View attachment 2229284
Zelensky: Urusi Inarusha makombora kwa sababu ya ukosefu wa mafanikio ardhini
https://bbc.in/3yKjukq
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amedai kuwa Urusi inarusha makombora ya masafa marefu katika miundombinu ya raia na ile ya kijeshi ya Ukraine kwa sababu jeshi lake haliwezi kuonyesha mafanikio yoyote muhimu.
Katika hotuba yake ya video iliyotolewa jana usiku, Zelensky alisema kumekuwa na ufyatuaji wa makombora katika maeneo ya Lviv, Sumy na Chernihiv, mashambulizi ya anga katika eneo la Luhansk na "shughuli za hujuma" katika maeneo ya mpakani.
"Haya yote sio tu kuleta mvutano kwa jimbo letu, sio tu kujaribu nguvu zetu," Zelensky anasema.
"Hili ni jaribio la jeshi la Urusi kufidia safu ya kushindwa mashariki na kusini mwa nchi yetu.
"Hawawezi kuonyesha mafanikio kwa hatua za jumla za kijeshi katika maeneo wanayojaribu kusonga mbele. Kwa hiyo wanajaribu kuonyesha mafanikio kupitia makombora yao na shughuli nyingine. Bila mafanikio pia."