Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Izi Ndio habari ambazo dunia inapenda tuzisikie
 
Good for them kama kweli walijiandaa na kumtia uchizi Ukraine!
 
Kuhusu ghala la mafuta walisema ni ajali ya moto. Najua hata hili watatolea kisingizio
Walisema ajari ila baadae CCTV footage zikaonesha blast ya kombora. It seems Ukraine walitumia old modified Tochka cruise missile kushambulia ndani ya kilomita zaidi ya 100 kwenye anga la Urusi. Siku hiyohiyo kuna moto mwingine uliwaka. Huu utakuwa ni moto wa tano kama sikosei, naamini kuna mchanganyiko wa mashambulizi na sabotage.

Concern yangu ni moto unaowaka Siberia ambapo nyika zinawaka moto na wazimaji ndio hao recruits walioenda Ukraine. Russia haina dedicated firefighters wengi ila hutumia jeshi la akiba, hata vifaa vya kuzima moto vingi hutokea jeshini. Siberia huwaka muda wowote ni kama nyanda za Australia
 
Baada ya UK, US na Ujerumani kupeleka silaha Ukraine - Mr Lavrov wa URUSI kasema kitendo hicho ni sawa na kumimina petrol kwenye moto....

Ameonya kwamba huenda dunia ikashuhudia vita vikuu vya 3 vya dunia - na Urusi muda wowote itafungulia neuclear weapons.

Jee huu ni mkwara wa Urusi ama ndiyo tujiandae ?

Mr Lavrov claimed the West was "pouring oil on the fire" by providing Ukraine with firepower and repeated warnings that the conflict could lead to a third world war.
 
Niliamua kukaa kando na huu Uzi lakini kuna propaganda imeenezwa ambayo siwezi vumilia, hakuna ushahidi wowote kuhusu Putin, aliezaliwa 1952, kuzuru bara Africa miaka ya 1970s.


Rekodi za Putin katika mtandao wa Kremlin zinaonyesha wakati huo alikua akisoma katika chuo kikuu cha Leningrad mpaka 1975 alipomaliza.

Alafu pia mafunzo ya kijeshi yaliotolewa tanzania kwa wa Mozambique yalipeanwa kwa asilimia kubwa na wachina sio wasovieti.

Na Mnangagwa hangeweza kua Tanzania 1973 kwa sababu alishikwa 1965 na kufungwa kwa miaka 10 na Wakoloni.
 
He added that the suspension proved Moscow was "not a reliable partner in any kind of business"
Ex KGB ameuwa business goodwill na EU and civilized world , vladimir ajiandae kuuzia washirika wake hasa mchina ,nishati kwa bei kwa bei ya kutupa kuuanzia 2023. Let freedom ring.
 
Ngoja tukumiminie facts
 
Putin is very bright...
 
Hiyo kujitoa ni hadithi
Kuna mjuaji mmoja humu Pro Putin alikuwa anatulisha tango pori kuwa France wamechoshwa na sera za NATO na akasisitiza kabisa yule Mpinzani wa Macron atashinda kwakuwa anasera zinazoendana na Putin.Sasa hivi yupo hapa anaruka ruka na macomment marefu hakumbuki tena hizi porojo zake [emoji23][emoji23]
 
Vifaru haviendi kama Russia walivyotaka tuamini ndio maana kuna mtazamo wa kusema vifaru vimepoteza maana. Infantry support, air cover, scout na tactics walikuwa poor. Mvamizi wa modern army akikuletea vifaru anatanguliza air cover kwahiyo ndoto za kumpiga kutokea angani unapunguza, anaongeza patrol kabla havijafika kuna dedicated vehicles zinasoma all radio waves, radar emitters, GPS devices na kutambua uwepo wa mtu almost ndani ya 5km na kupeleka taarifa hizo kwa tactical brigade commander ambaye anaamua wafanye neutralisation kabla ya kuleta armoured column.

After that wanaleta mine clearing vehicles zinatangulia mbele na kufanya clearance ya landmines ardhini na kuacha njia ambayo vifaru vitapita na infantry support. With that, chances za kusema vifaru ndani ya jeshi havina umuhimu ni ndogo. Hapo hatujagusia tank design ya Russia ambayo ni mbovu sana inafanya viwe na cookoff.

Hiyo ni scenario ila inategemea kuwa contested kwenye air dominance, artillery precision, guidance & range, communication, command & control, etc. Sasa Urusi alikuja kama anapiga Boko Haram na vile ashawaita neo-Nazis kawadogosha.

Vita ya mjini huwa ngumu zaidi kuliko ya porini ndio maana Russia watajishikiza na gains za Eastern, huku Kyiv bado hakuendeki kwa sasa. Russia on paper ana silaha nzuri ila number matters. Bado training ni muhimu mno, na nchi isiyo na audit kali kwenye jeshi haiaminiki hela zinazotengwa hufanya kinachostahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…