Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mimi nafahamu cold War iliisha, wewe kama nani unasema cold haikuisha ikiwa Ukomunisti wa Mashariki chini ya USSR ulianguka rasmi mwaka 1990 na ubepari wa magharibi uka take over Ulaya ya Mashariki?
 
Zelensky analalamika kuwa shoga zake wa kimagharibi wameanza kumshinikiza akubali kustopisha vita vya Ukraine kwa kufuata matakwa ya Russia na pia kwa maslahi ya hao shoga zake (nchi za magharibi)...

Naona mabeberu yameshaona maslahi yao yapo mashakani ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha kwenye nchi zao, kukosa nafaka ikiwemo ngano, kupanda bei za gesi na wese...wameamua kuanza kumminya kibaraka wao

 
We kweli wasted sperm, huyo jamaa huwa habishani na watu, njoo kwangu. Tueleze hizo biashara za Opium zinaingiza faida kiasi gani ya kuweza ya kuhimili vita ya miaka 20. Kama US alipoteza Dola trillion 8 talebani kapoteza nini?
Kuna hadithi moja inasema hivi

Kulikuwa jamaa mmoja alikuwa amekaa nyumbani kwake
Mara rafiki yake akaja kumtembelea, basi katika maongezi jamaa akasema Leo nimeenda porini kukata majani ya ng'ombe wangu, nimekuta majani yamechipua vizuri yaani nimepata majani mabichi ya kijani,
Rafiki yake akajibu kuwa si kweli Yale majani yana rangi ya blue na Siyo kijani
Ukatokea ubishi mkubwa Sana mpaka wakaamua kwenda Kwa mkuu wa mkoa
Na wakaahidiana kuwa Yule ambaye atakuwa hayupo sahihi atachapwa bakora 12

Basi walipofika Kwa mkuu wa mkoa wakasema mkuu tusaidie Kati yangu na mwenzangu Nani yupo sahihi na Yule ambaye atakuwa hayupo sahihi aadhibiwe Kwa kuchapwa bakora 12

Mkuu wa mkoa akasema sawa hakuna tatizo, haya sasa niambieni mlikuwa mnabishania nini??

Jamaa akajibu tulikuwa tinabishana majani ya mimea Yana rangi gani??,
Mwenzangu anasema Yana rangi ya blue Mimi namuambia Yana rangi ya kijani, sasa tunaomba utupe jibu Nani yupo sahihi na Nani amekosea

Mkuu wa mkoa akainama akafikiria halafu akainuka akasema aliyesema majani yana rangi ya blue yupo sahihi na wewe unayesema Yana rangi ya kijani umekosea, Yule jamaa aliyesema Yana rangi ya blue akaruka juu Kwa furaha na kwenda mitaani huku akishangilia kuwa ameshinda

Basi jamaa akachapwa bakora 12 na akaanza kuondoka huku akisikitika, mkuu wa mkoa akamuita akamuuliza unajua kwanini nimekuchapa???

Jamaa akajibu sijajua na Nina uhakika jibu langu la kusema majani yana rangi ya kijani ndiyo sahihi
Mkuu wa mkoa akamwambia ni kweli unachokiongea Ila nimekuchapa Kwa sababu, wewe ni mwerevu na unajua sasa ilikuwa vipi ukabishana na mpumbavu ambaye ameamua kuita kijani kuwa blue????
Nimekuchapa Siyo Kwa kukosea swali Ila Kwa kitendo chako cha kupoteza muda wako na muda wangu kumfundisha mpumbavu

Kwa hiyo huwa najiuliza mnapata wapi ujasiri wa kuwaelimisha wapumbavu ambao hawataki kuelimika na kushikilia kile walichoaminishwa au kinachowapendeza????
 
Kisa kizuri mno... Nimekuelewa jomba. I mean sana tu saaaana tena sana mwamba 😊!
 
Hakuna vita visivyoisha, vita baridi iliisha mwaka 1990 baada ya USSR kuanguka na Ukomunisti wake, Kilichobaki ni USHINDANI na tofauti za mataifa, HAKUNA VITA. Wachina na Warusi wanapambana kukuza geopolitical powers zao dhidi ya Marekani na mfumo wa demokrasia duniani.
Kama wewe na ubishi wako wote huu hujui vita visivyoisha baina ya Russia na west basi ntapata taabu sana.
Sasa nakuuliza NATO IPO kwa ajili ya kujilinda dhidi ya nani?
 
β€ΌοΈπŸ‡­πŸ‡ΊHungarian FM Peter Szijjarto,about the words of the speaker of the Hungarian parliament Laszlo Kever about Zelensky's mental problems-Laszlo Kever is absolutely right,even if Ukrainians are outraged by this‼️ While in Hungary in recent months tens of thousands of people have worked to help Ukraine and the Ukrainian people, Ukrainian politicians constantly talk about Hungary in an unacceptable tone, provoke us, lie and try to denigrate us. They never expressed gratitude out loud.
 
