RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,422
- 7,173
Mkuu mbona una jenga hoja za kuchekesha na kusadikika?Naomba usome nilichoandika juu kuhusu swali la mshindi. Nilimjibu mchangiaji aliyemwona Putin kama mshindi, hapa sijagusa swali la haki. Nilisema sidhani kutakuwa na mshindi kweli, nikataja vifo upande wa ukraine pia.
Nakubali Zelensky angeweza kusema waziwazi zaidi anachosema sasa, ambacho alitamka pia lakini si kwa maneno ya wazi vile.
Hata hivyo, hadi sasa naona tofauti kidogo. Nisipokosei wanajeshi wengi (sisemi wote) wa Ukraine walijitolea kutetea nchi, hawakupigania kama watu wanaolazimishwa.
Upande mwingine sina sababu ya kutia shaka taarifa zote kwamba sehemu ya askari wa Kirusi (sisemi wote) hawakuambiwa wanatumwa wapi, hawakulizwa kama wako tayari kupigania vita ya mashambulio, na walichoambiwa kuhusu serikali ya Neo-Nazi na kutetea raia Warusi wa Ukraine ilikuwa uwongo mtupu. Na udhaifu ulionekana upande wa jeshi la kirusi unalingana na idadi kubwa ya askari ambao hawakuwa na moyo wa kupigania...
Ya kwamba wanajeshi wa Urusi hawa kuulizwa kama wako tiyari kwa mapigano?
Kwa hiyo siku hizi wanajeshi wakitaka kutumwa vitani wana ulizwa kwanza kama wako tayari au la ?mm ndo nalisika kwako leo,sasa je wakisema hawataki una ahilisha vita.
Mwana jeshi kwenda vitani huwa sio ombi huwa ni lazima kwa sababu ni jukumu lake tena la razima, na ndio maana sheria namba moja jeshini hutakiwi kihoji amri unayo pewa jukumu lako ni kutekeleza basi.
Mkuu una chuki sana na Urusi sijajua ni kwann ,lakini hatua alizo chukua Urusi zingechukuliwa na nchi yeyote ile iwapo usalama wake ungekuwa mashakani, wakiwemo hao wamagharibi unao waona watakatifu.
Katika maisha yako ukitaka kuwa salama jifunze kucheza mbali na maslahi ya wenye nguvu.