Jesus Mlokozi
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 2,690
- 21,122
⚔️⚔️⚔️Lugansk People's Republic is completely liberated⚔️⚔️⚔️
Asubuhi ya Leo umetuaminisha Ulaya na Marekani ni kitovu cha haki za binadamu yaani wanajali utu!
Sasa Askari wa Uingereza aliyekuzwa katika maadili ya utu ndiye anawanyima haki ya kuishi kwa amani na heshima wakimbizi wa Ukraine huko huko Uingereza.
Ukiangalia kwa jicho la Tatu tukio hili linakupa picha mtunza amani na utu huyu wa Uingereza anachokiwaza juu ya nchi walipotoka wakimbizi hawa!
Ukisikia leo hii mpinzani wa kisiasa wa Putin mwanahabari au mfanyabiashara mkosoaji wa Putin amepigwa risasi, amelishwa sumu, amefungwa kwa makosa ya uhujumu uchumi au amekimbilia uhamishoni basi uwezekano wa Putin/Kremlin kuhusika ni 99% ila ukisikia leo hii jambo kama hilo limetokea(kama litatokea) US ,EU au UK uwezekano wa Biden , Boris Johnson au mwanasiasa mwingine kuwa na mkono wake ni 0.1%.Ulaya na Marekani kuwa kitovu cha haki za binadamu haimaanishi huko hakuna watu waovu, wabuguzi na wadhalimu. Ndio maana bado wanao polisi na mahakama. Tofauti ya huko na sehemu nyingine ni kwamba huko uvunjifu wa haki za binadamu sio "state sanctioned", hakuna "impunity" na wanaotenda hayo matendo huwajibishwa katika mifumo ya sheria.
Haya hapa sasa [emoji116]mashambulizi ya makombora 30 ya Silaha za NATO bila hata kuua nzi [emoji16][emoji16]Siku nyingine mbaya kwa ProPutin Warusi wa Buza.Ukraine Waitwanga Kambi Ya Jeshi Ya Urusi Kwa Makombora[emoji848]
![]()
Putin rocked as Zelensky's troops unleash devastating shelling
VLADIMIR Putin's army has been hit by a devastating airstrike near Melitopol.www.express.co.uk
Ulaya na Marekani kuwa kitovu cha haki za binadamu haimaanishi huko hakuna watu waovu, wabuguzi na wadhalimu. Ndio maana bado wanao polisi na mahakama. Tofauti ya huko na sehemu nyingine ni kwamba huko uvunjifu wa haki za binadamu sio "state sanctioned", hakuna "impunity" na wanaotenda hayo matendo huwajibishwa katika mifumo ya sheria.
Hao ulaya na marekani waliomuua Patrice Lumumba,na kufanya mapinduzi ya serikali za kiafrika,Wana democracy na haki gani za Binadamu?
Kwani wamarekani wa Ushirombo wao wanasemaje?
![]()
Hatimae majeshi ya Russia yameingia katikati kabisa ya mji wa Lysychansk na kupeperusha bendera za Russia, Luhanski na Donbass.
Majeshi ya Russia yapo sambamba na vikosi vya majimbo yalojitenga ya Donetsk na Luhanski pamoja na vikosi vya wapiganaji wa Chechen.
Ingawa Ukraine wakanusha kuhusu taarifa hiyo lakini wizara ya ulinzi ya Russia imethibitisha kwamba sasa Russia inaudhibiti kwa asilimia 100 mji huo ambao wafanya jimbo zima la kusini mashariki la Donbass.
Hilo ndilo lilikuwa ni lengo kuu ya Russia kuchukua eneo lote la Donbass na kuliunganisha na Crimea ili kuweza kusaidia shughuli za ugavi wa silaha zaidi na kumalizia malengo mengine halisi ya kuichukua Ukraine nzima.
Lakini kabla ya hapo majeshi ya Russia yatapaswa kukomboa miji miwili ya Kramarorsk na Slovyansk ambayo ipo katika moja ya malengo yake na hapo jimbo zima ;a Donbass litakuwa chini ya Russia.
Kama nilivyokuwa nilileta habari fupifupi huko nyuma kwamba Russia ilikuwa yaitafuta Kramatorsk ambayo ipo katika jimbo la Donetsk ambayo pamoja na Luhanski yote yafanya jimbo kuu la Donbass.
Mji wa Lysychansk ulikuwa ndo mji pekee wa sehemu ya kusini mashariki ulokuwa ukishikiliwa na majeshi ya Ukraine na kupoteza mji huo ndio ishara tosha kwamba sasa Ukraine imebakia na mji pekee wa Kyiv.
