Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Putin au Zelensky mmoja wao akifika November yuko madarakani kwa kweli dunia itakuwa haitendi haki.Naona Putin mpaka Nov mwaka huu out. Mimi naangalia kwa mapana lazima wamwondoe maana analeta simtofahamu duniani na anachotaka akieleweki
Baada ya tishio la Vladimir kuungamiza dunia kwa nuklia, kamati kuu ya sangoma wa Afrika ilikaa kikao cha dharura na hatimaye kutoa tamko hili nyeti- Valdimir will no longer be a threat to society by Jan 2023. Yetu macho.
 
Hasara ifuatayo; Kwa Urusi

Tanks - 1,000

Aircraft - 200

armored vehicles - 2,500+

Troops - 20,000+


Unateka eneo kubwa la nchi kwa kutumia askari ambao wengi wanaishia kuuawa wao na makamanda wao. Unajikuta maeneo yote yanarudi mikononi mwa wenye nchi yao na wewe unalazimika kuendelea kushikilia maeneo ya mpakani ambayo ndiyo yalikuwa ya kwanza kutekwa, tena unarudi kwa kupigana upya ukibomoa kila kitu kwenye mji huo.

Hapo unavyoona kuna Jeshi la kuteka chochote hapo? Hata kama Russia angekuwa na uwezo wa kuteka, kamwe asingejisumbua kuteka silaha ambazo amezitengeneza mwenyewe. Mara nyingi unapoteka silaha huko vitani hasa kwa nchi kubwa, lengo huwa ni kwenda kujifunza na kuiba technology iliyotumika kuutengeneza mfumo huo.

Sasa yeye silaha alizokuwa akipambana nazo zote ni za kwake, hivyo ukiniambia aliziiripua nitakuekewa lakini si kuziteka.

Ukraine wameangamiza silaha na mifumo mingi ya Russia, lakini za aina mbili tu, hizo waliamua kuzikamata na kuzikabidhi kwa US, sababu technology iliyotumika kutengeneza mifumo ile ni mpya kabisa.

Jata ukiangalia Geigraohia ya eneo la kivita, unajiuliza hizo silaha akiziteka vipi ikiwa askari tu na makamanda wao walishindwa kutoka hai


Namna nzuri ya kujiuliza iki kukubaliana au kuzikataa figure zilizotumika, nilitumia Logic hii;
Wakati Russia anaivamia Ukraine, alipeleka akari 150,000, akiwa na lengo la kuikamata Ukraine yote na kumkamata na kumuua Zelensky.

Wakati vita inaelekea mwezi wa pili, tukaona Ukraine wanaanza kukamata upya maeneo yaliyokuwa yametekwa.

Russia akazamishiwa hadi Meli vita yake.

Russia akaenda kujikita Mariupol na Donbas huku akiongeza asksri wengine 150,000.

Askari wengi wakawekwa in Standby mpakani upande wa Russia huku akianza kutuma makombora kutokea mbali akibomoa majengo na miundo mbinu katika miji hiyo na anapihakikisha amesha bomoabomoa ndiyo anasogeza askari wake.

Hili la maeneo waliyoyateka kukamatwa tena na Ukranians, huku akiingeza askari wengine kwa 100%+ na kuanza kupiga mashuti ya mbali huku na yeye akianza kupigwa makimbira kwenye ardhi yake, ndiyo Logic ninayoitumia katika kuzikubali au kuzikataa takwimu.

Kuna taarifa nyingi wakikanusha kwamba lengo siyo wala haikuwa kumuia Zelensky hii ni baada ya kufeli

Kumuua Zelensky ni kati ya mikakati ya Putin, ingawa katika hili alikua misled.

FSB wamefanya kazi kubwa sana ya kuua wale waliokua wanaenda kutekeleza hili, ambao hawakuwa ndani ya Heshi la Russia baki ni lile kundi la Wagner (Wagner Group). Wagner waliripotiwa kuingia Ukraine na ndiyo walikuwa na kazi hii ya kumuya Zelensky, lakini story zao ziliishia kwenye kuingia Ukraine, hawakusikika tena.

