Urusi muda mwingine wanakera sana, hii vita watashindwa kwa ujinga wao wa kutotumia silaha nzito kumaliza hii vita.
Au Urusi hana hizo silaha nzito kama tunavyoaminishwa?
Anaruhusuje wanajeshi wake wanateketea kwa wingi hivyo?
Anaruhusuje eneo wanaloteka, linakombolewa tena?
Hii vita ukraine inakuwa magofu, imeanguka kiuchumi, watu wanakufa ila Urusi na yeye anapata hasara kubwa sana kupoteza idadi ya wanajeshi wengi, vifaa n.k.
Gap analotoa Urusi kwa ukraine kujipanga, kupokea misaada ya vita na mafunzo, litamcost sana Urusi.
Na sijawahi kuona vita ambayo unampa adui nafasi ya kujipanga halafu akurudishe tena nyuma.
Hii vita ni ya kijinga sana.