West ndio wana control na ku run Dunia.. kuanzia Politically, socially and economically ndio maana nchi ikiishiwa reserve ya pesa ya Dollar inakuwa imefilisika automatically lakini nchi haitakiwi kuwa na Rubble ya Russia sababu haina maana. USA na West wana nguvu kuanzia kwenye pesa yao.
Sitarajii kwa namna yeyote ile Russia kuwashinda mabavu West wakiamua full scale war kwa sasa ukizingatia zaidi ya nusu ya Professional army toka Russia imefyekwa na Ukraine pekee.
Ni mtu mjinga tu anayeweza kupingana na ukweli kuwa;
1. USA ndo mbabe wa dunia hii kiuchumi, Kijeshi na maswala ya kiusalama (Intelligence & security services).
2. Kiuchumi peke yake Russia hayupo kwenye top 10 ya nchi Tajiri Duniani. Kwa mwaka 2022 tu, GDP ya USA ni zaidi ya mara 14 ya GDP ya Russia. Yaani USA GDP ni USD 20.89 Trillion against USD 1.48 Trillion for Russia.
3. Ni mtu mjinga au mwendawazimu anayeweza kuamini kuwa Russia anaweza kupigana na nchi zote tajiri tena zinazomzidi kiuchumi na akashinda vita. Yaani USA, Canada, UK, Japan, Italy, German and France.
4. Hakuna anayebisha kuwa ukilinganisha Military power (Firepower index) ya USA na Russia tofauti yao siyo kubwa. Mtu anayeiangalia vita hii kwa kulinganisha firepower index na kumwona Russia ni wa pili baada ya USA na kuamini kuwa hicho ndo kigezo cha Russia kushinda vita hii nitamwona kuwa ni mjinga ambaye hajaelimika na hajui maana ya vita. Kwa kulitambua hilo mzee Biden alizishawishi nchi zote za EU kuisaidia Ukraine siyo kwa bahati mbaya. Ni issue ya kimahesabu tu.
(i) Mosi, ili vikwazo vyovyote atakavyowekewa Russia vifanye kazi lazima nchi anazofanya nazo biashara zikatae kupata huduma yake ili akose pesa. Hilo limefanikiwa kwa 100%
(ii) kuunganisha nguvu kutamdhoofisha Russia kiuchumi na uchumi wake usinyae. Hilo sasa ndo linalomfanya Putin ahahe kumbembeleza China afanye naye biashara.
(iii) ku prolong vita hii ni mbinu ya kumtesa Russia ili ashindwe ku finance vita sababu uchumi wake utakuwa umesinyaa.
(iv) kuunganisha nguvu kwa mataifa haya kushughulika na Russia ni mbinu ya kumpunguzia nguvu ya kijeshi. Russia inaenda kuanguka kama USSR.
5. Kumaliza vita hii mapema ni kama unamhurumia Russia. USA na German wanalijua hili. Ndiyo maana hawataki kumpa Ukraine silaha nzito za kumaliza vita hii mapema. Vita hii haitaisha mapema kama wengi wanavyoamini. Ni lazima Russia aishiwe nguvu za kijeshi ndo itaisha vita hii. Wanachofanya USA ni ku minimize demage kwa Ukraine. Lakini vita hii haishi mwaka huu ni mpaka Putin atepete kijeshi ndo itaisha.
6. Kama Russia atatoa silaha nzito za kukabiliana na Bradley, challenger na Leopard 2, then USA na German wataleta silaha nzito zaidi. Kiufupi mgonjwa (Russia) atapewa dozi kulingana na hali ya wakati husika.
Hitimisho
1. Russia alishanasa kwenye mtego wa USA & NATO hataweza kujinasua na kuangushwa kijeshi na kiuchumi.
2. Vita hii haitaisha mwaka huu. Hii ni vita ya muda mrefu mpaka Russia adhoofike ndo vita itaisha.