Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hahahahahah 3 Sarmat Only! Kama kwenye deposit slip ya NMB yani😀😀😀
Tunapiga Marekani tu wengine wakiona moto mikia wataficha.
Sarmat tatu tu zinatosha kuiteketeza Marekani yote.
 
Hii vita imekwisha . Askari wa Ukraine wanakimbia mapigano ni hiyo ndio busara .Makamanda wao wanawakumbia na kuwaacha wenyewe. Katika mji uliochukuliwa na Russia hivi punde makamanda wa Ukraine wamevunja daraja wao wakasepa ili vijana wao washindwe kukimbia .Vijana wametupa silaha wakaogelea Warusi wamewaacha tu hawakutaka kuwadhuru
LoL!
Ila Russia wanahuruma sana, vita hii imekua ya kiungwana sana.
 
Unaona umeng'ang'ia Sana makombora basi upewe wew upige urusi mwenzako hana makombora ya kupewa ukimpiga ni kupakia tu kwenye vyanzo vya kurushia makombora na kuanza kuwatwanga hayo mabomu yakiisha uje uombe tena utakuta nchi Zima imekuwa mchanga kiasi kwamba mpka mbu watakosa parking
Ha ha ha haa"mpaka mbu watakosa parking".
 
Kelvin X We unazani kwa nini NATO wanamuogopa Russia kuliko hata shetani?

Wanajizungusha huku na kule. Na ukumbuke pia kwamba kuwa na Nuclear siyo tishio, tishio ni technology ya hizo nuclea weapons.

Usizani nuclear weapons za mataifa tofauti zina same S&T.


NATO wanazijua statistics halisi za uwezo wa Kivita wa Russia kwamba ni Hatari, acha hizi propaganda wanazo kulushia wewe, wao wanaujua ukweli.
Bro sisi wote tuna tegemea habari za vyanzo hivo hivo ila una fanya research kidogo. Rusia ana kadiriwa kuwa na nuclear war heards 6500 ila sasa US ana 5500, idadi sio ishu, US amefanya nuclear enrichment mara 500 ya lile la Nagasaki na Hiroshima.
 
ICBM sio silaa ni njia ya kufikisha silaha kutoka bara moja kwenda lingine na ukweli ni kwamba sio bara moja kwenda lingine ila wanaongelea masafa marefu. Mfano Marekani na Urusi zimepakana kule Alaska ICBM ya nini?

ICBM ina weza kufungwa kichwa cha nuclear au bom lingine lolote
I=inter
C=continental
B=ballistic
M=missile.
Nieleweshe vizuri kuwa ICBM sio silaha ni njia ya kufikisha silaha.
Plz.
 
Urusi hana jeuri ya kupigana na ushirika wa nchi zaidi ya thelathini ambazo kwa pamoja zina share gharama ya vita. Urusi ya Vladimir itafilisika tu.
Vita ni silaha na mafuta sasa Russia ana kila kitu plus chakula na ngano ya ziada anazipata huko huko front. Bei ya mafuta imepanda shauri ya vikwazo kwaiyo mauzo kidogo fedha nyomi
 
Teh Garry Kasparov ni Mrusi, aliye mlengwa wa jua linakozama. Yaliyomo ndani ya kitabu hicho na yale yanayotangazwa kutoka CNN, BBC na vyombo vyote vya magharibi kuhusu Putin yanafanana kasoro date of Publishing.

Hicho kitabu kakitoa 2015 baada ya sakata la Crimea. To Him, Putin ni threat na enemy to what He refer as "free world"... Kwamba He(Putin) need to be stopped.

Sasa hiyo free world ni nini? Ukikisoma atakupa majibu sitaki kumsemea mie [emoji23] kitabu kimejaa haya majina mawili, Russia na Putin.

Nakumbuka siku za mwanzo naanza kukisoma nilivoona title ikanivutia ila ndani sasa asalaleee. Hawa watu wako trained well kupandikiza aina ya fikra kwenye mind za watu.

Wakikukuta mweupe kichwani, yani huna taarifa za ziada aki ya mama huchomoi. Utalishwa "itikadi" hizo kila aliyepo mbele ako mwenye mtizamo tofauti na ule ulio elekezwa atakua adui. They are Professional Liers indeed!

Kingine nisije sahau, Winter is Coming anarefer Ujio wa Soviet uliovunjika milongo kadhaa iliyopita.

Kuna hadi movie ishachezwa yenye the same title, ka sikosei ni kwenye Game of Throne, Episode ya kwanza season 1 inaenda kwa hilo jina la Winter is Coming.

Kwa waliowahi kuiona hii series hiyo episode ya kwanza maudhui yake kiasi yanataka kufanana na hicho kitabu.

Hicho kitabu kinawafaa sana pro-NATO wakafanye palizi ya chuki zao zidi ya Putin zizidi kunawiri wazitumie kuhudumia familia zao!
Shukran kwa maelezo yako murua kabisa
 
Ni vita au operation?
Mtachanganyikiwa nyie.
Hii vita imekwisha . Askari wa Ukraine wanakimbia mapigano ni hiyo ndio busara .Makamanda wao wanawakumbia na kuwaacha wenyewe. Katika mji uliochukuliwa na Russia hivi punde makamanda wa Ukraine wamevunja daraja wao wakasepa ili vijana wao washindwe kukimbia .Vijana wametupa silaha wakaogelea Warusi wamewaacha tu hawakutaka kuwadhuru
 
Umenikumbusha Membe alivyosema Tz hata tukipewa msaada na shetani tutachukua tu[emoji1787]
Nafaka ni nafaka tu iwe ya wizi au halali ilimradi tunainunua kwa pesa zetu na ikipikwa tutakula na kushiba hao US wasitusumbue[emoji3]
 
Urusi hana jeuri ya kupigana na ushirika wa nchi zaidi ya thelathini ambazo kwa pamoja zina share gharama ya vita. Urusi ya Vladimir itafilisika tu.
na lengo kuu la mataifa ya magharibi ni kuoona URUSI ikidhoofu, kudhoofika kwa Urusi ndiyo itakuwa ushindi kwa mataifa ya Magharibi pamoja na US.

Putin kashaingia kwenye mtego, kuacha vita hawezi - he has only one option ni kupigana hadi mwisho though mwisho wenyewe utakavyokuwa hata yeye haujui.
 
Back
Top Bottom