Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Watu wamekariri kuangalia budget ya US ilivyo kubwa kwenye ulinzi, ndipo wanakariri Russia ipo weak kisa budget[emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hio budget yao ya ulinzi ya Russia ni effective kama hio budget ya USA ilivyo na nikikuambia inatosha kukabiliana na USA na chenji inabaki utashangaa.

Hapa tunazungumzia masuala ya PPP, Russia ni nchi iliyojaaliwa mali asili, wana madini mbali mbali ambayo yanahitajika katika shughuli za kiviwanda za kisasa.
Russia ni nchi tajiri sana kwenye mali asili wana kila aina ya madini kama boron, bauxite, vanadium, titanium sponge, tin, tungsten, potash, sulfur, silicon, rhenium, steel, pig iron, nickel n.k n.k
Hawa jamaa wana oil na natural gas, wana madini yenye thamani kubwa kama copper, ruby, almasi, pia wana makaa ya mawe n.k n.k wana taka taka nyingi sana ya hizi mali asili ardhini.

Russia imekua ikielezwa ndio tajiri kwenye mali asili duniani, japo naweza sema ni moja ya nchi zilizobarikiwa mali asili.

Kuna wengi hawajui hili shirika ambapo founder ni Vladimir Putin mwenyewe, likiitwa Rosatom.

Rosatom ni shirika kubwa sana, hawa jamaa wana teknolojia za kisasa kabisa kwenye masuala mazima ya nuclear energy, ndio shirika linaongoza kwa kutoa huduma za kiteknolojia kwenye masuala ya nguvu za atomiki duniani, hawa jamaa wanachangia kwa 76% duniani kote kwa huduma zao.

Hawa jamaa sio tu wanajihusisha na masuala ya nguvu za nuclear bali pia wana deal na tafiti mbali mbali za kisayansi zisizohusiana na masuala ya nuclear, hawa kwenye tech usiwapimie.
Haya masuala ya nuclear medicine, kama haya masuala ya CT scan, PET scan n.k hawa ndio mambo yao sasa, hapa ni matumizi ya radioactive katika uponyaji na uchunguzaji(diagnosis) kwa ujumla wake.

Hawa jamaa wanahusika pia na nuclear fuel, urutubishaji wa uranium, uchimbaji wa uranium, kutengeneza vinu vya nuclear n.k siwezi list vyote.

Hapo 2020 hawa Rosatom waliingiza uranium hapo USA ambapo ulikuwa ni mchango wa asilimia 16 pia hawa jamaa sio kuuza tu walifanya na urutubishaji wa uranium hio hapo USA.

Nimesema kidogo kuhusu uranium kwa sababu upate picha kamili ya kwamba Russia atatumia gharama ndogo kutengeneza silaha za kisasa, uranium anayo na mpaka anaiuza, Russia anauza uranium yake kwa faida which means USA watatumia gharama kubwa kuwa na silaha ya kisasa aliyonayo Russia, hako ni ka mfano kadogo upande wa uranium tu.

Nitakuja kuelezea kwa undani zaidi, haya masuala ya gas ya Russia na ushawishi wake nilishaweka humu uzi nikaelezea haya yanayotokea hivi sasa kuhusu umuhimu wa Russia kwa nchi za Ulaya, ule uzi utafute una kichwa cha habari Je, Iran inaweza kugeuza Aircraft Carrier za USA kuwa Shipwreck?

Nilizungumzia mambo mengi mengi sana humo.

Sasa kusema Russia ni nchi masikini kisa ina budget ndogo kijeshi wanakosea sana, huwezi kujiuliza kwa nini licha ya budget ya ulinzi ya USA kuwa mara 10 zaifi ya Russia lakini Russia ni nchi ya pili duniani kwa nguvu za kijeshi?[emoji1787][emoji16][emoji16]. China inaizidi Russia budget ya ulinzi.

Taifa la pili duniani kwa nguvu za kijeshi na ambalo linaongoza duniani kwa kumiliki silaha za nuclear unakuja ku comment kabisa eti watapigwa na Ukraine[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nitakuja na uzi wenye facts tupu kuhusiana na huu mgogoro na tutajadili na members humu.

