Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ushakunywa uji unakuja kujamba uku hivi vikwazo ni kama msumeno inakata mbele na nyuma waulize west wanavyo jamba jamba kila siku vikao alafu urusi wala husikii akilia waliisi urusi ataumia kuliko wao Ila imekuwa tofautii uswis kashatoa vikwazo vya pesa alivyoweka Kwa makampuni na warusi saivi urusi inangojea mwezi wa 11 Tu kelele zote izi zitaisha

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Hawawezi kulia Lia maana wanaongozwa na Nduli mmoja Putin tu , wanaugulia kwa ndani mkuu
 
Watu wengi hawaangalii hivi vikwazo vya uchumi alivyowekewa Putin , wanaangalia tuu amerusha makombora wapi . Asilimia kubwa ya matajiri wa Russia wamepata hasara kubwa sana .

Hela nyingi zilizoshikwa nje ndio zinanunua silaha zinarudi Ukraine. Nadhani maisha ya Putin na washirika wake wanajuta kuivamia Ukraine .

Putin anapiga vita viwili vikuu . Uchumi na vita vya makombora.
Yaan mtu anaamka tu na kula viporo vya mihogo huko matumbi...anakuja kuanzisha mada kama hizi jaman!! Ebu kamalizie viporo vyako huko kisha uende kuangua nazi..hizi mambo ya kimataifa sio level yako ww mmatumbi!
 
Ukiona uzi hauja haujapandishwa kwenye hapa

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo​

Ujue hizo ni takataka kama huu
Tulia wewe mmalekani wa butimba!!
ma terrorist ya azov steel plant,hatimaye yamejisalimisha Sasa haya ni kuyanyonga kwa kuwa yaliteka raia na kuwaficha ndani ya kiwanda Kama ngao Yao !!
 
#Caption Challenge to Pro Russia,

Wadau karibuni tufurahi, tushindane kutoa Caption ya hizi picha mbili, kesho tutangaza mshindi kutokana na wingi wa reactions kwenye Caption yake...🤗
Putin: Dogo, hivi unajua nikitoka madarakani nafikiria kukupasia kijiti wewe?
Medvedev: Ahahaaaah, ebu acha utani wewe mzee!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Marekani ikaanza kujiimarisha na kujiimarisha katika muungano wao wa NATO, hii NATO ni muungano wa mataifa ya kibepari kujihami dhidi ya mataifa ya kijamaa, hivyo Marekani na NATO wakaanza kujiandaa ili kuidhibiti Urusi, maana walijua wakidhibiti Urusi watakuwa wameidhibiti Cuba, baada ya Urusi nao kujua hilo nao wakanza kujizatiti ili kuidhibiti Marekani, ndio Urusi wakaunda umoja wao wa Warsaw Pact.

Kufatia hilo muungano huo wa mashariki kwa kipindi hicho ulioitwa Warsaw Pact ulianza kikao chake cha dharula mwezi February mwaka 1962 na ilipofika mwezi April mwaka 1962 walifikia uamuzi wa kuingia katika vita kamili ya kujihami dhidi ya umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO

Jumla ya askari 400,000 kutoka nchi mbali mbali za umoja wa kujihami wa nchi za mashariki walianza kusogea mipakani mwa nchi zao kujiandaa na vita dhidi ya umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO
Ilipofika August mwaka 1962 meli za kivita za Urusi zikiwa zimebeba askari zaidi ya 100,000 pamoja nyambizi zilizobeba silaha kali za nyuklia zilitia nanga kisiwani Cuba

Dunia yataharuki...

Mwezi September mwaka huo wa 1962 Rais wa Urusi wa wakati huo Nikita Khruschev aliwahakikishia nchi washirika wake wa mashariki kuwa endapo askari hata mmoja wa NATO angevuka mpaka na kuingia katika nchi zao basi nae angejibu mapigo kwa kuangamiza sehemu kubwa ya nchi ya Marekani hususani majiji ya New York na Miami, Kwani tayari nae alikuwa ameshaweka silaha kali za nyuklia mkabala na nchi ya Marekani, Inaonekana kabisa kuwa silaha hizo zilipelekwa kwa siri katika nchi ya Cuba.

Tamko hilo la Rais Nikita Khruschev lilizua hali ya taharuki ndani ya nchi ya Marekani, Haraka sana idara ya ujasusi ya nchi hiyo CIA ilifanya upelelezi wa haraka na kugundua kuwa ni kweli kabisa silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuangamiza taifa la Marekani zilikuwepo katika kisiwa cha Cuba mkabala na nchi ya Marekani

Vita kamili...

Tarehe 12 October 1962 bunge la Marekani lilikutana na kwa pamoja lilipitisha azimio la kuivamia nchi ya Cuba kwa haraka sana, Rais John F Kennedy Sasa alikuwa kwenye shinikizo kubwa sana la kutangaza vita ambayo kwa hakika ingekuwa ndio vita kuu ya Tatu ya Dunia, Akilihutubia taifa la Marekani usiku wa tarehe 16 October Rais Kennedy alisema kuwa kamwe taifa la Marekani halitoweza kuvumilia kitendo hicho cha kutishiwa usalama wake na akasema kuwa jeshi la Marekani litakwenda nchini Cuba kuziondoa silaha hizo kwa nguvu kwa sababu njia zote za amani zilikuwa zimeshindikana

Tayari jumla ya askari wapatao 300,000 pamoja na meli za kivita pamoja na ndege za kivita ziliwasili katika jiji la Miami kujiandaa kuivamia nchi ya Cuba, Meli kubwa kabisa za kivita za Marekani zilisogea karibu kabisa na kisiwa cha Cuba tayari kuanza mashambulizi ya kukiteka kisiwa hicho, Majeshi ya Cuba na Urusi nayo yalijibu mapigo kwa kusogeza vikosi vyake katika fukwe za kisiwa hicho mkabala na Majeshi ya Marekani

Uwanja wa mapambano...

