Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Mdogo wako huyo [emoji23] akifanikiwa kujibu hilo swali la 4 inavyotakiwa bila kupindisha aweke number nimtumie na ya kutolea [emoji847]
 
Utoto.
Kama unakiri kwamba kulikuwa na dola kadhaa zilizotawala na kuanguka,vipi usiamini kwamba huyo USA naye ataanguka!?

Na kwanini asiwe mrusi ndio atakayemuangusha.

Kumfananisha mrusi na Germany au Uingereza ni kumkosea heshima. Kwani hao wote wamegeuka makoloni ya America ili tu awalinde na mrusi

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Umemsahau Yuri Gagarin na Outer space technology.
 
HAWAELEWEKI YANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkulungwa nimekupa ushauri wa bure kama elder jikite kuokota habari na kupachika humu, mambo ya International relations wewe ni layman.
 
Kwanza nashukuru kwa ustaharabu uliouonyesha katika maandishi yako. Pia sipendi nikukwanze kwa hizo typing error zinazotokea kwenye maandishi yangu. Nisamehe kwani natumia hizi simu janja.

Nashukuru kwa kukubaliana nami kuwa tujadiliane kwa kuangalia yale maeneo matatu.

Kwa sasa nipo njiani nitapita maeneo flani kwa ajili ya manunuzi kido kisha back to my home place, hivyo nitakuwa na muda mzuri wa kuandika with supporting documents/evidence.

Mwisho kutokana na umbri wako mkubwa naomba nikusalimie kwa mfumo tuliourithi toka kwa mkoloni, SHIKAMOO ...

Nikutakie mjadala mwema na nakuhaidi nitarudi baadae ili tuendelee kuelimishana
 
Karibu sana. Hapa tunapojadiliana wengi wanapata elimu.
 
Usilazimishe mambo,
Narudia ili huo umaandazi unaosema uupigie mstari, linaloendelea ni kuwa Tsh msimamo wake ni huu:

SINA USHABIKI NA USA, SINA USHABIKI NA URUSI. NALAANI AU KUSAPOTI TENDO LINALOFANYWA NA HIZO NCHI MBILI.

Kuna yule mkenya anatetea NATO, aliitetea kwa kuiponda Tz na nikaungana na wapenzi wa Urusi kumshambulia. Kama hukunielewa pale endelea kuchoka.
 
russia mwenyewe amekung'utwa (kashindwa vita) na Duchy of poland, sweden Lituania, France, Turky, Britain, Japan, Latvia, Estonia, Georgia, Ukraine, na unaona kabisa kuna nchi nimezilist hapo baada ya kushindwa vita hizo nchi zikawa huru, aliisaidia ethiopia kivita ili eritrea isijitenge akapigwa eritrea ikajitenga, na serikali ya kikomunist ya ethipoia ikaanguka, Afghanistan palimshinda (na ni sababu mojawapo iliyopelekea ussr kuvunjika na kwenye vita hii afghanistan alisadiwa na USA) Chechen urusi kala kichapo, russia ni nchi ambayo ni matokea ya kuvunjika kwa soviet union na USA alikuwa nyuma ya kuvunjika huko.

Russia ni muumin wa ujamaa ambao ulishamshinda na imebidi tu afuate ubepari na ndipo maliogarch walipogawana keki ya taifa na watu akina Abhamovich kuibuka-wizi wa mali za taifa huo. Warusi wanapiga hela za michongo kwao na kuwekeza western.

Huo ujamaa wa russia hakuna popote ulipoonyesha kufanikiwa na ndiyo maana hata Tz ipo hapa ilipo. China ilibadili gia angani baada ya kuona ujamaa haulipi na ndiyo maana china trading partner wake mkubwa ni US. Russia kiuchumi (GDP) hata top ten haipo inashindwa na nchi kama india, brazil.
 
Kwanza ndugu nakushauri ujifunze matumizi ya paragraph. Upo na mawazo mazuri lakini yanakosa mtiririko kwasababu huna elimu ya mwandiko.

Urusi ilikuwepo kabla ya USSR. Najaribu kutafuta namna ya kukujibu lakini naona uwezo wako ni mdogo mno wa kubeba mambo.

USHAURI:-
Jaribu kukuza kwanza uwezo wa kufikri kwa kula dagaa, mifupa ya samaki, asali na maziwa. Ukifanya hivyo kwa mwaka mmoja utapa improvement.

Asante.
 
Izo laana au sifa zako zinafaida ganii kwenye hii dunia ya wababe
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒAm done.
 
Unashabikia Urusi sababu umechoka na vitisho vya USA kwa nchi yako na Africa na una mambo mengine mengi unayoyataja. Sawa. Tuanze na vitisho.....

Unaamini Ukraine atakaposhindwa utakua umefanikiwa kwa kiwango gani kukwamisha huo ubabe? Tuanze na hili la unabe kisha tutaamia kwenye mengine meengi unayoyazungumza.

Halafu, Hakuna imotion wala sypmth inayoletwa hapa, Unachukua mambo meeeeengi ya duniani na kuyaweka kwenye jambo moja la Ukraine na Urusi na kufanya kujadiliana na wewe iwe ngumu sababu unakuja na tendo na kulipachika kwenye nchi nzima na matendo yake yote hata yale ambayo sina tatizo nayo.

Huo mchanganyo ndo ninaoukwepa kwa muda sasa ila hunielewi. Sasa twende, naomba unipe jibu la swali nililokuuliza ili nikulete nipotaka usimame. Nataka nikufanye uzungumze hoja moja baada ya jingine. Kisha utakuta kuna mambo nayasapoti kutoka kwako na kuna mambo nitayapinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…