Mkuu hapa hatujadili ninani yuko sahihi au nani asiye sahihi.
Maana Ukraine na Urusi wote wako sahihi kwa minajili ya maslahi yao .
Upande wa Ukraine una pigana kulinda mipaka na uhuru wa nchi yao na upande wa Urusi inapigana kuhakikisha mipaka yake ina baki salama ,na mshindi ni yule atake hakikisha ana timiza kile alicho enda kupigania.
Unanichekesha sana, yaani unaona ni sawa kwa raisi wa Ukraine tuteketeza maelfu ya vijana wa nchi yake na miundo mbinu waliyo ijenga kwa miongo kadhaa kwa ajili ya kulitetea taifa lao ,ila hapo hapo unaona si sahihi kwa Putin kuteketeza vijana wake kwa ajili ya usalama na maslahi ya taifa lake?
Mwana jeshi hajawa mwana jeshi kwa ajili ya kuvaa magwanda na kubebelea bunduki kama pambo, bali yupo kwa ajili la kufa akipigania maslahi ya taifa lake lililo mlea kwa hiyo hata akifa hakuna mjadala juu ya hilo.
Hata sisi tuna vijana wetu hapo kongo na mpaka sasa ni zaidi ya vijana kalibia 40 wamesha uawa hao vijana walikuwa na familia,wazazi ,marafiki walio wapenda lakini walikufa kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa na hilo ni jukumu lao na wala sio ombi.