Meli za kivita za Urusi zikiwa zimebeba silaha kali kabisa za nyuklia zikiwa Sasa zinakabiliana ana kwa ana na meli za kivita za Marekani, Tarehe 27 October 1962 ni siku ya kukumbukwa sana Duniani, Siku hiyo wizara ya ulinzi ya Marekani ilitoa amri kwa ndege zake za upelelezi za kivita kuingia katika anga ya Cuba, ndege hizo zilikuwa na kazi ya kuangalia Majeshi ya adui yamejipanga vip ili kuweza kukabiliana nayo, Ndege hizo ziliweza kuonekana na rada za Majeshi ya Urusi na mara moja walianza kuzishambulia.

Majeshi hayo ya Urusi yalifanikiwa kuangusha ndege moja ya upelelezi ya jeshi la Marekani jioni ya siku hiyo ya tarehe 27 October 1962 na kusababisha kifo cha askari wa jeshi la anga la Marekani luteni Rudolph Anderson, Kifo cha rubani mdogo mwenye umri wa miaka 34 Luteni Rudolph Anderson kilimsikitisha sana Rais John F Kennedy, Asubuhi ya tarehe 28 October 1962 Rais Kennedy alikwenda hadi nyumbani kwa familia ya marehemu kutoa salamu za rambi rambi.

Katika Hali ya kuhuzunisha sana Rais John F Kennedy alianza kulia baada ya kumuona mke wa marehemu akiwa mjamzito na pia aliwaona watoto wadogo wa marehemu mmoja akiwa na miaka 5 na mwingine akiwa na miaka 3, taarifa za kuangushwa kwa ndege ya kivita ya Marekani zilienea kwa kasi sana Duniani na Kila mtu alijua tayari Sasa Vita imeanza, Jeshi la Uingereza usiku wa siku hiyo lilituma kikosi maalum cha makomandoo kwenye mstari wa mbele wa kivita huko mashariki ya ulaya

Vasil Arkshipov aiokoa dunia...

Usiku wa siku iyo ya tarehe 27 October 1962 nyambizi ya kivita ya Urusi B-59 ikiwa imebeba silaha kali za nyuklia ikiwa chini kabisa ya bahari pasipo kuonekana na rada za Majeshi ya Marekani ilisogea karibu kabisa na pwani ya Florida ili kuanza mashambulizi endapo jeshi la Marekani lingeanzisha vita.

Nyambizi hiyo iliongozwa na Captain Savitsky pamoja na Admiral Vassil Arkhipov iliingia usiku huo karibu na Florida, Ikiwa chini kabisa ya bahari walianza kuhisi kufuatiliwa na nyambizi za jeshi la Marekani.

Wasilokuwa wakilijua askari Hawa wa Urusi ni Kwamba nyambizi hizi za jeshi la Marekani zilikuwa katika doria yake ya kawaida na wala haikuwa ikiifuatilia nyambizi hiyo ya Urusi, Kwa kuwa walikuwa chini kabisa ya bahari hawakuwa na mawasiliano yoyote na wenzao, Kulinganisha na hali waliyokuwa wameiacha Cuba Nahodha wa nyambizi hiyo Captain Savitsky alijua kabisa kuwa Sasa Vita imeshaanza na kwa maagizo waliokuwa wamepewa ni kusubiria vita ianze na kushambulia pwani za Florida kwa makombora ya nyuklia.

Haraka sana Captain Savitsky alitoa amri ya kufyatua makombora ya nyuklia kwa nyambizi za Marekani na pia kwenye fukwe za Florida zilipokuwa kambi za kijeshi na kituo cha kijeshi cha Marekani kwa wakati huo, Ili kutekeleza amri hiyo ilihitajika idhini ya Admiral Vassil Arkhipov.

Vassil alikataa kata kata kuachia makombora ya nyuklia kwa nyambizi za Marekani akisema kuwa swala zito kama hilo linahitaji amri na idhini kutoka Moscow na sio kwa yoyote yule, Askari wote wa kwenye nyambizi hiyo walikuwa wakipingana na Vassil mabishano ndani ya nyambizi hiyo yaliwachukua saa nzima na hatimaye wote wakakubali amri ya Admiral Vassil Arkhipov ya kutokupiga makombora ya nyuklia na haswa baada ya kuona nyambizi za Marekani zikiondoka bila ya kufanya shambulizi lolote kwao.

Hakika kilikuwa kitendo cha ujasiri sana kwa Vassil kuwashawishi wenzake wasishambulie nyambizi za Marekani maana endapo nyambizi zile za Marekani zingewaona na kuanza kuwashambulia wao basi ni dhahiri kuwa nyambizi hiyo ya B-59 ya Urusi ingeteketea na wote waliokuwamo ndani yake wangeuawa

Nyambizi hiyo ya B-59 iliondoka haraka sana eneo hilo na kurudi ilipokuwa ngome yao katika pwani za kisiwa cha Cuba usiku huo huo wa tarehe 27 October 1962 na vita ikawa imesimama, toka hapo Urusi na Marekani wakaanza mazungumzo ya Amani ya kuiepusha dunia kuingia kwenye uwezekano wa kutoka vitani.

 
Kwa hii trend ya wanajeshi wa Russia kufa mmoja Kwa Kila wanajeshi watatu na vifaa vyao vingi kuharibiwa ndio watateka UKRAINE yote?🤔
Huu Uzi unatakiwa upelekwe Kwenye jukwaa la kimataifa.
Umekuja ulidhani upo kwenye jukwaa la vichekesho eti ..... Ficha ujinga wako basi
 
Back
Top Bottom