Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Hahaaa... Umenikumbusha November 2022 kuna Bomu lilitua Poland kwa bahati mbaya. Lile bomu lilikuwa la Ukraine, walikuwa wanatungua drones za Urusi, wakakosea target bomu likaenda moja kwa moja hadi Poland.

Zelensky kuwajambisha akasema Urusi wameanza kuishambulia Europe. Hiyo taarifa ilikanwa na Viongozi 12 wa Urusi kila mtu anasema sio wao.. Hahaaaa... Walijua ukishambulia Nchi yoyote ya NATO, wote wanaungana kukupiga. So Urusi walijua wamefanyiwa figisu. Walilialia sana
Biden aliposema kuwa siyo Russia walimshukuru sana kitu ambacho siyo cha kawaida adui yako kukushukuru. 😂😂😂

Zele aliwatupia zigo 😂😂😂 walihaha sana
 
Ok,labda ikiwa Urusi hasapoti mpango huo, je hilo linatosha kumpa uhalali wa kuivamia Ukraine, kuua, kaharibu makaazi,...nk????
Bwana@Ngoke amsikilize mwakyembe ili afanye maamuzi ya kuihama au kubaki kwenye nchi yake mwenyewe,haramu ni haramu na haki ni haki. Putini anataka kutumia hiyo njia kupata support ya ulimwengu.
 
Niambie kampuni yoyote ya kirusi iliyofanya kazi tanzania ikawalipa wafanyakazi wake vizuri wakawa na maendeleo,
Binafsi natumia sana kigezo hicho kupima uwezo na utu wa mtu.
Hata kwako nyumbani,huwezi kuniambia una uwezo mkubwa wakati house girl/boy wako ana mba kichwani.
Kwanza unafurahisha kiasi chake yani kwanini isiwe tanzania ikawa na makampuni yake nje ili iwalipe wengine hua najiuliza tu kutoka nje kwa viwango vizuri na vya maana?

Alafu hujui kua juzi tu russia imefanya wema wa kusamehe deni la afrika karibu doller 20 bilioni za kimarekani.

Masikin kapata wapi hizo nguvu za kusamehe deni kubwa namna hiyo na uchumi wake pia haujayumba.

Jengine kufikia 2024 wafanyakazi wa urusi wataongezewa mishahara yao kwa asilimia 18 na jiulize lengo la vikwazo lilikua ni uchumi udolole lakin kumbe ndio unakua mpaka mishahara inatarajiwa kuongezwa.

Masikini hizo nguvu zote anatoa wapi najiuliza tu?
 
Kazi imeanza. Urusi kaeni chonjo. Ukriane itarudisha ardhi yake yote iliyovamiwa. Urusi ni sawa na Jirani anapiga muziki kwa sauti then unaenda kumpiga na kuchukua ardhi yake kisa wewe una uwezo..
 
Ujerumani imeshapeleka mzigo Ukraine na umepokelewa Jumatatu hiii. Ndiyo kifaru bora kwa sasa duniani.

Kilomita 500 ni kama Dar mpaka Karibu na Mwanga mkoani Kilimanjaro.

INTERACTIVE_UKRAINE_LEOPARD_2_TANKS_JAN25.png

Chanzo Aljazeera!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] taarifa inasema Germany wamekubali kuwapa Ukraine hizo tanks. Wew unasema wametuma. Anyway Germany wamekubali kuwapa Ukraine tanks toka late January ila bado havijafika [emoji41]. 500km max range ni uwezo wa tank kutembea bila kujaza mafuta
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] taarifa inasema Germany wamekubali kuwapa Ukraine hizo tanks. Wew unasema wametuma. Anyway Germany wamekubali kuwapa Ukraine tanks toka late January ila bado havijafika [emoji41]. 500km max range ni uwezo wa tank kutembea bila kujaza mafuta
Vimefika. Pia Hispania imetuma Leopard 2 idadi ni 6. Vipo Ukraine. Pia na ureno imeleta mzigo wa Leopards

Nyie mnataka mjue vipo sehemu gani. Hatusemi ila ni mashariki na kusini mwa nchi.
 
Kauli za hawa watu si za kubeza hata kidogo.

1. Kitendo cha Prigozhin kukiri kuwa Wagner PMC wamepata badly demage (been pretty battered) in Bakhmut ni ushahidi kuwa Bakhmut imegeuka kuwa slaughter-fest kwa Wagner/Russia troops. Japo pia kasema kuwa eti ame destroy Ukrainian army. Swali la kujiuliza, kama ame destroy Ukrainian army mbona hajaiteka Bakhmut?

2. Putin amekiri kuwa ni kweli vikwazo alivyowekewa Russia vimeleta "negative consequences" na kwamba tatizo la kukosekana kwa ajira litaendelea kuwepo japo kwa kiwago kidogo.

Kauli hizi mbili zinatupa picha kuwa sasa Putin na Prigozhin wameanza kuusema ukweli.

Pili vita hii ikiendelea uchumi wake utaanguka. Tatizo la unemployment litaongezeka na warusi wataanza kupiga kelele.

Tatu, Prigozhin anakiri kuwa vita hii ni ngumu na watashindwa.

Tuvute subira tu ipo siku wataamua kuondoa majeshi yao kimya kimya maana ukweli wameshaujua kuwa vita hii hawashindi.
 
Back
Top Bottom