Duniani ogopa Teknolojia na watu.Bwana wewe si mtoto, usilete hapa hoja za kitoto. Ukitaka kushiriki hapa, jielimishe!!
soma Moscow Times: 12 National Guards Appeal Dismissal For Refusing To Invade Ukraine - The Moscow Times
Askari 12 wa National Guard wa Urusi walikataa kwenda Ukraine maana sheria ya ajira yao inasema kazi yao ni kutetea Urusi, si kuingia nchi nyingine. Wako mahakamani sasa wakipinga kuachishwa jeshini.
Pia katika sheria ya kimataifa mambo yamebadilika tangu 1945. Majenerali Wajerumani walihukumiwa kwa jinai za kivita, sheria kimsingi haikubali tena kutekeleza amri yoyote kama ni dhahiri si halali.
Ninajua pia kwamba utaratibu huo unapuuzwa mara nyingi hadi leo, lakini ni angalau misiningi ilianza kuwekwa.
Halafu usitangaze porojo eti ninachukia Urusi. Unajuaje? Kwa sababu nampinga kiongozi mbaya anayeingiza nchi yake katika vita na umaskini mimi nachukia taifa hili kubwa lenye watu wengi wazuri? Waliochangia mema mengi kwa utamaduni wa Dunia?
Tafadhali, washa akili kabla ya kuandika. Naamini unayo ila siasa kali inaweza kuzimisha.
Niongezee kidogo mkuu hapaMkuu punguza hasira na jaziba hapa tunajadiliana na hatufokeani.
Hiihii Urusi inayo ongozwa na dikteta kwa mujibu wako ndio wana jeshi wagome kwenda vitani na waachwe bila ya kupewa kesi ya uhaini?maana hata Marekani baba wa demokrasia huwezi thubutu kukataa amri ya mkuu wako wa jeshi.
Lini watu wenye mitazamo ya kimagharibi mkampenda Putin ? Putin ana kubalika na wananchi wake kwa zaidi ya aslimia 75 wewe ninani mpaka umuone ni kiongozi asiye faa?
Eti una mchukia kwa kuitia nchi umaskini ww maisha ya warusi yana kuhusu nn mpaka huumizwe na ugumu wao wa maisha ?ww kwenye nchi yako isiyo kuwa na vikwazo vya wamagharibi maisha ni rahisi sio?
Na rudia tena katika maisha yako jifunze kucheza mbali mno na maslahi ya wenye nguvu ili ubaki salama tofauti na hapo yata kukuta na wala hizi sheria hazita kusaidia kwa lolote.
Kwanza tatizo la unene uliopitiliza, lipo zaidi Marekani kuliko ulaya.Kaka amka, acha ndoto.Hadi sasa tatizo la Ulaya si njaa, ni unene wa kupindukia.
Gesi iko, uzalishaji unaendelea. Bei zinapanda; walifaulu kuvuka matatizo makali ya UVIKO na lockdown, wanaendelea.
Kama Putin ataamua kweli kufuta mapato yake kwenye mchezo wa Rubel, tutaona karibuni.
Kwa sasa tuombee kwanza amani kwa watu wa Ukraine na wanajeshi wa pande zote mbili. Mauaji yaishe.
Mengine tuone baadaye.