[emoji23][emoji23] Hatari...
Hapana Jamaa angu, na hatutegemei hata siku moja kuona "mtu mwenye jeuri" akikubali kushindwa. There's no way to defeat Russia in Ukraine, nao wanalijua hilo fika Lakin hawawezi kukubali kushindwa kamwe.
Jarib kuwatizama EU, Ona namna wanavotaka kufanya economical suicide kumkomoa Russia kisa Ukraine... Unaamini kweli ni kwasababu ya Ukraine ndio watake kwenda that far?
Duniani kote huwa tunaamini hakuna adui wala rafiki isipokuwa kwenye maslahi, na hii ndio hulka ya mwanadam. Sasa mie na wewe tuulizane kwanini wanataka kwenda this far katika mapigano yao na Russia?
Nchi za EU zinaongoza kwa Tax, na yote hii ni kwasabab nchi hizi hazina rasilimali za asili hivo pato kubwa la serikali linatoka kwa Raia wao. Mfano Denmark, France na Austria inaenda zaidi ya 50%... Na ni nchi tu kama Hungary, Czech na Estonia zenye lowest tax rate. Sizani kama na haja ya kukuelezea kodi ni nini.
Sasa angalia ukubwa wa hizo kodi kisha fikiria mfumuko wa bei za bidhaa unavowakamua Raia wa kawaida. Zote hizo ni outcomes za matendo ya viongozi wao kisha wanaisingizia Russia...
Katika kulielewa hilo chukulia mfano wa hapo TZ... bei za vitu zilivyopanda. Ongeza tozo za kila sampuli kisha piga hesab kwenye mshahara ule ule ambao haujaongezeka hata thumuni, 10k ya jana sio 10k ya leo.
Sasa huo Ugumu unaoufikiria ndio Ugumu unaowakumba Raia wa EU na Western kwa ujumla... na ni vitu ambavyo media inaficha haizungumzi. Na hawazungumzi kwasabab media zote kubwa zinafanya kazi za hawa walioko nyuma ya hizi "morons" tunaowaita viongozi.
Ni Raia hao wa nchi hizo wanayatamka pembeni, wanaugulia ila hawana jinsi. Viongozi wao hawapo kwa ajili yao wapo kwa ajili ya Master wao wanaemtumikia. So kushindwa ama kushinda kwao hawajali... What matters kwao ni kutengenza Crisis then through that Crisis wajanja wanatengeneza Pesa.
Kuna maandamano kila kukicha ila hayapewi headlines, hizi kauli za "Media are lying" hatuzitoi tandale... tunazitoa kwa Raia wa nchi hizo. Majuzi kati Huyo Papa wa Katoliki alinukuliwa akisema kua Harakati za NATO kwenye mipaka ya Russia ndio zimepelekea mzozo huo uliopo hivi sasa.
Hio taarifa haikupewa kipaumbele kabisa kwasabab haiwafurahishi wakubwa.
Kwa kifupi tu issue ya wao western kukiri kushindwa sizani kama kutatokea, wako ready ku'fight Russia to the last man Standing. Na wakishindwa Ukraine, watazua sehem nyingine na nyingine...
Na nirekebishe kauli vizuri... tatizo sio US bali hicho kikundi kilichopo nyuma ya serikali ya US ndio tatizo ulimwenguni. Binafs sio mdau sana wa hizi State Affiliated Media. Obviously ukijikita kwazo unakuwa much disinformed.
Ukitaka kuyaona ama kufaham mengi ya nje basi tengeneza Connection na watu wa kawaida tu kwenye maeneo unayotaka kujua habari zake ama fatilia yanayojiri ulimwengunki kwa waandishi wa habari wana harakati.