Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kumbe jeshi la nchi moja(RUSSIA)anapambana na nchi zenye nguvu zaidi ya 30 na anawatoa kamasi.
Whatever you call it, lakini ukweli unabakia kwamba Urusi kapapasa sehemu isiyomuhusu., ataumia tu atake asitake.
 
Nikajua labda ulipotokwa tu kwenye post yako niliyo kuquote kumbe hizi ndo akili zako halisi, basi sina muda wa kuendelea kuhangaika na akili nyeupe kiasi hiki.

Kama mtu unaamini (japo hakuna yeyote Russia or westerners aliesema hivo) kuwa operation ya Urusi ingechukua wiki moja na kumpindua rais zelensky basi wewe ni bure kabisa katika haya mambo.

Kama Operation ya jeshi lako la askari polisi kupambana na panya roads wa chanika ilichukua zaidi ya wiki mbili, ndo operation ya jeshi la wanajeshi lak1 dhidi ya jeshi la nchi nzima ya ulaya limalize mission yake ndani ya wiki moja kweli?
Kwanza hayo maneno umeyatoa wapi na nani alisema na kwa ushahidi upi?

Sehemu nyingine unayoonesha weupe wako nipale unapoiita hii operation kuwa ni Vita, kama Pentagon na EU wanatumua neno Russia-Ukraine conflict na siyo Russia-Ukraine War, wewe hiyo vita umeitoa wapi na umeipima kwa criteria zipi?

Uliona wapi vita inapiganwa huku ukimsaidia adui chakula na matibabu kwa raia na wapiganaji wake?

Ama kweli siyo kila mwenye kichwa ana akili za kung'amua mambo wengine wanavitumia kuhifadhia meno na kufugia nywele tu wakijitahidi sana basi wanavitumia kuvukia barabara.
 
Unafikiri EU ana pesa za kuchezea? Kwanza alipoomba hizo $5 bil wakamshangaa.

Pia, Sasa hivi kila nchi zimeshafikia kikomo cha kutoa misaada, ndio maana huoni Tena zile mbwembwe za Kama awali.

Kama Ukraine angelikuwa anaonyesha kushinda hii vita, jamaa wangekuwa na moyo wa kuendelea kumsaidia.

Lakini kila msaada wa silaha wakimpatia zinaishia kuchomwa Moto. Sasa nani ataendelea na biashara ya namna hii..?
 
Myukrain wa buza jifariji TU,mrusi Alisha jikatia pande la ardhi lenye ardhi yenye rutuba,ukanda wa viwanda na bandari kama tatu za baharini,hapa upande mmoja yupo mrusi kaskazini,sehemu ya kaskazini magharibi swahiba wa mrusi,kipande alichokichukua kina muunga na cremia,lengo ni kukiunganisha na Moldova,upande uliosalia ndio polandi,Sasa hapo ulipo buza endelea kujifariji Ilhali wenzio wapo kikaangoni,wakiomba omba msaada kutoka Kwa mabeberu 🤔
 
Kuna watu humu wanajidanganya kwamba eti jaribu kumpa mbuzi rungu afu utegemee atampiga Tembo - Sasa subirini muone namna Ukraine anamkomesha mtu mzima.

Hizo Laser weapons mbona hatujaona zikimaliza battlefield ?


Russia Laser weapons on the battlefield in Ukraine.
 
Whatever you call it, lakini ukweli unabakia kwamba Urusi kapapasa sehemu isiyomuhusu., ataumia tu atake asitake.
Mpaka sasa zelenks anatembeza bakuli(kwamba mpunga Us anaompa hautoshi) ,western wanaomba UN iwasaidie kupata msosi kutoka Ukraine, Rubble imepanda thamani, India mnufaika wa punguzo la bei ya mafuta ya Russia,EU lugha gongana kuna wanaotaka mwanaume atolewe vikwazo ,Ugerumani na Poland wanamkwaruzano, USA kakiri kuna supa power tofauti na yy (china, Russia)
Mi naona uendelee kuchoma mahindi hapo kijiweni
 
Hakuna anayebisha kwamba Ukraine hatembezi bakuli, tunasema Mrusi alifikiri mambo ni laini, kakutana na kisiki kiasi hata yeye mwenyewe anashangaa.

Mwanzoni alisema atakayetoa usaidizi wowote kwa Ukraine atakiona cha moto sasa mbona wanatoa tu na hana la kufanya afu anaishia kulalamika.
 
Kama mtu unaamini (japo hakuna yeyote Russia or westerners aliesema hivo) kuwa operation ya Urusi ingechukua wiki moja na kumpindua rais zelensky basi wewe ni bure kabisa katika haya mambo.
BURE KAAAABISA, nakazia mwamba 😌
Kama Operation ya jeshi lako la askari polisi kupambana na panya roads wa chanika ilichukua zaidi ya wiki mbili, ndo operation ya jeshi la wanajeshi lak1 dhidi ya jeshi la nchi nzima ya ulaya limalize mission yake ndani ya wiki moja kweli?
Kazoea movie bro, Masaa mawili imeisha. Kizazi cha Spider Man hiki 😂
Sehemu nyingine unayoonesha weupe wako nipale unapoiita hii operation kuwa ni Vita, kama Pentagon na EU wanatumua neno Russia-Ukraine conflict na siyo Russia-Ukraine War, wewe hiyo vita umeitoa wapi na umeipima kwa criteria zipi?
Ndio uwezo wake wa kufikiri ulipoishia 😪
Ama kweli siyo kila mwenye kichwa ana akili za kung'amua mambo wengine wanavitumia kuhifadhia meno na kufugia nywele tu wakijitahidi sana basi wanavitumia kuvukia barabara.
Nakazia tena jomba...


Washeherashaji tupo makini 🤗
 
Kama una telegram search Intel Slava V uone uhalisia on ground. WiOn wapo neutral.
 
Mwezi wa 3 huo Mrusi kakwama kumaliza vita Ukraine, we doubt Russians military strength kwa kweli.
 
Kama una telegram search Intel Slava V uone uhalisia on ground. WiOn wapo neutral.
nishacheki, propaganda za kivita kibao wakati battlefield mambo magumu. tulitegemea sasa hivi Zelensky awe Poland mbio lakini wapi.
 
What is your reference?.
Kwenye military strengths?
Aisee utaumwa kichwa bure yaonekana haya mambo yamekuzidi kimo. Kwa nini usiende kwenye ule uzi wa Kimasihara.
Mwezi wa 3 huu kipi kinamsumbua Mrusi kumaliza vita? au vita hajaianza bali hiyo ni military operation tu - haya tujuze wewe unayeelewa mambo ya kivita 🙂
 
Haa Putin akiondoka sio kwamba vita itaisha no ,usinielewe hivyo atakayekuja hatakuwa mbaya kuliko Putin ila ndio atakayekamilisha hii operation kama ilivyokusudiwa.Warusi wanashangaa tu kwa nini Putin hamalizi kazi anathema makida making siku 90
Bora Putin kuliko ajaye putin anahuruma sana angekuwa yule aliyepita au mkuu wa majesh wa sasa kwanza vita ingekuwa ishaisha na ameua wengi
 
Yaani n hivii kwa mfano wewe apo(Ukraine) unaugomvi na mm(Russia) ila kuna mtu n baunsa kama mimi(NATO/US)nae pia ni adui kwangu ivyo kupitia vagi langu na ww anauchukua mkono wako ananitwanga ngumi( Proxy war).Umeona hapo ni kwamba hajanipiga direct ila anakutumia wewe sasa wewe kwa kujua au kutokujua unachakazwa.

Nimeona nikufungue macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…