Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Dah Asante kiongozi kwa kunipa sifa.nami nazipokea,kwa sababu wewe ni moja ya vichwa makini sana humu jamvini.kupewa heshima hiyo na kichwa kama wewe ni heshima kubwa sana kwangu.

Nyongeza kwa Nini sisi wengine tunaiunga mkono Urusi kwa "baadhi" ya mambo yake.

Wakati wa ukoloni USA ilikua ndio rafiki mkubwa wa wakoloni,watesi wetu.
Viongozi wa Afrika wa wakati huo akina Nyerere,kwame Nkuruma,Patrice Lumumba,Keneth Kaunda,Robert Mugabe,Govan Mbeki,Nelson Mandela,Sam nujoma,Augustine Neto,Samora Machel,Jose Eduardo Dos Santos na wengi wengineo walianzisha harakati za kujikomboa kutoka makucha ya wakoloni.
USA Alikua alizisapoti nchi wakoloni kwa Hali na Mali,mbali na wakoloni aliwasapoti watawala wa Afrika ya kusini na Namibia ambao walikua ni makaburu.hawa walikua na mkono wa chuma zaidi hata kuishinda wakoloni wenyewe.
Walikua makatili,kwa kuua watu weusi,kubaka,kupiga,kufunga,kuwabagua na Kila aina ya mateso ikiwa ni pamoja na kuchoma nyumba zao.
Weusi wakaanzisha vikundi vya kujilinda na kudai uhuru na haki zao.

Nguvu za Urusi kijeshi,silaha na mafunzo.

Hakika nakuambia kama sio Urusi Hadi Leo Makaburu na wakoloni wangeendelea kutawala kwa mukono ya chuma.

Weusi waligundua kuwa Makaburu na wakoloni hawaelewi kabisa lugha za diplomasia na majadiliano ya kudai haki na uhuru wa mtu mweusi.
Lugha pekee ambayo wakoloni na Makaburu wangeielewa na kweli waliielewa sana,ni mtutu wa bunduki,vita,mapigano na ubabe.
Makaburu waliwahi kuua wanafunzi weusi wa shule kwa risasi.
Kilichofuata ni ukiua mtu mweusi na mweusi anaua mweupe.
Makaburu wakwa wanatumia uwezo wao wote wa kijeshi silaha na ujasusi na msaada kutoka UK,Israel,USA na France na German,.weusi wakawa wanazidiwa.
Hapa ndipo Urusi ikaingilia kati kwa kutoa misaada ya mafunzo,silaha,fedha,elimu,hifadhi na Kila kitu kwa wapiganaji wa kiafrika kutoka nchi yoyote ya Afrika iliyohitaji msaada wa namna hiyo.
Sio TU Urusi Bali Cuba,china na nchi nyingi za kisoshalist na kikomunisti ziliwasaidia watu.weusi kutoka na madhira ya Makaburu na wakoloni na hatimae Makaburu na wakoloni walishindwa kwa msaada wa Warusi.
Urusi pia ilisimama kidete huko umoja wa mataifa kuweka maazimio,mashinikizo na mapingamizi ili kuhakikisha wakoloni na Makaburu wanashindwa na walishindwa kweli.
Urusi ilijenga vyuo vya ufundi Tanzania mfano huko mbeya Kuna chuo matata sana Cha ufundi, na nchi nyingine za Afrika,
Ilisaidia kuyajenga majeshi ya Tanzania kisilaha na miundombinu ya kijeshi,mafunzo na mengi mengineyo.
Rubani mmoja matata sana na WA kipekee wa Kitanzania aliejifunza Urusi na kupata mafanikio makubwa sana ,alielisambaratisha jeshi la nduli Amini na baadae kuwezesha kujengwa kwa chuo imara kabisa Cha jeshi la anga Bora kabisa la Tanzania ni CDF (RTD)Robert Philemon Mboma,huyu mwamba pamoja na kusomea nchi nyingine Alipata kusomea Urusi.
(Kama Kuna makosa hapa Naridhia kusahihiswa)

Urusi hua Haina misaada yenye masharti kama wengine.
Urusi ni rafiki wa kweli kwa Waafrika.

Ule ugeni wa Rais wa USA wa wakati ule, George Bush ulipo kwenda kutembelea nchi moja ya Afrika kwa mbwembwe,walifanikiwa kuzima rada zote, wakati ndege ya Bush ilipoingia katika anga la nchi ile,lakini rada moja walishindwa kuizima, ambayo kwa kweli ni rada iliyotengenezwa Urusi.(made in Russia)
Naomba niishie hapa kwa Leo.
Wewe ni mtu mzima nadhani utakua umeielewa nchi hiyo.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘Kwako mtoa hoja,
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘Kwa Hawa πŸ‡·πŸ‡Ί mabingwa,
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘KwaπŸ‡ΉπŸ‡Ώkuwa na mtoto kama wewe,kichwa.
 
