Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Cha ajabu mi so mwarabu Ni mkatoliki Safi . Niliumizwa zaidi na alichofanyiwa colonel gadafi.
Nikaamua kuwa upande ambao Ni salama bila kujali cool Gadaf alikua mwarabu

Kwa Wakristo na watu wa madhehebu mengine ukiwaskliza kwenye huu ugomvi wanatumia akili yao vizuri maana wamegawanyika, kunao wako upande wa Urusi ila kunao wako upande wa Ukraine, ila hawa wa dini ya mwarabu wamemwagika wote upande wa Urusi kisa wanaamini anamkomoa Marekani, ambaye siku zote wameaminishwa ndiye adui wa dini yao, ila utakuta wanajaza fomu za green card wakale bata Marekani.

Sio mitaani au maofisini kila mfuasi wa dini ya mwarabu ninayekutana naye yupo upande wa Urusi, na hoja yao ni moja tu, kwamba Putin anapiga mashoga wa Ukraine.
Jana ofisini nimebishana kwa hoja na Wakristo ambao wako upande wa Putin, tumepelekana vizuri maana ukiwaskliza kwa namna fulani kwa kweli wanatumia akili zao vizuri, kuna namna fulani wana hoja zenye mashiko, na pia na wao wanazikubali baadhi ya hoja zangu, mjadala wote ulikua balanced.

Sasa njoo kwa hawa waarabu wa kwa Mtongole, jamaa anashikilia la ushoga, ukimbana kwamba Ukraine haiongozi dunia kwa idadi za mashoga, anahamia kwanini Ukraine inataka kujiunga NATO ilhali yenyewe ni jirani wa Urusi, ukimbana kwenye hilo kwa kumwambia Latvia ni jirani wa Urusi na yuko NATO, anahamia kwa hoja kwamba Ukraine kuna manazi, ukimbana kuwa rais wa Ukraine ni Myahudi jamaa anaanza kutokwa povu na kusema mashoga wauawe tu.
 
Huna unachojua ndomana nikikwambia wewe sio mfuatiliaji unanibishia. Huu mgogoro unafuatiliwa dunia nzima Sio Tanzania tu. Inshort Russia ana support kubwa sana watu washachoka na ufedhuli wa WEST.

Kwa povu za Watanzania hususan wafuasi wa dini ya mwarabu ni tofauti sana na wanavyojadili duniani kwingine, huu mgogoro nimeufuatilia sana tena kwenye social media nyingi, ila sijaona utashi kama wa kwenu nyie wafuasi wa mwarabu.
 
Nyinyi ndio mlianza kushabikia kuanzia UN mpaka Nairobi,unajifanya umesahau wakati mliweka bendera ya Ukraine pale KICC? Onyesha wapi serikali yetu,au mwananchi watz wamehangaika na bendera za Urusi,au matamko ya kijinga kama yenu?

Naongea kuhusu nyie wafuasi wa dini ya mwarabu, hamna social media nyingine dunia hii imechachamaa ushabiki wa Urusi kama nyie humu, huwa niko kwenye nyingi tu nafuatilia, kule kwingine watu wako balanced ila nyie mumeshikiliwa akili kwa mitazamo ya kidini.
 
Kwanza sidhani kama kuna taifa limeweka ushabiki kwenye huu mgogoro wa Ukraine kama Tanzania, yaani JF hapa mnalumbana hata kuwazidi Ukraine-Urusi wenye ugomvi wao, kisa tu mitazamo ya kidini hususan kwa nyie afuasi wa dini ya mwarabu.
Nahisi ushabiki kuhusu Urusi - Ukraine upo katika nchi nyingi. Ila Tanzania inafaa kuwa na majadiliano makali.
Tanzania masimulizi haya ya "kupinga ukoloni na ubeberu" yana nguvu.
Na katika historia ya nchi watu wengi waliona ukoloni na ubeberu kwenye "magharibi" na wapiganaji wa uhuru -hasa Wazanzibari- walipata msaada kutoka Urusi / Umoja wa Kisovyeti. Pamoja na nchi za magharibi kusaidia Rhodesia na Afrika Kusini kwa miaka kadhaa wakati wa ubaguzi wa rangi, ilhali Urusi / Umoja wa Kisovyeti ilisaidia wapiganaji wa uhuru.

Kwa upande mwingine Urusi yenyewe ilikuwa mkoloni mkubwa mojawapo duniani, ikaendesha ubeberu Asia (na Ulaya Mashariki), lakini mbali ya Afrika.

Je ilisaidia wapiganaji uhuru wa Afrika kwa sababu ilipenda Waafrika na uhuru wao?
Au ilichukua nafasi ya kuingilia kati kama beberu mmoja aliyelenga hasara ya beberu mwingine?
 
EMP forces zishafanyiwa majaribio miaka ya Cold war na ni rahisi kwa wenye nuclear ICBM. Sasa badala ya kutumia EMP si ni sawa na kutumia missile ikapiga kwenye silo.

Na hilo suala linajulikana ndio maana kuna mutual assured destruction. Na bado kuna nuclear deterrent triad kwamba kwenye land kuna Minuteman III zipo kwenye silos mamia ya makombora. Kwenye anga kuna B-52 Stratofortress, B-1B Lancer, B-2 stealth bomber na sasa mpya za B-21 Raider ziko na mabomu na missiles za nyuklia. Majini kuna Ohio class subs zipo na mamia ya warheads.

Alafu tunajichosha, ni mpuuzi pekee either ndani ya Russia au Marekani anaweza anzisha nuclear exchange
Kwa hiyo tukanunuae mafuta Urusi au tuache !!??
 
Urusi ilipoteza idadi kubwa ya vifaru tayari. Hasa zile ambazo zinaua askari ndani yake wakati grenedi zinazotunzwa ndani yake zinalipuka (hapo picha za vifaru hivyo na kichwa cha bunduki pekee). Labda wana akiba bado ya vifaru lakini tatizo kubwa zaidi ni kuwa na askari wa kutosha waliofundishwa kuvitumia. Hii inahitaji muda - ukiweka vijana bila mafunzo ya kutosha katika mashine hizo, utapata matokeo kama kwenye video.

(tatizo hili ni sababu vifaru yva NATO vyote vina muundo tofauti - grenedi hazitunzwi katika sehemu pamoja na askari; hivyo uwezekano wa askari kutoka hai baada ya kifaru kimepigwa ni kubwa kuliko kwenye vifaru vya Kirusi. -- Warusi walitambua udhaifu wa vifaru hivyo (T64, T72, T80+T90) hapo walipobuni T-14 Armata - ambayo ni bora lkakini haipo, walishindwa kutengenza zaidi ya vifaru chini ya 20 vilivyoonyeshwa kwenye peredi...)
Urusi gani hiyo unayo zungumzia, labda urusi ya kwamparange ndiyo imeishiwa silaha.....majuzi tu urusi imepata Oda ya kuiuzia india silaha za mabilioni ya dola ..... Urusi ndiyo moja ya nchi 3 duniani zinazo ongoza kuuza silaha nyingi duniani ....sasa nchi yenye uwezo wa kuzalisha silaha za kuuza dunia nzima unasema ineishiwa vifaru .....
 
Back
Top Bottom