Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 13,481
- 26,392
Thanks! Hii katika medani za kivita inaitwa TACTICAL PREPOTENCY (China over US) na TACTICAL PREDOMINANCE (US over everybody else).Kwa China bora direct War kuliko vikwazo kama US atatafuta ushindi dhidi yake. Ndio maana kila mda najaribu kusema tusubiri end results tutakuwa na mengi ya kuzungumza.
Kama mnafatilia haya mambo vizuri niwape swali lingine mlitafakari.
Kwanini US hapendi direct war (military) with Russia (Simsemei kalisema mara nyingi tu) hapo hapo anakwepa vita ya kiuchumi dhidi ya China (mkumbuke alimpa vitisho vingi dhidi ya mahusiano yake na Russia yet hadi sasa hajafanya chochote na China anaendelea kufanya biashara zake na Russia).
Kwanza inabidi tuelewe kua China ni Superior in term of economy, anampa challenge US kwenye huu upande. US anaweza kupigana na huyu kivita ila sio kiuchumi.
Russia ni superior in term of military, huyu anampa challenge US ukurasa huu. Nae US anaweza kupigana na Russia kiuchumi ila sio kivita.
Ukimya wa China jana ni ushindi kwa East no matter nyie mnalitizama vipi. Jana Marekani kanyimwa kile alichokua anakitaka, ambayo ni vita kati yake yeye na China. Vita ambavyo again ingemsaidia kupiga ndege wawili kwa pa1. (China en Russia)
Sasa tubaki tunazungumzia issue ya vikwazo na kivipi US hawezi hiyo league kwa China.
🔸Mosi China ni World largest producer, kampiku US miaka kadhaa iliyopita. Asilimia 28 ya vitu vyote duniani vinatengenezwa China. China ni world largest manufacturing hub kuliko US tena kwa tofauti karibu 10%
Ukitaka kujua litaiathri vipi dunia, angalia GERMANY hapo EU ambayo ni third largest manufacturing hub duniani kuyumba kwake kulivyo haribu uchumi wa ulaya kwa pa1.
Hiyo situation ya Germany izidishe mara 6 ndio itakuwa hali ya China kwa "Chumi" zingine duniani.
🔸US na China wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa, ila hii biashara kati yao ni kua US anaagiza vingi kutoka China kuliko China anavyochukua kutoka US. Kufupisha maelezo ni kua US ana trade deficit with China.
Hapa kati mlisikia hadi "baby formula" za US zatoka China, So umewaza nini kitajiri kwenye vita ya kiuchumi dhidi yake?
🔸 Main Supplier wa industries za US ni China. Kuipiga vikwazo china ni kuharibu industry sector ya kwake mwenyewe US. Lugha nzuri hapa niseme itakuwa ni self destruction.
All giants US companies zaitegemea China na mwanae Taiwan kwa mambo mengi, mfano wengi hapa hukimbilia final products ya bidhaa tunazotumia bila kujua au kuangalia imetengenezwa kwa kipi na kipi kutoka kwa nani na nani.
🔸Again china anashikilia deni la US zaidi ya Dollar trillion 1.
Akiamua kuliuza hili deni kwa speed ata trigger inflation US zaidi ya ilivyo sasa je nini kitajiri?
🔸Ukitizama sectors muhim za uchumi wa China zipo balanced. Industries, Agriculture, Services zina almost uwiano sawa. Lakini kwa US Sector kubwa ni "Services" ambayo inachangia zaidi ya 80% ya pato la taifa (GDP).
Uchumi ambao uko vulnerable kuharibika ni wa US ambao unategemea maisha mazuri ya Raia wake. (Spending ndio key ya Services Economy), hali ngumu kwa Raia inapelekea Spending kua kidogo, hivyo kuathiri hii sector. Na hili ndio jibu la kwanini quarter zote hizi mbili uchumi wa US unaonesha negative growth wakati hayupo kwenye vita na yoyote (kwa mujibu wa vyombo vyao vya habari 😅).
🔸China ni largest creditor duniani kuliko hata hizi taasisi za fedha za kimataifa mnazozijua. Hapa tusiweke maelezo mengi kwani kila mmoja anajua mikopo ni utumwa. Mkopeshaji ana sauti juu yako, Mzinguane akutie default. Je US ataweza kumshawishi nani asijihusishe na China?
Natamani kuendelea kukuonesha namna gani vita ya kiuchumi kwa US na China ilivyo ya kufikirika kama ilivyo vita ya Silaha kati ya Russia na US sema asubuhi hii nitachelewa kufanya mambo mengine.
Hapo kwa China vs US wakisema walianzishe (Vita ya silaha) atakaye athirika haraka ni China ambae adui yupo mlangoni mwake. Hatopata nafasi ya kutoka nje kwenda kutafuta nyumba ya adui ilipo.
Kuna njia nyingi za China kuiadhibu marekani kuliko kuuwana kwasababu ya hicho kibibi kinachoelekea kutia "nanga".
Mfano ka chini fikiria vipi China akiamua kufanya just one Move, yani "act 1" tu kama ya Russia ya kusettle payment za bidhaa zake kwa fedha yake. Nini kitatokea kweye dollar? Kupotea kwa dollar kuna maana gani kwa taifa la US?
😀
Tuishie hapo nikipata mda nitarudi, nakazia kile kile tusim'overestimate China wala kum'underestimate. Sie tutulie kati kwa kati tuenjoy show!
Maana now mpira upo kwa China, ana kila sababu za ku'retaliate against US bila kunyooshewa kidole. Kwetu sie warusi wa machame ni burudani tu 🤗.
Muhtasari wa maelezo yote ni kua US anaweza kupigana kivita na China ila sio kiuchumi, US anaweza kupigana na Russia kiuchumi ila sio kivita.
cc: T14 Armata (tuletee japo comment yako ya mstari mmoja mkuu)!