Mwanangu Galip Vrl atanisaidia kutoa muongozo.
Ile link basi mie nimeiona nikajua wamfanyia masihara πŸ˜‚, hiyo link kama ulitype kimasihara basi jua sio legesha bali genuine link ya WWE, World Wrestling Entertainment maarufu huku kwetu tumezoea kusema "Mieleka". Kuleee tuliko pata kumjua John Cena na wengineo WWE.COM

haha Galip Vrl katika ubora wake with his sarcasm. thats below the belt to ukronazis and khohols cum sim 2 defenders. haina comeback
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ila lakini si niliwaambia wajomba, tuna mchambuzi wetu wa US tawi la JF aliwahi zungumza hivi na vile.

Na hapo tumemtekenya kidogo tu katekenyeka bwelele πŸ˜‚

That's why nawaambia huwa na enjoy sana nikiwa hapa... Ni cheko kwenda nyuma mbele kuna matope AF.
 
pro-russians, i salute u guys. u always reminds me of my late grandfathers. He always oozed wisdom May He Rest in Peace alinifunza mambo mingi sana kuhusu west and east asian countries. . Before he died he said to me Gorbachez alikosea dunia. africa wakati wa cold war tulikuwa mrembo wakupiganiwa na milengo yote mbili..am happy history now is repeating itself(courtesy of putin)
 
Simtoke huko muwaachie nchi yao, muungano wenyew sio muungano bali mnawakolonia. Hawawataki acheni kupeleka mbarig zenu huko
 
Pro-nato rafiki yenu Zelle ameukubali mziki wa Russia .

Volodymyr Zelensky's evening address.

"The situation in Donbas remains very difficult. Our army is doing everything possible to stop the Russian terror and inflict the greatest possible losses on the occupiers. Avdiyivka, Pisky, Maryinka, Bakhmutskyi and other hot areas in the Donetsk region take the main efforts and, unfortunately, many lives. It is also difficult in the Kharkiv region, in the south of our country, where the occupiers are trying to concentrate their forces."

So it’s bad everywhere? lol this is gentle easing into we lost territory.
 
Sasa hivi kakaliwa kooni..,kama nawaona west wanavyoiendesha hii vita kwa remote control [emoji41]
Alitumia ubabe badala ya akili.
Anaona aibu kujitoa.Akujifunza vita vya afghanistan alidhani anapigana na taliban kumbe anapigana na USA kama ilivyo Ukraine.
 
Hii story nilisoma na nilishachangia miaka iliyopita, ukiimaliza story nionyeshe meli ya Marekani iliyozama vitani. Nami nakuonesha Moskva iliyopigwa na Ukrainian made missile, watu wazembe ambao hata kwenye top ten world arms industry hawapo. Hapo tutajua nani ana ulinzi imara wa meli zake.

After that nakuonyesha Sukhoi ikiwa na Khibiny yake na bado ikapigwa na outdated Buk missile. Ndege zina Khibiny ila zinaogopa hata MANPADS
 
Uko sahihi Jomba, hizo propaganda za Kremlin tu hazina maana. Halafu hiyo Washington Post nahisi itakuwa ya pale rangi tatu mbagala. Hawana tofauti na Joti TV.

Wanaanzaje kuifananisha Aegis na vitu vya ajabu in your Voice πŸ˜‚πŸ˜‚.

Anyway asante kwa kutufumbua macho jomba. The only commander in chief we knew ndio ushasema sie wakina hadi tupinge πŸ€”πŸ€—? Tumekuelewa mazee!
 
Hiyo link ya Washington Post walikotoa taarifa iko wapi. Mbona taarifa ilitolewa na redio ya Russia. Washington Post ndio primary source? Aliyesema hayo yote ni Russia, na US hakutolea taarifa za uchochoroni kama hiyo.

Naomba hiyo link ya taarifa yako nione maajabu. Nakusisitiza ndege zenye Khibiny zinapigwa pale Ukraine kwa kutumia Buk na MANPADS. Russia inayodaiwa kufanya electronic countermeasures kwa USS warship isingeshindwa kufanya kwa silaha nyingine ndogo na zamani vile. Hata satellites na mfumo mzima wa Starlink umewashinda Warusi. Sasa unashindwa kazi ya mhuni Elon Musk uje uweze kazi za kina DARPA, Lockheed Martin, Raytheon
 
Wewe jamaa inaelekea unajua sana madhaifu ya vifaa vya kirusi ..tutengenezee basi hata Tanzania mfumo mmoja mana unabeza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…