FSB wakishirikiana na naadhi ya washirika waliomo msshirika ya kijsdudi ya nchi nyingine waliwasaka Wagner popote walipo na kuhakikisha wanawaangamiza kabla ya kumdhuru Zelensky?

Kwanini FSB waliwafyeka Wagner wakati walikuwa wakipigana upande wao?

Wagner ni kikundi cha kijeshi kilichomo ndani ya Jeshi la Rusdia, kikundi hiki kina wanajeshi kutoka mstaifa mbakimbali rafiki wa Russia kama vile Yemen, Russia, Iran, Syria n.k. Kikundi hiki hujulikana kama jeshi binafsi la rais Putin ambalo ameliweka ndani ya Jeshi la Russia iki kupata mafunzo ya kijeshi na kwa ajili ya mission mbalimbali, ingawa kwenye mission huwa hakiwi chini ya amri na uongozibwa jeshi la Russia bali kutoka kwenye circles za Putin na Putin mwenyewe.

FSB walilazimika kuwafyeka sababu kitendo cha Wagner kumuua Zelensky kilimaanisha ni hukumu ya kifo kwa rais wao pia. Kwani kama wangefanikiwa, sasa hivi ingekuwa ni Russian president anatafutwa auawe, siyo kukamatwa ili ashitakiwe, bali auawe. Hiyo ndiyo sababu iliwapelekea FSB kupambana kuwamaliza Wagner na ililazimika kwa maeneo yale hawafiki watoe taarifa kwa wenzao wa CIA, Bundesnachrichtendienst (Federal Intelligence Service - German), Foreign Intelligence Service of Ukraine (FISU), MOSSAD, MI6, Canadian Security Intelligence Service et cetera.

Thanx Thaddeus

Britanicca
Ulaya nzima sijaona mji wenye usafiri wa haraka kama Moscow, kama mtu anabisha aje na data zake.
Usafiri wa underground train, huwezi kukaa station zaid ya dakika 5 hujapata usafiri wa unapotaka kwenda, na gharama zake ni cheap kuliko nchi yoyote ulaya, wakati mji wa London train moja hadi jingine kutokea huchukua takriban dakika 15 hadi 30 na huo mji wa London ndio unaaminika uko busy kuliko miji mingine ulaya.
 
.
Screenshot_20220504-141516.jpg
Screenshot_20220504-081315.jpg
 
Putin yupi aliyegundua na Putin yupi anayetaka kumalizwa? Uwezo wako mwisho ni kujua yanayoendelea Tanzania lakini ya huko Kremlin ni makubwa kwako. Yaani unamzungumzia Putin kama Unamzunguzia Mnangagwa. Ulianza na majasusi wa Marekani wapo Moscow haikutosha Ukasema afya ya Putin sio ridhiki leo unasema KGB wanapanga kummaliza...bado kusikia juu ya mpango wa mkewe na wanawe.

Cha kukusudia tu tunza nguvu yako mpaka 09 May mwaka huu maana inasemekana Russia itatangaza vita kamili kwa Ukraine. Hapo ndio utakapoona nguvu kamili ya Urusi
Wewe jamaa ni mswahili haswa, una mambo ya kiswahili sana yale yale ya Mohammed Al Sahaf wa Iraq. 🤣 🤣
 
Hii article nimeisoma Leo asubuhi Twitter nimeshangaa namna Putin anavyopata upinzani kutoka ndani ya serikali yake hasa usalama WA taifa.
Niwaambie Tu watu wasiojua Mambo ya kimataifa kuwa wakati huu westerners wameungana Sana kupeleleza Russia anafanyaje pia zinatumika kila mbinu ili kidhoofisha nguvu zake kwasababu muda huu ambao Russia yupo vitani ndiyo muda muafaka WA kuibomoa nchi.

kuna watu wanasema may 9 atatangaza vita kamili bila kujua kuwa waliopo field hawana molari ya kupigana..

alafu ukiona raisi anaanza kugombana na watu wake hapo usitegemee ushindi zaidi ya sabotage tu

"kuna watu wanasema may 9 atatangaza vita kamili bila kujua kuwa waliopo field hawana molari ya kupigana.."

