Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Wakuu, Warusi leo wameanza kuukimbia Mji wa Izyum. Eti wanaenda kujipanga upya Katika Wilaya ya Severodonetsk iliyopo Mkoani Luhansk. Umbali wa KM 130 kutoka Izyum. Naamini hadi Jumatatu Ukraine itakuwa imeukomboa Mji Mungu akipenda. Umeona wameogopa kupitia Njia ya Karibu ya km 128 Wilayani Borova coz kuna Mtego wa Ukraine, wameamua kuzunguka Svyatohirsk km 131. Ndo wanaondoka hivyo, hata wajipange vipi, Izyum hawaipati tena.
 
Ukraine imefanya kazi nzuri Izyum na kufanikiwa kukamata Wafanyakazi wa Jeshi la Urusi 390(Hawa ni Wapishi, Wahandisi, Mafundi, Madaktari) Vifaru vya kubebea Wanajeshi 11, Vifaru aina ya BTR-5 Vifaru aina ya BMP-11 Vifaru aina ya BMD-1 Vifaru aina ya MTLB-2, Artillery systems-4 Vifaru aina ya MLRS-1, Mortar-10 Malori ya Mizigo 8 Ndege zisizo na rubani (UAV)-5

Picha nitaweka kadili nitakavyo pata kutokea Izyum
 
Kikosi cha Ukraine cha 95th Air Assault Brigade kimeonesha Vifaru vya Urusi Vilivyo haribiwa aina ya BTR-82, BMP-2, T-72B, na T-72B3.
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi hawaoni kama wanajiaibisha kwa hii vita? Yaani wamepigwa kama watoto wadogo.
 
Magari ya Jeshi la Urusi aina ya Tigr yakiwa hoi
Your browser is not able to display this video.
 
Sasa urusi si ni taifa la hatari kijeshi na intelijensia si wampige mmarekani tu!?[emoji16][emoji16]
Shida ni kwamba hawakujua kama Mmarekani anawajua kuliko wanavyomjua,kabla vita haijaanza kuna kamanda wao(Russia) alisema Marekani kwenye tech ya kijeshi na Idara ya Afya wako juu sana hawawezi kujilinganisha nao.

Putin alitakiwa aelewe ujumbe wa Kamanda wake. Wanajeshi wake hawana morale sana compared to Ukranians.Wakitoka hapo Donetsk lazima wasogee mpaka Crimea na kuikomboa.
 
Rais wa Uturuki anataka kutuma Nyambizi Mariupol kuwaokoa Azov Majeruhi. Je, atafanikiwa?
View attachment 2224920
Mpaka kusema hivyo inawezekana ameshapima ukubwa wa jambo analotaka kulifanya. Turkey kwenye intelijensia wapo vizuri itakuwa tayari wameshausoma mchezo.

Hata alivyokataa kupiga kura Finland na Sweden kujiunga na NATO alishapima na anajua matokeo yake.Hapa Mrussi anazungukwa na kuchezewa mchezo.
 
Nimekuelewa mkuu. Wakitumia ndege zitadunguliwa maana Ukrain inamiliki anga lake. Kazi imeanza.
 
Kurudishwa nyuma kwa sehemu uliyokuwa umeishirikia kwa muda na umejijenga kijeshi ni udhaifu na mwanzo wa kuanza kumuogopa adui yako.Wanajipanga huku wenzao wanakuja pasipo kurudi nyuma.
 
Silaha zake ndizo zitatumika kumpiga.
 
Kuna hiki kifaru cha Urusi kinaitwa BAT-2. Ni vifaru adimu, tangu vita ianze hiki ni cha pili kukamatwa. Ni vifaru vya gharama sana. Hata Urusi ukute wameleta visivyozidi 10. Kimekamatwa. wenyewe wanakiita BAT-2 heavy engineering vehicle
 
Sasa hawa wanakimbia Vifaa vya Jeshi walikuwa wanamuachia nani? Urusi bana.. Wote hawa Wamadakwa na vifaa vyao.

Hapo kuna kifaru aina ya MT-LBVM, Risasi za Kila aina, NSV HMG - hii salaha ina majina ya Walioitengeneza, Kirefu chake ni (Nikitin, Sokolov, and Volkov heavy machine gun), na Vilipuzi vya aina mbalimbali vya kulipua vifaru kama (RPG-30, RPG-26 na MRO-A )
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…