Kuna kitu kingine huwa nashangaa kwenye huu uzi hasa kutoka upande wafuasi wa magharibi. USA na Coalition yake ya NATO washam'declare Russia as their enemy lakin yet wanavunja makubaliano ya awali wanaendelea kujipanua kuelekea kwake.
Biden anasimama kutwambia Russia’s Unprovoked and Unjustified Attack on Ukraine ilihal wao ndio waliolipanga kutoka awali ili kupigana na Russia nje ya mipaka yao. Moja ya kauli hizo ni hapa kwenye hii video.
The same man aliyejitapa wazi bila kupepesa kwamba alituma watu kwenda kulipua Yugoslavia 24th March 1999. Leo anasimama kumuita mwenzie War Criminal, Butcher na mengineyo.
Mshauri wa Zelensky nae ni mmoja wapo wa waliopanga haya yanaoendelea Ukraine, kwa kifupi wameshiriki katika kuwatoa kafara raia wao kuwapa ardhi hao MaGlobalist wa kimagharibi kupigana na Russia kwenye Ardhi yao. Msikilizeni vizuri. Na alitoa hint kati ya 2021/22.
Na katika kubwa ambalo halikuonekana kwa wengine either mahaba au ushabiki, target ya USA na western ni kumwondoa Putin madarakan kama walivofanya kwenye tawala zingine ambazo tunazifaham kama Libya, Iraq na kwingineko walikojarib wakashindwa baada ta Putin kuingilia kati.
Ile kauli ya kusema kua Putin hatakiwi kuongoza haikuwa ya bahati mbaya ile ilikuwa ajenda, Lakini how? Weakening Russia Economy, make people starving, Njaa huwa ni adui mkubwa wa mwanadam [emoji23][emoji23][emoji23] mbele ya njaa nchi haikaliki maana ake yatafanyika mapinduzi kisha utawala utapinduliwa.
Kitu ambacho waliki'underestimate ni Putin's ability to handle matukio kama hivo. Putin ni Jasusi na very tactical, Hana siasa nyingi kama wao kwasabab tayari ashajengewa picha hasi na analijua hilo kutoka kwa hao hao wamagharibi. Anajua anachokifanya na hatimae kaweza kuwaingiza kwenye 'trap' yake.
Ni ipi twendelee kwenye post nyingine uko mbele.