Hivi Jamani hizi siraha zinapelekwa huko Ukraine zinaenda bure au wananunua maana kila nchi inataka kupeleka siraha huko.
Isije kuwa Kuna manufaa huko wanapata. Eti Jamani tujuzane.
 
Marekani yalalamika kuwa Russia inasafirisha ngano ya Ukraine (iliyoizuia kwenye maeneo ya Ukraine) kwenda kuiuza kwenye nchi 14 zenye uhaba wa chakula, nyingi katika hizo zipo Africa...

Marekani imechukia kwa nini ngano hiyo imepelekwa Afrika badala ya kupelekwa kwenye nchi za mabeberu ya kimagharibi, na hivyo imeamua kuziadhibu kidiplomasia nchi hizo zinazopokea ngano hiyo.

Russia ndio mkombozi wa Africa, hawa wengine ni mabeberu tu wananua ngano kutufikia sisi.
 
Jaribu ku summarize, mambo ni mengi sana humu ndani , ni vigumu kuweza kupata muda wa kusoma hadithi za Abunuwasi.
 
Marekani na Western Europe ni nchi kubwa kwa propaganda but in reality Russia kawaacha mbali sana! Kwa upande wa silaha
Huenda Russia sio nchi masikini kama tulivyoaminishwa kupitia propaganda
Mkuu hizo ni propaganda tu ambazo dunia iliaminishwa ila hii operation ndo imekuja kufunua ukweli wote,

β˜†Hakuna nchi masikini inayo ogopwa na USA, EU na NATO

β˜†Hakuna nchi masikin iliyo na uwezo wakuzionya jumuiya na nchi tajwa hapo juu.

β˜†Hakuna nchi masikini inayojitengenezea silaha zote za kivita tena zinazo ogopwa na super powers.

β˜†Hakuna nchi masikini ambayo mgogoro wake unaathili dunia nzima(e.g mfumuko wa bei na njaa)

β˜†Hakuna nchi masikini inayoweza kugeuza miji kuwa magofu huku dunia nzima ikiwa imeufyata hata kurusha jiwe ndani ya nchi hiyo.

β˜†Hakuna nchi masikini inayoenda kupigiwa magoti na UN, inayopigiwa simu na viongoz wa super power countries kuombwa isitishe operation.

β˜†Hakuna nchi masikin inayomiliki taasisi ya mambo ya anga za mbali(Roskosmos) na yenye uwezo wa kurusha satellites zake yenyewe bila msaada wa nchi yeyote. Satellites siyo Mitumbwi na anga siyo maji.

Mwisho: Twende mbele turudi nyuma Russia ni super power country na ni miongoni mwa nchi chache sana duniani iliyobarikiwa kuwa na utajiri wa asili(Mafuta, gesi, madini, utalii, nafaka, ardhi kubwa na n.k).
 
Halafu kuna wapuuzi bado wanaiona Marekani nchi ya maana, USA nchi ya kishetani sana.

Kwa hiyo anataka Afrika tufe kwa njaa kwa maslahi yake yeye.

Mungu saidia Urusi akamilishe hii operation kwa kadri ya malengo yake, halafu upepo wa dunia ugeuke tumechoka na ubabe wa USA.
 
Uongo namba 1;NATO wako kazini Kila siku kuchunguza Russia anafanya Nini.- *NATO Haina majasusi
Hakuna Taasisi ya Ujasusi ya NATO, usichanganye vyombo kama CIA, M16, MIT au Mossad na NATO*

Nao Russia wako makini kujua NATO wanafanya nini na kuwazuia- Elewa kwamba NATO ni alliance ya kijeshi tu, hakuna kitu kingine wanachofanya zaidi ya kujiandaa kijeshi dhidi ya mashambuli ya KIJESHI.

Nakukumbusha TU ni kazi ya majasusi wa Russia ndio iliyomuweka Trump madarakani- Uchaguzi wa Marekani ni Uchaguzi wa wazi kura zinapigwa na kuhesabiwa hadharani, hakuna kura za kwenye vikapu US, ukishinda unashinda kihalali ndio maana hukumuona Hilary Clinton analalamika ameibiwa kura.

Nao west walijaribu kutaka kumtoa Putin madarakani lakini walikutana na mkono wa majasusi wa Urusi- Thibitisha West walitaka kumtoa Putin Madarakani.
 
Huyu dogo tulimuonya aache ujinga alikuwa hasikii! Pia tulimwambia ngoma za watoto hazikeshi alikuwa hasikii shaulizake sasa!
 
Uingereza kupeleka Mzigo wa kuzidi Ukr πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20220606-144236.png
    123.5 KB · Views: 33
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…