Kaka vita ina gharama kubwa mno kwa siku, sisi tulipigana vita miaka ya 70 lakini toka hapo uchumi ukayumba hadi leo.
Tena hii vita haiishii kwenye Uchumi, Mrusi aanze kujiandaa kufanya yafuatayo:-
- Kuanzisha mashindano yake maana FIFA hatutaki kumwona sura yake
- Kuanzisha UEFA yake maana hatutaki kumwona sura yake
- Kuanzisha Olympic yake maaha hatutaki kumwona sura yake.
- Michezo yote inayohusisha Umoja wa Ulaya na NATO hatutaki sura yake.
Yaani ni hivi ndugu zangu Dunia ya leo usijifanye mtemi utaumia - huwezi kujitenga na wenye nguvu wenzako, atapata madhara mengi mno huyu anayejiapiza kwamba ni mtemi wa Dunia subirini anguko lake.