Nashukuru bro kwa hiyo Compliment, Shukran Mucho ha ha eti kama Mapacha 😂😂😂
Nasikia hawa wote
Qibsyl na
Galip Vrl ni mtu mmoko 🤔😊. Anyway tuliache hilo.
Issue yetu ya China kwa Taiwan naona kidogo natofautiana na wengi including yeye mwenyewe bro
Galip Vrl
Najua kidogo kwenye Geopolitics ni all about "Uvumilivu na subra", kisha hekima na Busara nyingi.
China (Of course na mwenzie Russia) kua threat kwa yule ambae tunamzania na amekua akituaminisha hivyo kua yeye ni Superpower (US) sio kwa bahati mbaya. Inside wanajuana zaidi ya vile sisi tunavyowasoma kwenye mitandao.
Ile chess Move ya jana mie naiunga mkono kwa analysis zangu binafsi. Na kwa details chache nilizonazo juu yao.
US anapenda vita sana ambazo zinapiganwa mbali na mipaka yake. Na Historia yaonesha haisogelei kichwa kichwa nchi ambayo anaona inaweza kupeleka madhara kwenye ardhi yake. Kwa wakati mfupi, hapa sina maana kama China hawezi fikisha madhara kwenye ardhi ya US ila swali nani atamtangulia mwenzie?
Kuna nukta ukizitizama vizuri bado inanishawishi kuuamini mtizamo wangu nilio nao kwenye hili swala. Juu ya kufunga bakuli langu 😂 nisubiri dakika ya mwisho nitapata la kuzungumza.
Em fikiria visit ya Pelosi haiku ainishwa kwenye ratiba yake na US wakatamka hadharani kua hatofika, ila kaenda means hiyo ilikuwa inapangwa kimya kimya so maandalizi walikuwa nayo ya kutosha. Ingawa hili ni jambo la kawaida kwa US kuzungumza hivi halafu wakatenda vile.
Pale China karibu kila kona kazungukwa na vibaraka wa US, Ambapo US katia base zake. So kitendo cha kuanzisha tu ingekua ni karata mbovu kwake kurudisha mashambulizi kutoka pande hizo.
First and second world war vimewapa fundisho mataifa mengi yanayojielewa namna ya kudeal na mizozo level ya International. Hawaipeleki kitoto na kimhemuko.
Mda mwingi US na China wamekua kama Master na Slave wake, US akiwa mtoa order na China akiwa mtimiza order. Ila katika hilo US akajisahau hadi sasa imefika wakati ambao Master hana uwezo tena wa kuamrisha kwa Slave wake zaidi ya kumuharibu wakose wote.
Ni kipindi kirefu China kamjengea mazingira tegemezi US ambayo ni ngumu kwake kuchomoka.
Fikiria kampuni kama Apple, 19% ya faida wanayoipata inatoka China. Investors wa hii kampuni watakua radhi China ashambuliwe? Ukiacha mbali faida wanayopata suppliers wao wa materials ni hao hao China. Je nini kitatokea vita ya Uchumi baina yao? Huo ni mfano wa kampuni moko tu.
Mfani mwingine mmesikia hapo, TACL kuhusu kusitisha mradi wao wa kiwanda cha mabetri ya Gari ya Tesla na Ford. Hii ndio Supply chain niliyokua naisemea, Last consumer huwa anabeba final products made in dash dash bila kufikiria vilivyotengeneza anachokitumia vimetoka wapi.
Kibaya zaidi China ana bidhaa za aina zote, from cheap to high expensive, from low quality to high quality means anaweza kufanya biashara na jamii yoyote taifa lolote na watu aina zote duniani wenye nacho na wasio nacho.
Hapa tutamkuta Afrika, USA, EU, South and Latin America yani kila kona ya Dunia na kila bidhaa anaipeleka kulingana na soko husika. Tofauti na mshindani wake ambae anafanya biashara kwa specific countries ambazo we all knows ni EU na pale Middle east.
Katika kipindi ambacho EU inapitia mazito hadi kwake US ana suffer kwa matukio aliyotengeneza mwenyewe.
So nje ya Vita ya Silaha, China ana kila karata ya kuiadabisha US. East hakuna magasho kiwango cha SGR kuna watu wafupi ila wako makini. Matendo yao tunaweza kuona ni kama waoga ila wana plan konki linapokuja usukwaji wa matukio.
Tuupe mda nafasi yake tuna mengi ya kuzungumza.
Utakuwa unafiki kutetea kitendo cha Russia kujiondoa KIYV licha ya ule msafara wake wote alio uweka at the same time kuiponda response ya China despite mkwara alio uonesha. Hilo sakata la Taiwan halijaisha ndio kwaaanza linaanza.
Tukaeni kati tuenjoy show, Geopolitics ni mchezo unaohitaji utulivu wa hali ya juu tuweze kuuelewa.