Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Cha ajabu mi so mwarabu Ni mkatoliki Safi . Niliumizwa zaidi na alichofanyiwa colonel gadafi.
Nikaamua kuwa upande ambao Ni salama bila kujali cool Gadaf alikua mwarabu

Kwa Wakristo na watu wa madhehebu mengine ukiwaskliza kwenye huu ugomvi wanatumia akili yao vizuri maana wamegawanyika, kunao wako upande wa Urusi ila kunao wako upande wa Ukraine, ila hawa wa dini ya mwarabu wamemwagika wote upande wa Urusi kisa wanaamini anamkomoa Marekani, ambaye siku zote wameaminishwa ndiye adui wa dini yao, ila utakuta wanajaza fomu za green card wakale bata Marekani.

Sio mitaani au maofisini kila mfuasi wa dini ya mwarabu ninayekutana naye yupo upande wa Urusi, na hoja yao ni moja tu, kwamba Putin anapiga mashoga wa Ukraine.
Jana ofisini nimebishana kwa hoja na Wakristo ambao wako upande wa Putin, tumepelekana vizuri maana ukiwaskliza kwa namna fulani kwa kweli wanatumia akili zao vizuri, kuna namna fulani wana hoja zenye mashiko, na pia na wao wanazikubali baadhi ya hoja zangu, mjadala wote ulikua balanced.

Sasa njoo kwa hawa waarabu wa kwa Mtongole, jamaa anashikilia la ushoga, ukimbana kwamba Ukraine haiongozi dunia kwa idadi za mashoga, anahamia kwanini Ukraine inataka kujiunga NATO ilhali yenyewe ni jirani wa Urusi, ukimbana kwenye hilo kwa kumwambia Latvia ni jirani wa Urusi na yuko NATO, anahamia kwa hoja kwamba Ukraine kuna manazi, ukimbana kuwa rais wa Ukraine ni Myahudi jamaa anaanza kutokwa povu na kusema mashoga wauawe tu.
 
Huna unachojua ndomana nikikwambia wewe sio mfuatiliaji unanibishia. Huu mgogoro unafuatiliwa dunia nzima Sio Tanzania tu. Inshort Russia ana support kubwa sana watu washachoka na ufedhuli wa WEST.

Kwa povu za Watanzania hususan wafuasi wa dini ya mwarabu ni tofauti sana na wanavyojadili duniani kwingine, huu mgogoro nimeufuatilia sana tena kwenye social media nyingi, ila sijaona utashi kama wa kwenu nyie wafuasi wa mwarabu.
 
Nyinyi ndio mlianza kushabikia kuanzia UN mpaka Nairobi,unajifanya umesahau wakati mliweka bendera ya Ukraine pale KICC? Onyesha wapi serikali yetu,au mwananchi watz wamehangaika na bendera za Urusi,au matamko ya kijinga kama yenu?

Naongea kuhusu nyie wafuasi wa dini ya mwarabu, hamna social media nyingine dunia hii imechachamaa ushabiki wa Urusi kama nyie humu, huwa niko kwenye nyingi tu nafuatilia, kule kwingine watu wako balanced ila nyie mumeshikiliwa akili kwa mitazamo ya kidini.
 
Kwanza sidhani kama kuna taifa limeweka ushabiki kwenye huu mgogoro wa Ukraine kama Tanzania, yaani JF hapa mnalumbana hata kuwazidi Ukraine-Urusi wenye ugomvi wao, kisa tu mitazamo ya kidini hususan kwa nyie afuasi wa dini ya mwarabu.
Nahisi ushabiki kuhusu Urusi - Ukraine upo katika nchi nyingi. Ila Tanzania inafaa kuwa na majadiliano makali.
Tanzania masimulizi haya ya "kupinga ukoloni na ubeberu" yana nguvu.
Na katika historia ya nchi watu wengi waliona ukoloni na ubeberu kwenye "magharibi" na wapiganaji wa uhuru -hasa Wazanzibari- walipata msaada kutoka Urusi / Umoja wa Kisovyeti. Pamoja na nchi za magharibi kusaidia Rhodesia na Afrika Kusini kwa miaka kadhaa wakati wa ubaguzi wa rangi, ilhali Urusi / Umoja wa Kisovyeti ilisaidia wapiganaji wa uhuru.

Kwa upande mwingine Urusi yenyewe ilikuwa mkoloni mkubwa mojawapo duniani, ikaendesha ubeberu Asia (na Ulaya Mashariki), lakini mbali ya Afrika.

Je ilisaidia wapiganaji uhuru wa Afrika kwa sababu ilipenda Waafrika na uhuru wao?
Au ilichukua nafasi ya kuingilia kati kama beberu mmoja aliyelenga hasara ya beberu mwingine?
 
Kwa hiyo tukanunuae mafuta Urusi au tuache !!??
 
Urusi gani hiyo unayo zungumzia, labda urusi ya kwamparange ndiyo imeishiwa silaha.....majuzi tu urusi imepata Oda ya kuiuzia india silaha za mabilioni ya dola ..... Urusi ndiyo moja ya nchi 3 duniani zinazo ongoza kuuza silaha nyingi duniani ....sasa nchi yenye uwezo wa kuzalisha silaha za kuuza dunia nzima unasema ineishiwa vifaru .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…