Vyombo vya magharibi kwa makusudi makuu havitaweza kutangaza moja kwa moja hatua hii ilofikiwa na Russia lakini kadiri siku zinavyojiongea vyombo hivyo vitapaswa kutangaza jambo hilo ambalo ni ushindi mkuu kwa Jamhuri ya Russia.
Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na mkuu wa majeshi yanoendesha operesheni hiyo muhimu kwa Russia tayari wamemtaarifu rasmi raisi Putin juu ya ukombozi wa mji wa Lysychansk.
Mtakumbuka kuwa tarehe 21 mwezi Februari nilileta taarifa ya kuhusu raisi Putin kutia saini amri ya kuyatambua rasmi majimbo ya Luhansk na Donetsk na nini kingefuatia- Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk
Vita si kitu kizuri na hakuna apendae vita, ila kuna wakati yapo masuala ambayo hulazimisha vita.
Masuala hayo ni usalama wa taifa, rasilimali na mipaka yake yote na nafasi ya taifa husika kieneo na pia maslahi ya taifa ndani ya nje ya mipaka yake.
Mengine ni kulinda heshima ya taifa husika, alama yake pamoja na utaifa wake.
Raisi Putin maechukua maamuzi magumu kutekeleza vita hii ili kulinda heshima ya Russia kama moja ya mafaita makubwa duniani.
Kazi yaendelea.
Kwani mkuu Richard?
![]()
Hatimae majeshi ya Russia yameingia katikati kabisa ya mji wa Lysychansk na kupeperusha bendera za Russia, Luhanski na Donbass.
Majeshi ya Russia yapo sambamba na vikosi vya majimbo yalojitenga ya Donetsk na Luhanski pamoja na vikosi vya vya wapiganaji wa Chechen.
Ingawa Ukraine wakanusha kuhusu taarifa hiyo lakini wizara ya ulinzi ya Russia imethibitisha kwamba sasa Russia inaudhibiti kwa asilimia 100 mji huo ambao wafanya jimbo zima la kusini mashariki la Donbass.
Hilo ndilo lilikuwa ni lengo kuu ya Russia kuchukua eneo lote la Donbass na kuliunganisha na Crimea ili kuweza kusaidia shughuli za ugavi wa silaha zaidi na kumalizia malengo mengine halisi ya kuichukua Ukraine nzima.
Lakini kabla ya hapo majeshi ya Russia yatapaswa kukomboa miji miwili ya Kramarorsk na Slovyansk ambayo ipo katika moja ya malengo yake na hapo jimbo zima ;a Donbass litakuwa chini ya Russia.
Kama nilivyokuwa nilileta habari fupifupi huko nyuma kwamba Russia ilikuwa yaitafuta Kramatorsk ambayo ipo katika jimbo la Donetsk ambayo pamoja na Luhanski yote yafanya jimbo kuu la Donbass.
Mji wa Lysychansk ulikuwa ndo mji pekee wa sehemu ya kusini mashariki ulokuwa ukishikiliwa na majeshi ya Ukraine na kupoteza mji huo ndio ishara tosha kwamba sasa Ukraine imebakia na mji pekee wa Kyiv.
Vyombo vya magharibi kwa makusudi makuu havitaweza kutangaza moja kwa moja hatua hii ilofikiwa na Russia lakini kadiri siku zinavyojiongea vyombo hivyo vitapaswa kutangaza jambo hilo ambalo ni ushindi mkuu kwa Jamhuri ya Russia.
Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na mkuu wa majeshi yanoendesha operesheni hiyo muhimu kwa Russia tayari wamemtaarifu rasmi raisi Putin juu ya ukombozi wa mji wa Lysychansk.
Kazi yaendelea.
Kwa sababu hizo ndio serikari zinazowafadhili ili kuweza kutimiza matakwa yao, yaani kupitisha ajenda zao.Sasa kwa nini wapinzani kama Lissu na Wanaharakati wakosoaji wa serikali nyingi za Africa bado wanakimbilia huko Ulaya na Marekani kulinda maisha yao??
Kwa sababu hizo ndio serikari zinazowafadhili ili kuweza kutimiza matakwa yao, yaani kupotosha ajenda zao.
Turejee tukio la Tundu lisu kutaka ku
Kusivunjwe mikataba ya kinyonyaji ya madini na kelele zake.
Cuba nao wakiweka kwenye katiba Yao kifungu Cha kuruhusu Urusi kuweka silaha zake Cuba USA atakua confortable?Haki yao ya kikatiba ni pamoja na kujiunga NATO na EU.
