SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

NACHOMEKEA TU: Katika nchi za middle east nchi inayoongoza kua na population kubwa ya wayahudi ni Iran, ikifuatiwa na Morocco na Egypt. Sasa hapo utaelewa kua, Mossad kuweka kiwanda cha drones Iran ilikua ni sawa na kumpiga mlevi. Royal family ya Saudi Arabia wana damu ya kiyahudi kwahio hapo utaelewa kwanini Saudi wapo kimyaaa. Hao Morocco hadi bendera yao ina "The star of David" ikiwa katika rangi ya kijani. Kwahio usaidizi wa Israel upo kila sehemu hadi huko huko Arab world ila mmatumbi wa kizuramimba anadhani Israel itasimamishwa na Iran, bila hata US huu muziki wa Netanyahu ni munene sana.
 
Hii vita ni ngumu kwasababu iran hata akipigwa vipi hawezi kukubali kuabiki kwenye dunia ya kiislam kwamba kashindwa na wazayuni


Ni wananchi wa iran wenyewe watabadilisha mkondo wa vita

Wananchi wa iran wakiamua kuandamana km walivyofanya mwaka juzi utawala wa kigaidi utaanguka

Au ule utawala uliopinduliwa 1979 urejeshwe ikulu

Yasipotokea hayo ni kuwa ayatolah atabaki na baada ya muda mfupi watakuwa nchi ya kiimla km korea

iran kupitia putin na macron imeomba vita ismame kwa muda
Huu ni ujanja wa iran kutaka kuthibiti anga yake

Usa anataka kuingia kwenye vita direct ila tatizo akiingia kwenye vita atakosa nafasi ya kuwa msuluhishi uko mbeleni

Hapa kuna mtihani sio poa,subiri tuone wenye akili kunizidi watafanya nn
 
Da!! naiona serikali ya IRAN ikiangushwa,,,hamna ujanja,,
 
Katika post zako zote hii ndio umeongea uhalisia namna ulivyo. Kitu ambacho nadhani wayahud n Israel wamefeli nikua walidhani wakiishambulia Iran wananch wataandamana lakini hao ni Persians kwenye mambo ya vita huwa wanaungana na kibaya zaidi Israel and USA wanaona shida ni Iran nasio Ayatollah. Kwahio hapo ni pagumu. Israel imejaribu kupiga Vinu vya Nuclear lakini haijafanikiwa, Kama wakifanikiwa bas Iran nae naamin atapiga kinu cha Israel jambo ambalo litakua baya kwa pande zote.

Jambo lingine ningumu kuivamia Iran aridhin kulingana na Jografia yake, pia ikienda vita ya muda mrefu Israel hataweza kuhimili kulingana na nchi yao ni ndogo kieneo kulinganisha na Iran, pia population ya Iran nikubwa kuliko Israel na bahati mbaya Uturuki anaonekana hakubalian na alichokifanya Israel jambo ambalo linaleta ugumu. Kuna baadhi ya taarifa zisizo rasmi zinasema agents wa URUSI wanafanya kazi ya kurestore ADS software kutokea Uturuki.

Russia na France naona Wana approach nzuri kuliko USA juu ya kumaliza hivi vita.


Ngoja tuone lkn I can bet, Iran itapigwa USA& ISRAEL watatumia tactical nuclear kumkalisha lakini sio jambo dogo, Maana 20% ya mafuta ya China yanatokea hapo Iran kwahio mchina atamsaidia IRAN hata kwa njia za panya.
 
Hakuna damu ya kiyahudi,huwezi kuwa na damu ya kikristu au kiislam,uyahudi ni imani,imani haina damu
 
Ni Kweli sio ya kidini. Lakini amini usiamini all Musilims wapo na Iran. Na wale wakristu wapo na Mazayuni. Huo ndio ukweli.
 

Wananchi wengi hawapend utawala wa ayatollah ila jeshi la ayatollah la kiislam liwathibit vibaya sana

Iran ilizima internet kwasababu jumamos vijana walianza ku organize mtandaoni kufanya maandamano na wale vinara wanawindwa wanakatwa kichwa
Wapinzan wengi wanaishi ulaya kwa sasa iran yamebak manyani km tanzania

So hii vita ni mtego

Israel na china wanaurafiki nyuma ya pazia ndio maana israel hajashambulia meli znazobeba mzigo wa china

Ninavyojua ayatollah hawez kukubali kukaa meza moja na usa kusuluhisha ata prefer kufa km shahid kwa mujib wa mwamed😁
 
Yani makombora ya IRAN yana anzia kuwindwa Iraq ,Jordan na ndani ya israel na bado yana penya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…