Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Mfano ukiangalia kuondka kwa Warusi Snake ISland. Ukpenda kuamini walikwenda kwa hiari yao, basi. Siamini.Kama mmedhibiti anga sasa si mkomboe maeneo yaliyochukuliwa kma umeweza kumiliki anga inamaana unauwezo wa kufanya chochote. Sasa mbona maeneo yana megwa daily na kuna taarfia wanajeshi 6000 wa Ukraine wame surrender mnafeli wapi chief?? Kama anga mmemiliki
Naelewa malezo ya Ukraine, kuna uhusiano na mizinga yao mpya ya 2S22 Bohdana. Wana chache tu lakini zinaweza kurusha grenedi janja 6 kwa dakika. Labda wameweka mbili tu kwenye pwani linalotazama kisiwa, ilhali wana picha kamili ya kila kitu, waliweza kuleta uharibifu mkubwa, bila Warusi kuwa na uwezo kujibu. Hivyo walikimbia.
Sasa mizinga hii iliweza kupiga kisiwa kutoka sehemu ndogo ya mwambao pekee, maana hazifiki zaidi ya kilomita 40. Sehemu hii ya mwambao iko kusini kabisa, karibu na mpaka wa Romania, urefu kama kilomita 16 na kutoka huko umbali hadi kisiwa ni chini ya km 40.
Kama Urusi ingekuwa na uwezo wa anga, ingetuma ndege 2 na kufyeka mizinga ya 2S22 Bohdana,
Ila hawakufanya. Kwa nini?
Nahisi wanakosa uwezo.
Hivyo afadhali kuwaondoa wanajeshi hapa kuliko kutazama jinsi walivyouawa wote.