Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hii hoja ukiisoma kwa haraka ni kama ina nguvu.

Swali ni baada ya USSR kusambaratika madeni na amana zake zilibebwa na nani?

Ni sawa unaponunua kampuni unanunua mali na madeni pia!
Amana zipi mzee. Hapa tunaongelea issue ya Security. Ni NATO pamoja na Russia.

Nakusihi utafute hii uisome

Founding Act
on Mutual Relations, Cooperation and Security between NATO and the Russian Federation signed in Paris, France
27 May. 1997
 
Agreement ya 1990 ilikuwa btn Russia and NATO ilikwamba USSR iweze kuvunjika. Ndio maana baada ya makubakiano hayo USSR ikavunjika. Soma vitu. Nitakuletea documents
USSR ilivunjika yenyewe kwa kushindwa kujisustain, siyo kwamba ilijivunja kutokana na makubaliano ya NATO. Wakati wa makubaliano hayo Waziri wa mambo ya nje alikuwa Eduardo Shervadnaze akitokea Georgia, Waziri Mkuu alikuwa Nikolai Ivanovich Ryzhkov akitokea Ukraine; hawakuingia makubaliano hayo kwa ajili ya Russia wakati wao siyo raia wa Russia bali waliingia makubaliano kwa niaba ya USSR.

Mimi pia nina records za maongezi kati ya Rais Clinton na Rais Yelstin baada ya USSR kuwa imevunjika yanayoonyesha kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote ya namna hiyo baada ya USSR kuvunjika. Yelstin alijiweka karibu sana na Clinton wakati uchumi wa RUssia ukiwa in shambles akiomba USA isaidie kuinua uchumi wa Russia. Kuna records nyingi sana zinazoonyesha yaliyojiri kati ya URUSI na USA kuanzia mwaka 1991 hadi 2002 muda mfupi kabla ya 9/11.
 
We jamaa unawalisha wafuasi matangopori. Transnitria Ni moldovan occupied region ya Russia tokA 1992.
Maisha ya leo wafuasi wako washasahau hata wao wakidanganya wapo Kaliningrad tokA 1990 wakati wa anguko la Usoviet Kuna watu humu watakubali.
Tofauti na zamani Leo nikiamua kutafuta kwa Google mitaa ya Moscow naweza kutunga stories nzuri Sana jijini humo watu wakanielewa na watanisifu Kama ambavyo wanakusifu we'we Kwamba Ni mjuvi was kila Jambo ikiwemo ya ndani kabisa ya FSB, CIA na ikulu ya Korea N.
So Britanicca we Ni muongo mkuu wa humu ndani
 
Hapa ndo unakuja kujua Russia ilivyo na vichwa smart, yani wazungu wameshikwa pabaya mno na Russia kuliko walivyoishika wao.

Hapo anasubiri tu watikise makalio wazipige mnada reserves zake nayeye azipige mnada reserves zao.

EU bila USA anaiogopa mno Urusi na USA bila NATO anaigopa mno Urusi.

Urusi imekuja kutufunulia mambo mengi sana sisi wamakonde wa nchi za dunia ya tatu hadi leo tumejua kuwa zaidi ya 60% ya uchumi wa nchi za EU upo mikononi mwa Mrusi.

Hakika Urusi siyo Zimbabwe.
mrusi sio fala aisee Putin ni kichwa sana
 
Hii hoja ukiisoma kwa haraka ni kama ina nguvu.

Swali ni baada ya USSR kusambaratika madeni na amana zake zilibebwa na nani?

Ni sawa unaponunua kampuni unanunua mali na madeni pia!
Baada ya USSR kuvunjika, kila state ikachukua madeni na mali zilizokuwa kwenye ardhi yake. Kwa hiyo Tajikistan ikachukua deck za kurusha maroketi ya anga za juu pamoja na madeni yote yaliyotakana na madeck hayo, na hadi leo Urusi wanailipa Tajikistani wanapotaka kurusha maroketi yao, na Ukraine ikachukua mitambo yote ya Nyuklia, viwanda vyote vya kijeshi pamoja vilivyokuwa katika ardhi ile pamoja na madeni yote yaliyotakana na mambo hayo. Clinton alifanya juhudi sana za kuiaminisiha Ukraine iharibu makombora ya Nyuklia iliyokuwa imerithi na kufikia yale makubaliano ya Budapest Memorandum ambapo pamoja na mambo mengine yalikuwa yanaitaka Urusi kulinda usalama wa Ukraine, na Ukraine ikaikbaidhi Urusi makombora yale ya Nyuklia, lakini huyu Putin kakiuka makubaliano hayo, ila analilia makubaliano ya USSR ambayo yalishapitwa na wakati.
 
The Agreement between NATO and USSR does not apply today since USSR is extinct. At that time USSR included countries like Latvia and Lithuania who are members of NATO today. Do not justify evil actions by using wrong information.
Duh...Kichuguu nawe bwana acha hizo aisee...You should go back to history and geo-politics studies...You are talking of evil actions?? What about evil intentions and agenda? Who are the enemies of NATO?
 
Inasemekana kutokana na matatizo hayo ya kiafya, shoigu alimuintroduce kwa mganga wa kienyeji ambaye huwa anamtibu kwa kumuosha kwa damu ya mnyama anaitwa "antler", japo tiba hii inasemekana kukubalika sana huko rusia.

mahusiano ya huyu shoigu na putin yawezekana (kwa mtazamo wangu) yakawa yanakaribia kufanana na yale ya bashite na mwendazake, huyu shoigu anaakili za kienyeji sana, vifalu vya urusi vilivyoshindwa kuiteka kiev inasemekana vilikuwa vimezungushiwa ma -mbao kama kinga dhidi ya mizinga, yaani style fulani hivi kama ya majimaji war. matokeo yake wote tunayajua.
😂😂😂😂we jamaa noma sana
 
Kama Russia kwa muda huu wa uvamizi wao hadi sasa wamepoteza majenerali 9 na makanali 36 ambao ni viongozi wa ngazi za juu namna hiyo basi wanajeshi wa kawaida waliowapoteza watakuwa ni wengi sana.

Kwa muda mfupi wamepoteza maaskari wengi zaidi ya waliopoteza Afghanistan, Chechnya, Georgia na Syria. Ni pigo kubwa sana kwa kweli.
Hizo ni takwimu za propaganda kwa mujibu wa Zelensyk. Tunataka ukweli na siyo propaganda.
 
Back
Top Bottom