Kuna kifungu kabisa ndani ya katiba yao kinachosema hivyo! Sijui kama unafahamu hilo!
Ujue mkuu hapa tunatumia lugha hadhimu ya kiswahili.
Mkuu, ntafafanua kidogo.Kwani mkuu Richard?
1.Ebu nfafanulie kdogo, Iiv mpaka leo hii kinachofanya ukrain bado inamiliki UKULU ndani ya mji wa kyiv ni kipi?
2.Na..
Ni uenda inteljensia ya PUTIN inashindwa kuelewa ni wapi mamraka kuu ya nchi ipo wapi au imekaaje?
3.Ikulu ya ukrain ina ulinzi mkari saaana kupita nguvu ya jesh la PUTN? au ipoje.?
4.na je? lengo la putin ni kuleta heshima kwa NATO na kurudisha tu maeneo baadhi ya miji kwake?au kuimiliki nchi nzima?.
Kwako mwalimu.
Hehe hee POLENIWakimbizi wa Ukraine watarudi nchi mwao hata leo hii kama Putin akiacha kurusha makombora kwenye malls, shule, na makazi ya Wa Ukraine na akiondoa wanajeshi wa Russia wanaokalia nyumba, mashamba, na makazi yao huko Mashariki walipokimbia.
Putin, wafuasi na wapenzi wake hamtaweza ku "rewrite" historia hii ovu ya Russia.
Leo usiku sikilizeni mziki wa Russia huko Kiev . Hawa jamaa na Irani deni lao Huwa halilali.Walirusha yakawa intercepted, yamedondokea kwenye makazi yameondoka na watu kama wa 4 hivi.
Pongezi kubwa kwako,nimeeelewa mkuu.Mkuu, ntafafanua kidogo.
Kwanza fahamu kuwa hii vita ni kama game.
1. Kyiv ndo makao makuu ya serikali ya Ukraine hivyo kanuni za vita majeshi ya adui yanapoteka mji majeshi wenyeji hulazimika kujisalimisha khasa baada ya kuzungukwa. Utakumbuka kwamba hapo mwanzo Russia walikosea mbinu kwa kuanza na Kyiv lakini baadae wakabadili mbinu ndo wakaanzia chini ili kulinda sehemu hiyo na pia kuhakikisha shughuli za ugavi wa silaha na mawasiliano na manowari zilizoko kwenye bahari nyeusi.
Hivyo serikali ya Ukraine itaendelea kukaa Kyiv hadi mwisho hapo ambapo ndippo vita kali itapigwa, kumbuka sasa lengo la Russia limebadilika ataka Ukraine nzima.
2. Russia na Putin wanafahamu kila kitu nani yupo wapi na Zelensky yupo wapi kumbuka Russia wana mitambo ya satelite hivyo hata makombora wanopiga kudungua maghala ya silaha ni kutokana na doria za satelite.
3. Ikulu ya Ukraine mjini Kyiv ina ulinzi na mitambo mingi mipya yaani ADF imefungwa na ndo maana viongozi wengi wa mataifa ya nje bado waenda kumuona Zelensky na leo PM wa Australia ametua Kyiv. Hivyo elewa kuwa ulinzi upo lakini "the battle of Kyiv" ndo yangojewa. Pili Russia anafanya mambo yake kwa mipango na ungalifu hivyo Kyiv imeachwa mwisho ingawa huko baadae Ukraine yaweza kugawanyika kati ya kaskazini yaani Kyiv na Kusini yaani Donbass.
4. Kwa jinsi ambavyo NATO imejipambanua ( kwa kuwakaribisha Sweden na Finland) Russia haijasema wazi kuwa yataka Ukraine yote ila kwa mwenendo ulivyo yaonekana wazi kuwa malengo halisi ya Russia ni kuichukua Ukraine nzima.
Russia ikiiachia Kyiv peke yake bado haitajiona iko salama zaidi ingawa tayari wamesogeza silaha zaidi ya nyuklia pale Kaliningrad ambapo ndo makao makuu ya jeshi la majini la Russia yaani Russia navy wakilinda eneo lote la Baltic.
Ila kiukweli kabisa hakuna anefahamu kiuhalisi kabisa nini kinofuataia endapo kwanza Russia ikimaliza kazi ya Donbass kwa asilimia 100.
Ha ha ha Jomba jombaaa... Hii reply ina msisimko wa aina ake 😂😂😂Leo usiku sikilizeni mziki wa Russia huko Kiev . Hawa jamaa na Irani deni lao Huwa halilali.