipi kuhusu ATCAMS.
Nasikia USA kazingua kuzitoa. Hii itakuwaje?
Walishaahidi kutoa. Hayo mengine ni mbinu za kijeshi. Kama umeona, USA imempa ATACMS Poland eti ijilinde dhidi ya Belarusi. Poland hakuna Vita. Pia kuna Wanajeshi wa Ukraine wapo training Poland jinsi ya kutumia ATACMS. Ila hadi sasa sijasikia ATACMS zipo Ukraine. Ila nategemea hizo anapewa Poland ndo Ukreina.
 
Vipi kuhusu ATCAMS.
Nasikia USA kazingua kuzitoa. Hii itakuwaje?
Huu mzigo uloshuka ambao kuna M2 Bradley IFVs, HMMWVs na AN/TWQ-1 Avenger version, ngoja tuone Ubora wake. Kama kutakuwa na mabadiliko. Nadhani hatua kwa hatua. Ngoja kazi ipigwe mwezi ndo tutajua ubora kabla ya kulalamika sana. Kipindi Urusi amechachamaa na Drone zake za Iran aina ya Shahed-136, Ujerumani alitoa Silaha inaitwa Gepard self-propelled air defense systems. Tukalalamika sana kwamba sio silaha nzito. Baada ya wiki tukaona Mafanikio, sasa hivi Drone za Urusi sio tishio tena. Gepard moja inaweza angusha hata drone 30. Japo sio nyingi ila kila sehemu yenye Miundombinu sasa hivi kuna Gepard japo hakuna za kutosheleza Nchi nzima.
800px-Cheetah_PRTL.jpg
800px-Gepard_1a2_sideview.jpg
800px-Gepard_1a2_v0-mess.jpg
Gepard_1a2_overview.jpg

Hii ndo Gepard
 
Marekani wamefanikiwa kutengeneza miwani inayowezesha kuona Usiku aina ya ENVG-B night vision. Miwani hii inasaiddi kuona kukiwa na Vumbi, moshi, giza nene hata mtu akiwa chini ya ardhi. Hii miwani itawezesha Ukraine kupigana usiku na mchana.
 
Back
Top Bottom