SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Umeisoma comment yangu au umekurupuka kujibu?
Nimesema nchi yoyote inayoinuka kijeshi huku iko kinyume na matakwa ya NATO huwa lazima ikumbane na vikwazo vya kiuchumi maana majeshi bila uchumi hakuna kitu utafanya.

China walikuwa wajanja walianza kujenga uchumi baada ya kukua ndio wameingia kwenye majeshi sasa.
Kama haukubaliani na hilo toa mfano wa nchi moja tu duniani ambayo imekuwa kijeshi ikiwa kinyume na NATO halafu haijakumbana na vikwazo vya kiuchumi
Unafahamu kuwa China imewahi kupigana na marekani ?
 
Hao wote wamedhoofiishwa kuliko ilivyokuwa mwanzo Hezbullah hakuwa mtu wa kuisikiliza Serikali ya Lebanon ila baada ya mkong'oto saa hizi ana adabu, Houth anakaribia wiki hakuna kombora pale Ben Gurion, Hamas ndo wamebaki kugombea chakula cha wana Gaza.
Huwa mnaandika kwa kufikiria? Au kwa ushabiki?
 
Ukraine ilikuwa ikilenga high ranking officials wa Russian army mwanzoni mwa vita hakuna walicho achieve wakaona upuuzi maana hawakuweza na mpaka sasa hawajaweza kuwatoa Russia katika ardhi yao kwa hiyo mbinu yao.

Tuachane na Ukraine tuje kwa IDF wamelenga high rank officials wa Hamas mpaka sasa ipi Military objective wame achieve iliyo wapeleka Gaza ? Vita imeisha ?, mateka wamewakomboa ? Hamas wame waangamiza ?

Kuwalenga high ranking officials sio kumaliza vita au kunyong'onyesha nguvu ya jeshi itategemeana na hali ya mapambano,muundo wa jeshi,mafunzo,malengo ya jeshi husika unalo pambana nalo na pia uimara wake
Mnaweza kuwa na objective moja ila mmoja aka achieve na mwingine aka fail, ingekuwa hivyo unavyo fikiri nazani IDF wangekuwa wamewaza hilo kabla yako wewe ambaye hata panga la kumtisha kibaka akikuvamia usiku huna ila bonge la mjuaji kichwa empty
 
Kuna jamaa Mmoja hapa kasema Israel inaenda Iran kuchukua nchi, nimecheka sana😂 nikifikiria hayo makundi yanavyo mhenyesha Israel Iran ndiyo ataweza?
7, October, 2023. Hamas aliingia akawakamata watu wake akaondoka nao, na mpaka Leo baado anawashikiria mateka, Tulidanganywa na Netanyahu ndani ya siku 7 atawasambaratisha, mpaka Leo Miaka miwili Hamas baado wapo wanadunda tu, Israel ameishia kuwaua watoto, wazee na kuangusha maghorofa basi. Lakini Hamas ni kama ameshindwa.

Ndiyo tufanye ulingañifu kama Gaza kasehemu kadogo tu kijiografia ameshindwa! Je ndiyo ataweza Iran ambayo kijiografia ni nchi kubwa na wako vizuri kijeshi, siyo kama hao Hamas wa kuunga unga.

Au tuendelee kusikia propaganda!!
Kuchukua nchi ya iran ni ngumu,
Na uwezi kufanikiwa kwa jeshi la anga
Ni jeshi la ardhini tu ndo linaweza wanachokifafanya Israel ni kuziofisha jeshi iran.
Ndo hicho tuu
 
kwa hiyo wayahudi wanaoishi uarabuni na iran ndo wako nyadhifa za juu?
Ndio Ki historia wayahudi wameshika nyadhifa kubwa kubwa kwenye Dola za Middle East, na mpaka sasa kuna wayahudi wengi Tu waarabu, Wairan wenye vyeo na nafasi,

Hapo Iran kuanzia wanasiasa, matajiri, wanasayansi etc wapo wayahudi.
 
Hv kuna mtu kabisa anashangilia kuwa iran atatoboa 😁😁😁 , Iran anajitahdi kueliminate defence ya israel before is too late , mana anajua Israel lengo lake ni kuwaondoa viongozi tegemewa wa kijeshi wa iran wenye future na Irani akiwemo na Ayatolah , kitu ambacho irani anajua kipo ndani ya uwezo wa Israel , ndo mana israel anasema tuu simple kuwa Vita itachukua mda mrefu
 
Maana Kuna mtu katuambia iran wana makombola ya kutuma miaka mitatu 😁😁😁😁😁😂😂😂🤣🤣🤣

Sasa kwa matumizi Yao inamaana wanayo zaidi ya 100k
😁😁🤣🤣😂
Ukiwa humu lazima uwe na air defense zuri kichwani maana makombora na drone zinazotumwa humu some time ni sumu zinaweza kuondoka na wewe
 
Samahani wakuu kwa siku Iran ina uwezo wa kuzalisha makombora mangapi kwa makadirio ? Na inaweza rusha makombora mangapi kwa siku endapo vita vikiwa vya muda mrefu tufanye makisio kama vita vikienda miaka zaidi ya mitano ?
Haviwezi vita Kufika Miaka 5 unless Mataifa mengine yaingie kusaidia Israel. As of now Israel ana uwezo wa kupigana wiki kadhaa tu, ndio maana wao wanataka vita viishe Haraka na Iran anavirefusha.

Hakuna anaejua Iran ana makombora mangapi, pia wana makombora na silaha nyingi zenye quality tofauti tofauti. Kwa makombora makubwa kama hayo ambayo kombora moja linachanguka na kuwa makombora 26 obvious atakua machache ndio maana pia wanapiga sehemu maalum tu.

Ila kwa yale makombora chawa ambayo alikua anatumia Mwanzo Iran pengine ana stock kubwa inayozidi hata 10k,

Pia silaha Nyengine ambayo haizungumzwi ni Drone za Iran, vile anavitengeneza kama sisimizi, Urusi tu katumia zaidi ya 8000 vita vya Ukraine

Hizi drones hata Apache zinapata shida kuzi intercept, zinapiga sana Israel sasa hivi na nyingi hata Alarm hairaise.
 
Ila hizi vita za kisasa bwana ni vichekesho yaani unamtangazia adui yako kuwa utashambulia saa ngapi na maeneo gani haya maendeleo ya vita za kisasa ya ajabu sana na ya kufurahisha
Vita vipo Africa tu huko kwingine maigizo, week tu na makaburi ya halaiki kila kona
 
Back
Top Bottom