Hakika Tz iliwahi kua no. 1 kwa upelelezi Duniani.
 
Putin ana tatizo la Dementia maanake siyo mzima, pia ana ugonjwa wa satatani(cancer) ya tumbo, tatu ni ‘LUNATIC’ yaani kila mwezi uandamanapo anakuwa na ukichaa wa aina yake! Just imagine, kiongozi wa super power anawezaje kuvamia nchi huru popote pale dunia na kufanya ni sehemu ya nchi yake?!
Bangi Ni mbaya Sana aisee.
JamiiForums-1142540770.jpg
 
Hao NATO wanaogopa nini kwenda mtoa?? Dada unafikiri Russia ni Libya?? Usione NATO wanaufyata kwa Russia wanajua mziki wake, Putin sio gadaffi.
Sio.Libya ila watamtafutia dawa tu.Hiller alisumbua na wali manage.The good things about human being, ukiwa peke yako au peke yenu mnaleta shida solution inatafutwa tu kama wanataka hiyo ndio p
maisha ya duniani
 
Rumours are swirling in Moscow that former generals / KGB officials are preparing to oust Russia’s president Vladimir Putin to end the war in Ukraine, which is increasingly seen across Russia as a strategic mistake / an economic disaster.
Nimesikia the same ,shida sisi tunafikiria dunia imelala sana watu wanatafuta long term solution sisi tunashabikia mabomu na mafuta kupanda hukuntukisema Magufuli ,sijui samiank .Solution ni hii vita kuisha maisha yaendelee na sio kusema sijui Putin mwanaume nk Kama mwanaume aonyeshe mke wake kwanza kwa sababu yeue mwenyewe ameshidwa ku manage familia ndio vita ?Mjinga kabisa
 
Aya tuambie wewe kias gani anacho?? Na nipe source ya kuwa Russia ameomba kuondolewa vikwazo
Ukraine war: Lifting sanctions against Russia is part of peace talks, says Sergei Lavrov.

‘We are in favour of continuing the negotiations, although they are difficult,’ Russia’s Foreign Minister claims."
 
Tatizo lako wewe unataka kusikia habari nzuri za Urusi tu. Unataka kusikia habari za kuwa Urusi anaipiga Ukraine kweli kweli au Urusi ana silaha bora kiasi kwamba silaha za Ukraine hazifui dafu. Unataka kusikia wanajeshi wa Ukraine 20000 wamekufa ila wanajeshi 25000 wa Urusi wamekufa hutaki kabisa kusikia. Na huo wala siyo mtazamo mzuri.
wenzenu wanaleta na source , nikiuliza source ya habari hi iko wapi unaweza kuniambia?
 
Putin haungwi mkono na nchi yake , nimeshangaa sana Putin kushindwa kulijua hili mapema
Its so wonderful that Putin who is also a legendile with great expertise in covert, clandestine and intelligence do not know whats is prevailing in Russia but you an ordinary person from Bonyokwa knows! This should placed to the world wonders.
 
Putin ana tatizo la Dementia maanake siyo mzima, pia ana ugonjwa wa satatani(cancer) ya tumbo, tatu ni ‘LUNATIC’ yaani kila mwezi uandamanapo anakuwa na ukichaa wa aina yake! Just imagine, kiongozi wa super power anawezaje kuvamia nchi huru popote pale dunia na kufanya ni sehemu ya nchi yake?!
kwanini kavamia Ukraine na sio kwingine?
 
Back
Top Bottom