Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

common cause to achieve the universal aspirations of mankind: peace and security, freedom, and the rule of law.
What? Tulitegemea kila anakotia mguu huyu the so-called champion of democracy, kungestawi na kushamiri na kuwanda vitu hivi (peace, security, freedom, rule of law).

Lakini kila mahali Marekani anapofungua mlango kuingia, hidaya hizi zinatoweka kupitia mlango mwingine. Wala huhitaji kubobea katika fani ya rocket science ili kulitambua hilo!
 
Watapita Kama hawaoni,

Waje na sababu zao, Kuna mrussi mmoja wa makambako kasema et sio eneo muhimu

Tunataka walete magazeti yao kwenye hili[emoji16]
Walikimbia. Walipoteza askari na vifaa. Jeshi la majini halikuwa na uwezo wa kuwalinda.
 
Russia wakati mwingine namuona yupo sahihi kujilinda lakini pia kitendo cha Marekani kutaka kuweka base za kijeshi Finland kinamfanya Russia awe na wasi wasi maana adui yako inchi yake ipo mbali inamaana siku vita inaanza Russia inakuwa battle ground sababu base za Marekani zipo karibu nae na wakiweka mitambo itamuangalia Russia.
Marekani hataki hasara.
 
Kipi kinatochuzuia sisi, Burundi au Zimbabwe kushindana na Marekani au China??
^Remotely controlled leaders!^ Tatizo ni viongozi wetu vibaraka ama visionless ambao bila Washington & London kuwaelekeza la kufanya, wala hata hawawezi kupiga japo hatua moja ya maendeleo chanya. Kifupi, wapo tu kama ile jana asubuhi!

Unategemea nini kwa nchi ambayo inaacha kuwa pro-active kwenye maendeleo himilivu kwa kutumia rasilimali zilizopo, badala yake inageukia kutafuta hisani, misaada, fadhila, na mikopo kwenye mataifa mengine?

Haina tofauti na mtu mwenye uwezo wa kujipatia riziki, lakini akaamua kujitegesha mahali juani na mvuani ili kuombaomba day in and day out.

Ndiyo sampuli ya watu kama hawa wanaomwona yule aliyehimiza ^Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea^ kwamba ni kichaa. Are we really serious?

Hiki ndicho Putin anakipiga vita left, right, centre, back, front!
 
Marekani kuna baadhi ya maeneo angekuwa anafanya kuwaachia uongozi walio nao maana kuna baadhi ya maeneo akiingia tu anavuruga kila kitu na amani inaisha kabisa,
Lakini wakati mwingine anasaidia kwa utawala mbovu baadhi ya nchi.
Maana kwa baadhi ya nchi zetu za Africa pasingekuwa na nchi za kukomea kuna viongozi kifo pekee ndio kingekuwa kina waondoa
 
Lakini wakati mwingine anasaidia kwa utawala mbovu baadhi ya nchi.
Ninastaajabu na kushangaa kwamba bado hujaijua Marekani vizuri.

Core principle yake ya international geopolitics iko hivi: ^Everyone's America's friend and partner as long as her goals are furthered and not hampered nor threatened therein. Therefore, US has no permanent enemy nor permanent friend!^

Mantiki yake ni kwamba, hata kama taifa fulani lingekuwa jahili na safihi kama nini, maadam Marekani anafaidika na ubia husika, uongozi wa nchi hiyo utaendelea kuneemeka na kudumu miaka nenda rudi.
 
Hapo wanamwaonea wananchi tu. Kama tunavyojua vyama vya mpira havina siasa, inakuwaje wanaingia kwenye siasa?
UEFA banned Russian clubs from its competitions in a package of sanctions announced May 2, which also excluded Russia's women's national team from this year's European Championship and qualifying for the 2023 World Cup.
 
Ni sawa ndugu lakini pia wanasaidia..
Ingawaji ya hiyo principle inayoisema.
 
Ni sawa ndugu lakini pia wanasaidia..
Ingawaji ya hiyo principle inayoisema.
Labda kama ^kusaidia^ unamaanisha ^kusaidia KUHARIBU!^

Hebu pitia nchi ambazo Marekani amejidukiza ndani yake. Linganisha hali yake kabla na baada ya uvamizi wao. Ndugu yangu, hata Wamarekani wenyewe wanalijua hilo! Libya, Syria, Afghanistan, na mataifa mengine lukuki.

Marekani ni zaidi ya saratani ambukizi & angamizi duniani.
 

Aya ya kwanza sahihi ya pili naipinga, hivi kumuondoa kiongozi madarakani hadi lije taifa lingine limtoe? Raisi wa Cameroon, Raisi Equatorial Guinea unajua wana miaka mingapi madarakani? Umri wa baba mwenye mjukuu, wote wapo na over 40+yrs madarakani. Kwanini hao hawakuguswa Gadaffi wakamnyanyua?

Mjomba hawa hawana shida na nani anayetawala as long as ni kibaraka wao haijalishi anatawala hadi kufa au siku mbili kang'olewa.

Kwanza huko nimeenda mbali, hapa jirani yetu Rwanda. Paul Kagame, toka April 2000 hadi leo 2022, miaka 22 yupo in Power... Vipi wana shida nae? Yupo in Power kushinda V-Putin anayeiwa Dictator. Ulishawahi kusikia wana mdisi? Au kukata uhusiano nae?
 

Huyu ndo wakupigana na Mrussi?. Walitudanganya wamefanikiwa kutest lenye spidi ya 5x ya sound sasa wanakiri walifeli[emoji1787]

Ndomana sishangai kuona nchi 30 zinamwogopa Russia [emoji635] [emoji1377]
 
RUSSIA linapokuja suala la vita hajawahi kutokua sahihi toka baada ya vita ya pili ya DUNIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna cha bure kwa hawa jamaa...kwao ni kula utalipa...ni mpumbavu tu tena wa kiwango cha kimataifa anayefikiri kuwa wanatupenda.

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
Watapita Kama hawaoni,

Waje na sababu zao, Kuna mrussi mmoja wa makambako kasema et sio eneo muhimu

Tunataka walete magazeti yao kwenye hili[emoji16]
Wote tupo...ila Hilo litaongelewa Sana...yaani hata akina Biden na Boris eti nao wanaliweka Kama ushindi...duh....aisee...Kama mna muda tafuteni feature/news analysis article ya BBC yenye kichwa Cha habari..Why Russia could not hold on Snake Island...someni hiyo halafu mfanye tathmini...ndipo mtajua, somehow, the reasons behind Russia's withdrawal of its forces from that Rocky island...
Russia ni strategists bwana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…