Asante.
Jamii forum ingejaa watu ka nyie kingekuwa kisima cha maarifa watu tukajifunza...

Uko more detailed, unaweza kuzichambua na kuzihusisha taarifa mbali mbali ulizonazo...

Zaidi wajua namna ya kupresent taarifa ikaeleweka hata kwa yule ambae hana ile profession ya kitu unachokizungumzia...

Hongera bro...
Ningekuwa nimekaa nimetulia ningeongeza maelezo mengine kwenye hayo teari ulokwisha eleza...

Ila huu mfano mdogo ngoja nijaribu katika kukazia maelezo yako...

Ni sawa na watu wa dizain hizi mbili...

Wa kwanza ni mwalim mwenye taaluma ya Hesab, Fizikia, Kemia na Baiolojia... Wa pili ana elim ya Hesab pekee. Sasa akipatikana mwanafunzi anaetaka kujifunza masomo ma4 kutoka kwa walim wa aina hizi 2...

Ni kua kwa mwalim wa kwanza atakutana na full package hivo gharama zitakuwa kidogo na itamsaidia kusave mda wake katika mobility kwa sabab kila kitu chapatikana sehem 1.

Ila akienda kwa wa pili itamgharim gharama zaidi na mda vile vile kwasabab itamhitaji kutafta yaliyopelea kutoka sehem aliyolenga kwingineko.

Na kingine mbali na hiyo PPP yani Purchasing Power uliyoidadavua ni kua US kasambaza base nyingi duniani tofauti na Russia. Hivo gharama ya kuzihudumia.

Sawa na Njemba inayolipwa Mil90 kwa mwezi ila ana familia ka 100 hivi umlinganishe na mtu anayelipwa Mil 15 akiwa na familia 1 tu ya kuhudumia katika matumizi.

Af mtu aseme yule mwenye Mil90 anafanya vizuri kuliko huyu mwenye 15 utakuwa ni UZWAZWA.
 
Kichapo kiendelee..[emoji4]
IMG_20220323_184346.jpg
 
Pro Russia wengi sio Realistic kabisa yaani hawashangai Waziri wao wa Ulinzi anavolia Lia Ukraine wasipelekewe Silaha...

Vita na Uchumi ni pipa na mfuniko, huwezi tenganisha... Western countries wao Wana refusha vita, Ukraine yeye Washirika waje ni mataifa Tajiri, Russia washirika wake ni Tanzania na Eritrea.

Kifaru kimoja tu ni Zaidi ya Billion 10 za Tanzania, hapo hujazungumzia makombora, na mizinga mingine... In short na wazungu wanazidi kusogeza muda wa kuachana na Mafuta na Gesi ya Urusi, baada ya miezi kadhaa Soko la Russia la Mafuta linakuwa Nchi masikini za Asia
Tofautisha anaegaiza kifaru au kombora na yule anaetengeneza mwenyewe
 
Mkuu hapo utofauti ni Time-period hata California ilikuwa huru kabla USA hajaivamia na ilatambulika kama Taifa kisheria.

Na huu mfano wa California hauna utofauti na Ukraine,jibu swali rahisi sana Leo hii Urusi akatengeneza propaganda California ikajitenga-kisha waanzishe ushirikiano na Urusi dhidi ya USA wewe ukiwa Rais wa USA utafanyaje???
Hakuna mfano hapo....huwezi kufanaisha kwa huo mfano.
 
Unafahamu kuwa EU Wana clause ya Mutual Defence?

You can not protect your political or economical ideology without any form of Defence.

Mfano AU au EAC sio military alliance lakini mara nyingi wamekuwa na military forces kusaidia Ulinzi kwenye mipaka yake

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nipe source inayoonyesha AU au EAC Wana military forces zinazooperate katika mipaka yake.

Unaizungumzia Lisbon Treaty ambayo haitoi uhakika wa kujilinda au kusaidiwa iwapo vita itatokea kwenye Taifa Mojawapo la Ulaya.

Bado European Union ni muungano usiohusisha mambo ya kiulinzi Bali uchumi brother.
Screenshot_20220426-201038.jpg
 
Back
Top Bottom