Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

🤣🤣🤣 Lazima ulazwe mwaka huu
 
Rejea comment yako ya mwanzo uliyo ni quote.
Wewe kifupi weka orodha ya vita ambazo USA alishinda yeye kama yeye.

Hapa ni discussion ukiulizwa swali lijibu.
Tunataka kuonesha with evidences Russia vs USA
Huenda kuna mtu ameku quote ukachanganya na mm au huenda nimeku quote ukanielewa tofauti. Siwezi kubishana kati ya USA na Urusi nani mbabe ila ninapinga Urusi kuivamia Ukraine.

Hapa kinanchonifanya niingie humu ni mada hii,

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo.​


Kama unataka tubishane kwa hoja basi wewe simama katika kutetea uvamizi wa Ukraine na mm nisimame katika kupinga uvamizi wa Ukraine lakini sio tubishane nani mbabe kati ya USA na Russia.
 
Sio wewe tu unayejiuliza hilo swali bali wachambuzi wengi wanajiuliza juu ya ufanisi wa jeshi la anga la Urusi kwenye hii vita
Siku hizi harushi ndege maana zinadondoshwa...
Urusi alitudanganya kaharibu ndege zote za Ukraine, nashangaa snake Island imelipuliwa na ndege za Ukraine
 
Majeshi ya Ukraine hayana tactics ...wenzao wanarudi nyuma kimtindo Sasa ili wawazingire Sasa hao ukraine wanakimbiza utadhani wanakimbiza swala wasijue kuwa it is a trap😂😂😁😁interesting indeed
 
Habari za picha.Ukraine wana wasaidizi wazuri wa propaganda.Kama batallion nzima inaangamizika kihivyo kusingekuwa na vita tena.
Hamjazuiwa kusambaza propaganda
 
Warussi wa tandahimba mimba zinataka kuwatoka maana sio kwa kipigo mnacho pewa
 
Over confidence
Platoon inakaa for days bila surveillance.
Halafu why msafara kama mwenge tena porini.
Si over confidence hawa watu hawana morali kabisa, wanaona hakuna faida wanakufa tu.

Na hapo ukute wamepewa false intel ndo maana wakavuka.... Na zoezi zima limefanyika kwa siku 3 kuanzia kujenga daraja na kuanza vuka, waliovuka ndo walikuwa wanawalinda ambao hawajavuka, wakaanziwa wao na daraja afu wakapigwa ambao hawajavuka
 
Kwa kweli wew umesema vema ukisema kuhusu ukraine au urusi watu.wanachanganya na USA .
 
Reactions: Tsh
Basi hakujiandaa na vita, hii vita ikiisha tutaujua ukweli mwingi kuhusu Ukraine na Urusi.

Naona Ukraine yeye anapambana haswa hizi M777 za US zinafanya maajabu sana

Nimeona Israel imeruhusu Estonia ampe Ukraine Anti Ship Missile ambazo wanasema zina range ya 290KM na zinaweza tumika tokea kwenye meli, ndege hata mounts za magari, Estonia kampa 500, Israel atarefill

Hapo maana yake meli za Urusi zitaumia mno

Ukraine wameomba MRLS kutoka G7 countries,hapo wote wanasubiri nani atarefill ili wamtumie Ukraine hizo MRLS,akipewa hizo maana yake Crimea bridge halipo tena
 
Kwa kweli wew umesema vema ukisema kuhusu ukraine au urusi watu.wanachanganya na USA .
Na si hilo tu, sijajua kwann😃 kuna mambo huwa yanaibuliwa nje ya uvamizi na kuwa agenda kuu.
 
Nilikuuliza swali una lijua bomb linaitwa
Father of All Bombs!? Nikaona unachanja mbuga. Tunapoonglea Russia unatakiwa uielewe hiyo nchi.

Ipo miaka mingi kabla hata ya USA kuwepo. Na kumekuwa na migogoro kati yake na majirani miaka na miaka. Na urusi wamekuwa wakipambana karne na karne. Je unaijua sababu ya migogoro hiyo!?

Migogoro hiyo inatokana na hazina kubwa iliyomo ndani ya ardhi ya Urusi. Mataifa ya ulaya yamekuwa yakidondosha udenda kuweza kumilk ardhi ya Urusi. Taifa lolote likiweza kuidhibiti urusi litakuwa tajiri na kiranja wa dunia.

Hawa warusi wamekuwa wakipigana vita miaka na miaka.
1. Wamepigana na Mongols
2. Wamepigana na Persian empire
3. Wamepigana na Napoleon (France empire)
4. Amewahi kuwa gonga mjumuiko wa England, France na takata.
5. Amewahi kuwagonga Ottoman Empire.
6. Amewahi muwagonga wajapani.
7. Amewahi kuwagonga Astro-Hungary empire.
8. Alingonga Hitler second wolrd war.

Orodha ni ndefu mno. Hao warusi wanacholigania ni maslahi ya nchi yao tu. Ukikaa nao vizuri hawana shida na mtu.

Poland anawajua warusi, Finland anawajua warusi, Sweden anawajua warusi.

Hizi nyege wanazozionesha nakuhakikishia zitawatokea puani.
Fanya yote lakini usimchokoze mrusi.
 
Putin si mjinga kutoa silaha zote kwa ajili ya Ukraine wakati ana maadui wengi.na ndio maana hataki tangaza vita kamili maana akitangaza vita kamili itabidi apeleke vifaa haswa kwani Ukraine ataweza saidiwa ground na nchi yoyote ile

Kingine Urusi hana marafiki, China,Cuba, Vene, NKorea,Iran wamekaa kimya kama hawaoni
 
AWACS, Global Hawks za Marekani Poisedon zipo angani zinakusanya data na wanawapa Ukraine, Ukraine kujiridhisha wanatuma Baykatar kisha wanatuletea video za maangamizi
 
Na si hilo tu, sijajua kwann😃 kuna mambo huwa yanaibuliwa nje ya uvamizi na kuwa agenda kuu.
Hakua uvamizi mzee. Ingekuwa ni uvamizi ungeona hao Ukraine wanatupa mizinga na kurusha ndege za makobora ndani ya urusi. NATO na Ukraine wanajua kabisa WHO IS RUSIA.
Russia is the father of this World. Russia angekuwa na kihere here kama mmarekani nakuhakikishia dunia hii ingekuwa tofauti kabisa.

Russia yupo kimya anajaribu kuwaeleza kwa upole kabisa, kwamba achaneni na mpango wenu wa viwanda vya kibiolojia karibu na nchi yangu. Fanyieni hata popote lakini msisogee kwangu. Hawaelewi. Anawatahadharisha NATO kwamba acheni kuongeza eneo lenu upande wa mashariki. Hawasikii.

Mkianza kula kichapo msianze kulia lia tena. Father is in the House anafundisha adabu watoto.

Nakuhakikishia kihere here kinvyozidi kupamba moto utamsikia Poland na Moldova wanakula kibano. Msilie maana Urusi huwa anatoa angalizo kabla ya kuanzisha kichapo.

Bado anawaonya hawa Finland na Sweden. Kuna kipondo kitamwangukia mtu. Wewe subiri tu.

Na unatakiwa uache kulia. Maana zege mlilikoroga wenye, huwa halilali.

Nakusihi tu uendelee kunywa mtori nyama zipo chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…