#HUENDA CHINA IKAPORWA TONGE MDOMONI HUKU INAJIONA
Tayari Nancy pelosi kashatua Taiwan na hatuajaona china akiivamia Taiwan
Sasa kituo kinachofata ni Taiwan kujitangazia uhuru wake,
Bado mchina hajakwepa mtego wa marekani
BEHIND THE SCENE
ukiangalia china ndo taifa la pili Kwa uchumi duniani baada ya marekani, na ndio linaleta challenge ya kiuchumi Kwa marekani, hilo marekani anaitafuta china Kwa Kila namna iingie kwenye mgogoro ili iwekewe vikwazo na pia kuifanya ukuaji wake wa kiuchumi udumae
Kwa mujibu wa ripot ya shirika fedha Duniani IMF, inakadiliwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2022, uchumi wa marekani utafikia GDP 24 trillion us dollar wakati uchumi wa china utafikia GDP 18 trillion us dollar [emoji385]
Lakini hilo sio kubwa sana, kikubwa ni Kasi ya ukuwaji wa uchumi wa mataifa hayo, ripot ya IMF inaonesha Kwa mwaka huu 2022 ukuaji wa uchumi wa marekani ni WA kiwango Cha asilimia 3.5% wakati china ni 5.57% hii inaonesha picha nzuri Kwa upande wa china
Lakini pia wataalamu wa uchumi wa IMF wanakadilia ifikapo mwaka 2026 uchumi wa marekani utakuwa ni GDP 27 trillion us dollar[emoji385][emoji383] wakati china itakuwa na uchumi wa GDP 24 trillion us dollar [emoji385][emoji383]
Hapo utaona Kuna utofauti wa gap, kati ya mwaka 2022 na 2026 ambapo Kwa mwaka 2022 china imepigwa gap la kiasi Cha 6 us dollar trillion
Ila Kwa mwaka 2026, gap hilo limepungua na kuwa 3 us dollar trillion
Lakini hilo issue sana
Issue ni Kasi ya ukuwaji wa uchumi, IMF inakadiliwa ifikapo mwaka 2026 Kasi ya ukuaji wa uchumi wa marekani itaporomoka na kufikia 1.6% kutoka kwenye 3.5%
Wakati upande wa china Kasi ya ukuaji wa uchumi itashuka na kufikia 4.8% kutoka 5.57%
Sasa Kwa mwaka 2022 marekani imepigwa gap la Kasi ya ukuaji Kwa kiwango Cha 2.07% wakati Kwa mwaka 2026 marekani itakuwa imepigwa gap la ukuaji wa uchumi Kwa kiwango Cha 3.2%
Hii inaonesha kuwa kadri miaka inavyokwenda Kasi ya ukuaji wa uchumi wa marekani inasinyaa wakati Kwa upande wa china inaonekana kuchanua hivyo unaweza ukakadilia Kwa takwimu hizo ifikapo 2030 huenda china ikaizidi marekani kiuchumi
Na ukishakuwa mbabe upande wa uchumi ushawishi wako unaongezeka hivyo unakuwa na nafsi kubwa ya kuwa super power wa Dunia kama alivyo marekani sasaivi
Sasa kupitia hilo marekani haitaki kukubali kuja kuwa chini ya yoyote na haipo tayari itafanya Kila lowezekanalo kuhakikisha hilo halitokei, na ndio maana binafsi naona china Bado haijakwepa mtego wa marekani
Lazima marekani ifanye juu chini kuhakikisha china inaingia kwenye mgogoro ili ukuaji wake kiuchumi ushuke, kwahiyo ili china iingie kwenye mgogoro marekani ataishawishi Taiwan ijitangazie uhuru wake alafu tuone kama china ataivamia Taiwan
Kama china ataivamia Taiwan maana yake malengo ya marekani yametiki
Ila kama hataivamia Taiwan maana yake amekubali kuipoteza na kama ataipoteza Kwa kuiacha taiwan iwe huru, basi tutamuona marekani akipeleka Kambi za kijeshi na kumwaga silaha Kali Kali na hivyo kuwa mwiba Kwa usalama wa china
Kwahiyo china inawakati mgumu sana wa kimaamuzi ngoja tuone itaamuaje
Nini maoni yako?
C$p kutoka fb Archimedes justine
Sent using
Jamii Forums mobile app