Ila mkuu hata kama unalipwa ila unataka kuzidi unazi.
Yaani mm nikubali kuishi maisha magumu kisa tu kuikomesha nchi fulani?
Hebu tupe ushahidi wa hichi unacho kiongea.
Marekani ana wakataza wenzake kununua mafuta ya Urusi huku yeye akiongoza uagizaji wa mafuta kutoka Urusi.
Marekani ina na mamlaka gani kulazimisha wa EU? Trump alijaribu kukataza Wajerumani wasinunue gesi ya Urusi. Kinyume chake, wakiamini kwamba biashara itajenga amani, walijenga bomba la Nordstream 2 ili wapate gesi ya Urusi. Marekani walilia hadi kupoteza sauti.
Sasa anakuja Bwana Putin na katika siku chache hali inabadilika. Nordstream 2 imekufa, baada ya miezi 4 wanamaliza makaa ya Urusi, mwisho wa mwaka mafuta ya Urusi, gesi wanendelea kuounguza kihatua ili wasiangushe uchumi...
Vilevile Obama na Trump walijaribu kuwalazimisha Wajerumani wawekeze katika jeshi. Walikataa.
Anakuja Bwana Putin, akijionyesha haheshimu sheria ya kimataifa wala kujali mikataba , tayari Ujerumani inatangaza sasa wanatenga € bilioni 100 za ziada kwa jeshi.
Unapata wapi picha hii kwamba Marekani inaweza kuamuru sasa? Kila dalili wananchi wa EU wamemtambua Putin kama hatari kwao. Kwa hiyo wako tayari kujitolea na kutoa sadaka fulani (hadi kiwango gani) kupambana na hatari. Haieleweki?
Hasa wakiona kuna unyama kama Bucha, na Putin anakana tu kinyume ya ushahidi na MASHAHIDI HAI wote,
KAMA angesema bahati mbaya kamanda fulani alikosa, ingekuwa tofauti, au angalau tufanye utafiti wa jeshi letu (jinsi marekani walivyosema baada ya
My Lai huko Vietnam), ingekuwa tofauti, Maana watu wanaelewa, vita ni jhambo baya ianyoamsha unyama nda ni watu, jinai zinatokea pia upande wa Ukraine. Hivyo watu wanaona tu uwongo, uwongo, uwongo, ambayo ni hatari, basi wajikinge.